Naombeni msaada na ushauri kuhusu solar...

Betri ya N100 ni sawa na 12V ......AH ngapi ?
N100 ndo AH 100 MKUU.
yes Ni 12v na full system ni 12v.

Charger controla niliweka ila haikuwa bora kwangu niliitoa.
Ni Sundar 30A Ina 60,000.
15712956202443416387553781174535.jpg
15712956530346159130040838009396.jpg
 
Hizi solar za kununua dukani ukalipa cash wanakuingiza mkenge utaitumia kwa muda inaharibika. Kuna kampuni inaitwa ZOLA! Kwa mtambo wenye thamani ya laki Tisa, unalipa 72,000 wanakuja wanakufungia na wanakupa mkopo wa kulipa kwa miaka 3. Nimeutumia miaka 2 sasa haujawahi kuzingua wala taa kuharibika.
Mtambo kama huo wa laki 9 unawasha taa ngapi na socket ngapi mkuu
 
Je solar yako imefugwa pamoja na charger contoller? Hii inasaidia kucotrol kiasi cha power kinachopaswa kuingia kwenye battery ili isiwe over charged ili betri idumu kuna wengine wanafunga direct hio so sawa huenda betr imeshakuwa na shida lakini pia lingine angalia connection kutoka panel kwenda kwenye chaji na pia kutoka kwenye chaji kwenda kwenye taa kama zipo sawa.
Hapa kwenye kufunga Direct bila kutumia controller, nadhani inaweza kuwa na hatari zitakazojitokeza mapema sana. Au pia inakubalika?
 
mm naungana na mafundi wote waliokuja kukuangalizia ila kingine aujasema kama unatumia charger controller.. nimetumia betri nying sana ila betri nliyokuja kuipenda n sunder ingawa nayo sukuiz ivyo betri 18Ah aifai kwa invetor mana amp zake ndogo inawah kukata moto inatakiwa uchajie sim kwa Dc na taa Dc ila kuchaj sim yako tu kwa biashara
Heshima kwenu wakuu !
Nipo kijiji fulani nyanda za juu kusini...natumia solar tangu Jan
Nilinunua betri mpya ya Sundar yenye ukubwa wa 12V 18 AH/ 20HRS na Panel ya Watt 20 nikawa natumia taa 1 na kuchaji simu pekee
Mwezi wa 4 nikaongezea taa 4 (za Watt 3 mbili na Watt 2 mbili)

Mwanzoni mwa mwezi huu ikaanza shida ikawa haiawki kabisa nikaita fundi akasema betri ni ndogo kuliko matumizi ikachokonoa ikawa fresh
Baada ya siku 3 tatizo likarudi vilevile akaja fundi mwingine akadai betri sio tatizo ila waya tu akachokonoa ikawa fresh ila now haiwaki tena

Wataalamu mnahisi tatizo nini ?
Na je nitafute betri au niongeze panel ya Watt ngapi ?
Matumizi yangu ni :
1/kuchaji simu
2/Taa 5 za Watt 3 ila huwa nawasha 4 na kulala naacha mbili tu

Natanguliza shukrani
 
mm naungana na mafundi wote waliokuja kukuangalizia ila kingine aujasema kama unatumia charger controller.. nimetumia betri nying sana ila betri nliyokuja kuipenda n sunder ingawa nayo sukuiz ivyo betri 18Ah aifai kwa invetor mana amp zake ndogo inawah kukata moto inatakiwa uchajie sim kwa Dc na taa Dc ila kuchaj sim yako tu kwa biashara
Mkuu sikuweka solar controller
Betri ya 18AH inanitosha kabisa coz matumizi yangu ni madogo taa 5 lakini inayotumika zaidi ni 1 ndani chumbani, sebuleni situmii sana, nyingine chumba cha wageni (hii haitumiki hadi iwepo sababu)
Kwahiyo taa mbili tu za nje ndo zinatumika zaidi

1)Nimesoma ushauri wa wadau hapa nimeamua kwamba nitanunua betri mpya ya juu ya 18AH na panel ya kuzidi 20W na charge controller

2)km nikishindwa basi nanunua tu betri size hii hii ya 18 AH na controller tu halafu nitakuwa na nidhamu ya matumizi kwanza nitaweka taa za 1W badala ya 3W
 
Hizi solar za kununua dukani ukalipa cash wanakuingiza mkenge utaitumia kwa muda inaharibika. Kuna kampuni inaitwa ZOLA! Kwa mtambo wenye thamani ya laki Tisa, unalipa 72,000 wanakuja wanakufungia na wanakupa mkopo wa kulipa kwa miaka 3. Nimeutumia miaka 2 sasa haujawahi kuzingua wala taa kuharibika.
Hizi kampuni za kukopesha solar ni kama BAYPORT au hizi taasisi za kukopesha watumishi pesa halafu mwisho wa siku mtu analipa mara3 ya alichokikopa. Mtoa mada sikushauri ukakope sola. Utalia kilio cha mbwa koko. Nimewaona watu wengi sana vijijini waliokopeshwa sola wanavyoteseka kwa kunyonywa na hizi kampuni oama Mobisol, Zola etc. Mimi nimenunua solar kubwa ya 200W betri N180 pamoja na inveter na charge control na taa 10 kwa TSh.950,000/= made in German. Lakini kuna jirani alikopa mtambo kama huo akalipa 450,000 kianzio na sasa kila mwezi analipa 60,000 kwa muda wa miaka minne.
 
Heshima kwenu waungwana,

Natumia umeme wa solar una betri la 12V 33Ah nimefunga pamoja na controller na panel ya Watt 40
Taa zinawaka bila shida

Kuchaji simu chaja naweka direct kwenye betri sasa kuna tatizo tangu juzi nikiweka tu simu inagoma na simu kuandika CHARGER IS OVERVOLTAGE PLEASE DISCONNECT THE CHARGER .....Nikaamua kununua chaja mpya nikifikiri tatizo ni chaja ila shida ipo palepale

Hii ishu tatizo nini?
Nifanyaje kulitatatua hii ishu?

Nitashukuru msaada wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima kwenu waungwana,

Natumia umeme wa solar una betri la 12V 33Ah nimefunga pamoja na controller na panel ya Watt 40
Taa zinawaka bila shida

Kuchaji simu chaja naweka direct kwenye betri sasa kuna tatizo tangu juzi nikiweka tu simu inagoma na simu kuandika CHARGER IS OVERVOLTAGE PLEASE DISCONNECT THE CHARGER .....Nikaamua kununua chaja mpya nikifikiri tatizo ni chaja ila shida ipo palepale

Sent using Jamii Forums mobile app
Battery inatoa DC current na voltage, simu inatumia AC current!! MBONA SIONI LOGIC YA UNACHOFANYA MKUU?

Nnachojua kama unatumia vifaa vya AC ni lazima uwe na inveter itayo badili umeme umeme wa DC kwenda AC!! ndipo uweze kutumia kwenye vifaa vya AC ikiwemo hiyo simu yako1!

NB: Ngoja wadau waje kwa msaada zaidi!!
 
Hizi kampuni za kukopesha solar ni kama BAYPORT au hizi taasisi za kukopesha watumishi pesa halafu mwisho wa siku mtu analipa mara3 ya alichokikopa. Mtoa mada sikushauri ukakope sola. Utalia kilio cha mbwa koko. Nimewaona watu wengi sana vijijini waliokopeshwa sola wanavyoteseka kwa kunyonywa na hizi kampuni oama Mobisol, Zola etc. Mimi nimenunua solar kubwa ya 200W betri N180 pamoja na inveter na charge control na taa 10 kwa TSh.950,000/= made in German. Lakini kuna jirani alikopa mtambo kama huo akalipa 450,000 kianzio na sasa kila mwezi analipa 60,000 kwa muda wa miaka minne.
Kampuni ipi ya ujerumani ndugu ili tufuate nyayo maana ni bei nzuri. Na je naweza kunyosha nguo?
 
Battery inatoa DC current na voltage, simu inatumia AC current!! MBONA SIONI LOGIC YA UNACHOFANYA MKUU?

Nnachojua kama unatumia vifaa vya AC ni lazima uwe na inveter itayo badili umeme umeme wa DC kwenda AC!! ndipo uweze kutumia kwenye vifaa vya AC ikiwemo hiyo simu yako1!

NB: Ngoja wadau waje kwa msaada zaidi!!
Sijakuelewa vizuri mkuu
Hiyo ni solar chaja angalia vizuri
Ina maana nimekosea kuchajia hapo ?
Suluhisho ni nini ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijakuelewa vizuri mkuu
Hiyo ni solar chaja angalia vizuri
Ina maana nimekosea kuchajia hapo ?
Suluhisho ni nini ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ulinunua chaja za kawaida jua inatumia ime dizainiwa kutumia umeme wa AC (TANESCO) kabla ya kuichomeka kwenye battery ilikua lazima ubadilishe umeme wa battery (DC) uwe umeme wa AC (umeme wa tanesco) ndio uweze kutumia kwenye chaja yako!!

Ulicho fanya ni sawa na kuchanganya maziwa na dawa ya malaria!! HAVIENDANI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom