Naombeni msaada kuhusiana na hali hii katika ndoto

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
4,513
3,554
Habari ya wakati huu wana JamiiForums.

Ni matumaini yangu mnaendelea vyema, kwa mlio na mkwamo Mungu awafanyie wepesi.
Bila kusahau tuendelee kuchukua tahadhari kuhusiana na ugonjwa huu wa korona ambao umeikumbu dunia. Bila shaka ni kwa muda ni imani yangu itakwisha.

Moja kwa moja kwenye mada.

Iko hivi kuna mara kadhaa nimekuwa nikiota ndoto niko mahali fulani, lakini kuna kuwa na ile hali ya kuhisi au kudhani hilo eneo nimewahi kufika au kuliona kabla. Sasa hii huwa inanitatiza, ningependa kupata maoni kwenu wanajamii nyinyi kwenu jambo kama hili likoje.

Kwa mwenye ufahamu uelewa au anaepitia kitu kama hiki aje atoe maoni yake niweze kupata ufahamu au ni mimi mwenyewe na matatizo yangu.

Akhsanteni, naomba kuwasilisha.

#JIKINGE NA KORONA.
#TUENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI KWA KADRI TULIVYOAMBIWA NA WATAALAMU WA AFYA NA VIONGOZI WA SERIKALI KWA UJUMLA.
 
Mkuu ulishalipa madeni yote?

Kama bado jiandae kupelekwa mahakamani maana ulishawahi kwenda mahakamani hivyo hiyo ndoto ni kukuandaa tu usipolipa madeni utapelekwa mahakamani.

Tafsiri imekomea hapo
 
Mi naotaga napata kazi jeshini,Till sijawahi enda jkt Wala Sina hobby na uaskari, Ni zaidi ya mara 6 hii ndoto.
Yangu imenishiida, Pambana na yako mkuu,
Kila la kheri.
 
Ila mimi kuna pahala nilisikia kwamba ndoto za hivyo zinamaanisha kuwa kama uko na kitu au mradi inatakiwa uingie darasani usomee hicho unachokifanya au simply ukasome.
But ni muda kidogo ko tafsiri ya hakika sikumbuki vyema kama kuna watu wanajua wanaweza saidia.
Mi huwa naota nafanya mtiani wa form six wakati nilishapita huko kitambo Sana nachukia Sana na naota mara nyingi mnooo sijui maana yake

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone

Eti nabakia Africa.
 
Mi naotaga napata kazi jeshini,Till sijawahi enda jkt Wala Sina hobby na uaskari, Ni zaidi ya mara 6 hii ndoto.
Yangu imenishiida, Pambana na yako mkuu,
Kila la kheri.
Ujiandae kupokea kipigo kitakatifu toka hao jamaa.. na kama ndoto inajirudia jua kipigo hakiepukiki cha kufanya hapo ni kuchagua kambi gani ya jeshi ikamilishe ndoto yako kwa kipigo kitakatifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom