Naombeni msaada wa kisheria kuhusu hili jambo langu

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,072
1,697
Habari za usiku huu wadau, nimeandika bandiko hili ili kuomba msaada wa kisheria kwa mtu yeyote yule mwenye uwelewa wa sheria!

Mimi nina mshikaji alinipa pesa tufanye biashara fulani hivi, ile pesa kweli ikaingia kwenye biashara kwa bahati mbaya ile pesa ikakata sehemu kubwa tu.

Sasa jamaa nilipomuelekeza akawa mkali nikamwambia basi kama vipi mimi nitakulipa pesa yako, kwa kuwa pesa ilikuwa nyingi kama M 5 hivi nikalipa mpaka M 4.2 bado ananidai kama 800 hivi.

Sasa kulingana na hali halisi ya hili gonjwa jamaa anadai anataka kwenda kunifungulia kesi ya wizi wa kuaminika sasa ninavyojua mimi haya ni madai sasa kwa nn anifungulie kesi ya wizi wa kuaminika?

Sasa kisheria natokaje hapo kwenye iyo kesi ya wizi wa kuaminika!

Nisaidien tafadhali
 
1. Wakati mnapeana pesa mliingia makubaliano yaani mkataba?

2. Wakat mmekubaliana kumrejeshea pesa zake mlikubaliana kwa maandishi?
Na mlikubaliana kumrudishia kwa muda gani?
Kila ulipokuwa ukimrudishia hela ulitumia njia gani?
Mlipeana mkononi? Ulimtumia kwenye simu? Ulimuingizia bank au ulitumia njia gani?

3. Taarifa ya kukufungulia mashitaka kwa kosa la wizi wa kuaminika amekupa kwa kutumia njia gani?
Amekwambia kwa mdomo au amekuletea barua?

Tuanzie hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom