Naombeni msaada wa kisheria jamani haraka

KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,822
2,290
Kuna jamaa yangu mmoja allinipa kazi ya kumtengenezea blog makubaliano yakiwa laki na ishiri blog yake ikiwa tayari, na tulikutana tu kwa njia ya mtandao. lakini baada ya kumaliza kutengeneza blog hakuonyesha dalili za kunilipa fedha yangu.

Nikaamua kutumia uungwana tu sikumgasi hata kidogo. baada ya siku chache akaniambia anatafuta computer ya kununua nikamtafutia komputer ambayo makubaliano ilikuwa tulipane laki mbili kwa awamu.

Wiki ya kwanza laki na wiki ya pili laki iliyobakia, lakini alinipa elfu 90 tu kwa wiki mbili na kwa usumbufu mkubwa sana.

Mimi nikaamua kuahirisha biashara nikachukua computer yangu kwa makubaliano yakuwa baada ya mda kidogo nikipata mteja mwingine nitamrejeshea kiasi chake cha pesa alichokilipa.

Ajabu baada ya siku mbili tu kaja kunidai hela tena kwa nguvu zote, mimi nikamjibu sina hela yakukulipa kwasasa.

Alipoona hamna dalili ya kupata pesa yake akaamua kwenda kwa mjumbe.
nayeye ni mkazi wa ubungo lakini kaenda kaja kwa mjumbe wa huku mtaani kwangu G/Mboto

Nilipooona kaja na mjumbe nikaelewa sasa nikikubali kuwa nadaiwa itabidi tuweke maandishi, nasikupenda iwe hivyo kwakuwa hatukuanza kisheria kuuziana.
nimeamua kumkana kusema sijamuuzia computer na wala siuzi computer na sifanyi biashara ya kuuza computer.

Wajumbe walipoona nimemkana na imeshindikana wameondoka na kwenda kumuandikia barua ili kesi iende polisi.

Sasa nauliza je kama nikienda mahakamani nikasimamia hoja yangu ya kutokuuza computer na wala sifanyi biashara hiyo naweza kutiwa hatiani?

Na jamaa yeye anamashahidi ambao wameniona nikiwa naibeba hiyo computer nikimpelekea na hata nilipoenda kuibeba na baadhi wanajua yakuwa nilikuwa naiuza.
sasa je naweza tiwa hatiani bado?

Na biashara mwanzo mwisho haina maandishi ya aina yoyote ile mpaka sasa.

Naombeni ushauri wana jamiiforums
 
Hahahahaahahah umenichekesha sanaa, nlitaka kukusaidia hapa kisheria ila nimeogopa uhuni wako uliomfanyia huyo jamaa. Hahahahahaa mtajuana wenyewe huko.
 
Tafuta 90 yake mpe mbele ya mjumbe yaishe.
Huo ndio ushauri wangu. Utakaa selo usipozingatia na hata ukishinda kesi utakuwa umepoteza muda
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom