Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 549
- 781
Wapendwa Habari za jioni,
Niko Muhimbili Emergency hapa nimemleta baba yangu anapata Changamoto ya upumuaji kawekewa oxygen toka saa 8 na sukari yake iko juu sana over 20 ila haijaguswa hadi muda huu.
Shida ninayopata imetokea tu bahati mbaya Manesi wamemchukia sana kiasi sijajua kwanini na nahofia wanaweza kumuua nikiondoka. Nurse aliyekuwa Day leo alimpenda sana hata pampasi alituambia tununue atamvalisha, ila aliyeingia Night kamchukia sana hata sisi kumlisha imekuwa shida ana visirani na Mgonjwa hadi naogopa sijajua amewakosea nini wakati hata kuongea hawezi. Nitamtaja jina lake baadae na vitendo anavyomfanyia na Afroking zake.
Niko kwenye wakati mgumu sana niko kwenye Taasisi ya Serikali ambayo inaweza ku-influence nikasaidiwa haraka sana kwa maelekezo kabisa ila nahofia nikiitumia nafasi yangu watanijua na wanaweza kummaliza kwa style nyingine.
Niko kwenye wakati mgumu sana naombeni msaada, ushauri na maoni yatakayoweza kusaidia kuokoa uhai wa Mzee wangu.
UPDATE:
Mzee wangu alifariki,nilipambana kwa jitihada zote nilizoweza sijutii hata kidogo ingawa nyingine zilileta matokeo hasi nyingine chanya ila naamini kuwa Mungu alipanga siku yake iwe hiyo changamoto za kibinadamu zimechangia tu.
Bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwa wauguzi,kubwa sana nimejifunza mambo mengi sana ila nashukuru na kusamehe ntatimiza wajibu wangu kwa namna nyingine kusaidia taifa langu.
Nawashukuruni sana mlionishauri na mlionikejeli na kunitukana pia kwenye wengi kuna mengi,nilifanyia kazi yale ambayo Mungu aliniwezesha kuyafanyia kazi kutoka kwenu.Asanteni sana.
Mungu ailaze roho yake kwa amani.