Naombeni msaada wa kisheria kuhusu mikataba

Ragna

Member
Jan 22, 2017
50
16
Habari wakuu. Poleni na majukumu.

Kuna rafiki yangu ametumika kama mzamini wa mtu fulani ambae alikopa kwenye hizi Microfinance Institute na huyo aliyekopa amekimbia, sasa burden ya kulipa deni imemwangukia mzamini.

Lakini mimi kama mimi nimejaribu kupitia huo mkataba wa yule jamaa aliekopa sijaona STAMP inamanisha uko mkataba auna stamp duty atuwezi kutumia kipingele hicho kwenye mkataba kama invalid contract na muanga akagoma kulipa hilo deni baada ya mkopaji kukimbia.

Msaada wa watalaam wa sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stamp duty siyo kigezo katika Maswala ya kimkataba, ila katika tafsiri nyepesi mdhamini katika mkataba si mkopaji bali ni shahidi anae kaa kama uthibitisho au mtu anaye mtambua mkopaji.

Majukumu au wajibu wa mdhamini katika mikataba ni;

1. Kutoa uhalisia au ukweli wa namna ya mambo yaliyo kubalika katika mazingira ya kimkataba kwa chombo cha sheria Kama itafika huko.

2. Kuwa daraja kati ya mkopaji na mkopeshaji ambapo katika mazingira hayo anaweza kuwa muwasilishaji wa mchango au kiasi kilicho paswa kurejeshwa kulingana na makubaliano husika, Kama mkopaji atakuwa labda ametingwa na majukumu mengine kurahisisha jambo akaona vema ampe mdhamini kiasi kifike mahala husika.

3. Mshauri kati ya pande mbili za mkataba.


Note.....!!!

Madeni ya kimkataba huwagusa moja kwa wahusika wa pande mbili za mkataba na katika mazingira hayo mdhamini hawezi kuwajibika kwa namna yoyote ile kwa kitu alicho kaa au simama Kama shuhuda ila ingekuwa amemdhamini mtu kwenye makosa ya jinai na mtuhumiwa akatoroka hayo ndo makosa anayowajibika mdhamini aidha katika kumtafuta mtuhumiwa au kilipa faini ya fedha iliyo andikwa katika hati ya udhamini.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stamp duty siyo kigezo katika Maswala ya kimkataba, ila katika tafsiri nyepesi mdhamini katika mkataba si mkopaji bali ni shahidi anae kaa kama uthibitisho au mtu anaye mtambua mkopaji.

Majukumu au wajibu wa mdhamini katika mikataba ni;...
Nadhani umechanganya kati ya mdhamini na shahidi. Shahidi wajibu wake ni kushuhudia na kutoa uhalisia wa mkataba atakiwapo kufanya hivyo iwapo utatokea mkanganyiko. Mdhamini itategemea mkataba umeandikwaje,

kuna baadhi ya mikataba inaweka masharti kwamba iwapo mkopaji atashindwa kulipa (kwa sababu yoyote au kama itakavyokubaliwa) basi mdhamini atawajibika kwa kiasi fulani au kwa mkopo wote.

Hivyo mdhamini ni zaidi ya shahidi, majukumu ya mdhamini yanategemea sana mkataba umeandikwaje
 
Kama nimekuelewa sawia,

1. Soma mkataba unampa wajibu gani mdhamini.

2. Kukimbia kwa mdeni hakupelekei moja kwa moja wajibu wa kulipa deni kuhamia kwa mdhamini.

3. Iwapo mdeni kakimbia, kwanza mdhamini ana wajibu wa kusaidia kupatikana kwa mdeni, ikiwemo vielelezo kutoka serikali za mtaa, polisi n.k

4. Iwapo jitihada zote zimegonga mwamba, basi mdhamini atakuwa na wajibu wa kulipa deni lililobaki (japo sio lazima kwa utaratibu wa mdeni, anaweza kuomba utaratibu mwingine) kwa sababu wajibu wa awali haukuwa wa kwake. Wajibu wake uliishia kwenye "dhamana".

NB: Nielewavyo mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom