Naombeni msaada wa haraka niokoe maisha ya baba yangu Hospitali ya Muhimbili

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
546
773
Wapendwa Habari za jioni,

Niko Muhimbili Emergency hapa nimemleta baba yangu anapata Changamoto ya upumuaji kawekewa oxygen toka saa 8 na sukari yake iko juu sana over 20 ila haijaguswa hadi muda huu.

Shida ninayopata imetokea tu bahati mbaya Manesi wamemchukia sana kiasi sijajua kwanini na nahofia wanaweza kumuua nikiondoka. Nurse aliyekuwa Day leo alimpenda sana hata pampasi alituambia tununue atamvalisha, ila aliyeingia Night kamchukia sana hata sisi kumlisha imekuwa shida ana visirani na Mgonjwa hadi naogopa sijajua amewakosea nini wakati hata kuongea hawezi. Nitamtaja jina lake baadae na vitendo anavyomfanyia na Afroking zake.

Niko kwenye wakati mgumu sana niko kwenye Taasisi ya Serikali ambayo inaweza ku-influence nikasaidiwa haraka sana kwa maelekezo kabisa ila nahofia nikiitumia nafasi yangu watanijua na wanaweza kummaliza kwa style nyingine.

Niko kwenye wakati mgumu sana naombeni msaada, ushauri na maoni yatakayoweza kusaidia kuokoa uhai wa Mzee wangu.

UPDATE:
Mzee wangu alifariki,nilipambana kwa jitihada zote nilizoweza sijutii hata kidogo ingawa nyingine zilileta matokeo hasi nyingine chanya ila naamini kuwa Mungu alipanga siku yake iwe hiyo changamoto za kibinadamu zimechangia tu.

Bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwa wauguzi,kubwa sana nimejifunza mambo mengi sana ila nashukuru na kusamehe ntatimiza wajibu wangu kwa namna nyingine kusaidia taifa langu.

Nawashukuruni sana mlionishauri na mlionikejeli na kunitukana pia kwenye wengi kuna mengi,nilifanyia kazi yale ambayo Mungu aliniwezesha kuyafanyia kazi kutoka kwenu.Asanteni sana.

Mungu ailaze roho yake kwa amani.
 
Hamna watu wanaopitia maisha magumu kipindi hiki cha Corona kama wagonjwa wa Kisukari

Mungu awasaidie, maana Madaktari wengi kwasasa wanawakimbia, kwa kuhofia kua shida yao ya kupumua,imetokana na Corona, kumbe unakuta, Sukari imepanda, mgonjwa kapatwa na komplikesheni.

Hatimaye Anaga Dunia.

Jambo lako, halitopishana na la huyu mama, kama na endapo tu, Hutochukua Hatua madhubuti

Screenshot_2021-02-10-23-21-22.jpg
 
Wewe unauguliwa na mzee wako hali yake mbaya na unasema unanafasi serikalini unasubiri nini kuitumia? Tumia hiyo nafasi kama ni kweri muite muonyeshe kitambulisho huyo mhusika na jifanye unamuomba msaada ataogopa na ata musaidia mzee wako acha kuzembea.
 
Wewe unauguliwa na mzee wako hali yake mbaya na unasema unanafasi serikalini unasubiri nini kuitumia? Tumia hiyo nafasi kama ni kweri muite muonyeshe kitambulisho huyo mhusika na jifanye unamuomba msaada ataogopa na ata musaidia mzee wako acha kuzembea.
Hiyo ndio sehemu muafaka ya kutumia nafasi. Lkn nafasi tunazitumia kuwanyanyasa walio chini yetu maofisini, kuchukua wake za watu maofisini, kutisha majirani, kujitutumua kwenye bar na kuwabambikia watu kesi.
 
Hizi si ndio hospitali zinazosifiwa kwa huduma ! sasa fanya hivi , mhamishe huyo mzee mpeleke Agha Khan halafu tupatie jina la huyo ofisa wa hospitali mwenye chuki haraka sana tufanye kazi .

Liwalo na liwe
Manina zake huyo nesi huyo bwana atakuwa afisa kipenyo aweke kitambulisho mezani mzazi ashughulikiwe mapema. Wanavyo chelewa kumpa huduma mzee ndivyo itakavyokuwa ngumu kwa mzee kurudi katika hali yake ya kawaida.

Pole sana kamanda.
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom