Ntikwite
Member
- May 13, 2017
- 93
- 52
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23, ni mfanyakazi wa Serikali, mwaka 2017 niliamua kuwajengea wazazi wangu nyumba ya kuishi na niliijenga kwa shida sana maana ilifika wakati nikachukua mkopo benki na hela yote nikapeleka kwenye hiyo nyumba na kiukweli nilijibana sana na kwa maumivu makubwa, lakini baada ya kumaliza ujenzi baba yangu aliingiwa na tamaa ya kutaka kukopa pesa benki kwa dhamana ya hiyo nyumba
Nirudi nyuma kidogo yaani kabla ya hii nyumba baba alikuwaga na nyumba nzuri lakini iliuzwa na Saccos mwaka 2006 kwa sababu ya mkopo wa namna hii, naendelea, mabishano kati yangu mimi na baba yalikuwa makubwa na mimi sikuwa na nguvu kwa sababu nilikuwa mbali na nyumbani na baadaye alichukua mkopo huo.
Alianza kurejesha marejesho benki na ilipobaki miez mitatu akafeli. Kiukweli sikutaka nyumba iuzwe kwa sababu hela iliyokuwa imebaki ilikuwa ni chache na nilikuwa naimudu coz alikuwa anatoa 194k per month for 1yr na makubaliano yetu yakawa akikopa tena sitakuja kuhusika.
Jamani mimi mpaka sasa siamini baba yangu amechukuwa Tsh. Milioni 5 mwezi uliopita kwa makubaliano ya kurejesha 472k per month for 1yr na juzi kanipigia simu kuwa amemaliza ile hela na kujuta sana kuwa amekosea sana na hela ameimaliza yote na ananiomba msaada tena nimsaidie, mimi kiukweli kipato changu hakitoshi hata kulipa hiyo hela ya kila mwezi coz tayari ninabmkopo.
Jaman mimi nifanyaje jamani nyumba inaniuma sanaa nashindwa kuelezea vizuri hapa ila nina mengi juu ya hili.
Naombeni msaada wa mawazo.