Naombeni mnisaidie niwe Mzanzibari. Nina Degree, maisha yamekuwa magumu kwangu

Zabby99

Member
Oct 26, 2021
5
16
Habarini ndugu zangu, ni matumaini yangu mpo fresh.

Mimi ni mhitimu wa chuo ngazi ya degree katika fani ya uhasibu.

kiukweli nimejiajiri lakini hali si mchezo huku mtaani, ofisini nashinda masaa 14, kila siku lazima niende ofisini yani hata nlikopanga geto kuna wengine hawanijui vizuri, sijakaa sawa kuna kodi ya frem, tra, halmashauri, n.k yani hali si hali jamani.

Nimeomba sana ajira sehemu mbali mbali na hata kufikia interviews lakini bahati haikiwa upande wangu maana kiukweli ushindani ni mkubwa sana.

katika kujuliana hali na wanafunzi wenzangu wengi walionizidi darasa, tuliosoma nao, n.k nimeona wahitimu wengi waliotokea zanzibar tayari washapata ajira na maisha yanapendeza, wengi tayari wamemudu kuwa na magari, makazi mazuri, familia, n.k wakiwa na umri mdogo kabisa.

Kiukweli wengi walikuwa na uwezo wa kawaida sana ila upepo safi umewapitia wana ajira, wengi wapo huku huku bara wachache wanafanyia Zanzibar.

Nimeona na mimi mnipe ushauri nifanye kitu gani nitambulike kama mzanzibari maana wanasema ukiwa karibu na waridi basi na wewe utanukia.

Ningependa mnisaidie kunipa mbinu niwe raia wa Zanzibar tafadhali.
 
Tatizo sio Uzanzibari tatizo ni wewe mwenyewe ataukisaidiwa bado utafika Zanzibar na kuona wa Oman wa rika lako wanamaisha mazuri na wamefanikiwa utarudi apa kuomba msaada wa kupata uraia wa Oman kwa kuwa wana JF si wachoyo tutakupa tena mbinu lakini bado ukifika huko utaona Wahindi wa rika lako waliofanikiwa zaidi utarudi tena kuomba mbinu hapa JF na mchezo utakuwa ukizungua na kuzunguka
Hivyo jiboreshe mwenyewe pambana kipimo cha mafanikio si utaifa.
 
Population ya wazanzibari sio kubwa sana na Wapemba wanaosoma ni wachache sana kwahyo kwenye kipengele cha ajira wenyewe ni kama kushuka mlima kitonga iwe kwa hapa Bara au kwao visiwani
kiukweli wanajinoma, yani nawaonea wivu natamani na mimi ningekuwa wa huko, kazi za bara wana 21% na hata zikitoka huwa wanakuwa wachache kuikamilisha basi wanaajiriwaga kirahisi tu, pia na huko kwa wana ajira kwenye mashirika ya serikali ya Zanzibar.

Kwa ufupi ukiwa na elimu ya chuo + ukiwa mzenji ajira ni mteremko.

Kimbembe kipo huku sasa, degrees zipo kama yebo yebo, ushindani ni wa hali ya juu acha kabisa
 
Tatizo sio Uzanzibari tatizo ni wewe mwenyewe ataukisaidiwa bado utafika Zanzibar na kuona wa Oman wa rika lako wanamaisha mazuri na wamefanikiwa utarudi apa kuomba msaada wa kupata uraia wa Oman kwa kuwa wana JF si wachoyo tutakupa tena mbinu lakini bado ukifika huko utaona Wahindi wa rika lako waliofanikiwa zaidi utarudi tena kuomba mbinu hapa JF na mchezo utakuwa ukizungua na kuzunguka
Hivyo jiboreshe mwenyewe pambana kipimo cha mafanikio si utaifa.
Mkuu mimi nachotaka ni ajira tu niweze kujikimu pia niwe na mda walau wa kupumzika hata masaa machache.

yani hapa nilipo nipo ofisini tangia saa moja nafunga saa tatu na nusu usiku. hii ni kila siku.

siku nyingine biashara inabuma hata msosi unakuwa shida.

Nina mwenzangu nae ni machinga ana degree yake, jua linampiga acha tu.

kuna kipindi naona wazikabisa kujiajiri ni utumwa.
 
Nachojua Zanzibar wana mgao wao wa ajira asilimia 21 na bara tuna asilimia 79.

nafasi ziktangazwa mfano 100 basi wabara wanachukua nafasi 79, wazenji 21

sasa katika hizo nafasi 79, bara wanaweza kuomba watu elf 50, hapo uwezekano wa mtu kupata ajira ni asilimia 0.15%

katika nafasi 21 za wazenji, wanaweza kuomba watu 200 tu maana wengi wanakua washaajiriwa na pia wazenji idadi yao wanaoitimu vyuo ni ndogo, hapo uwezekano ni asilimia 10.

kumbuka pia wao wana serikali yao yenye taasisi, mashirika, n.k. huko wanaajiriwa wazanzibar tu. kuna mashirika kama zrb ni kama tra ya huku, zff ni kama tff yya huku , zssf ni kama nssf ya huku, ikulu zanzibar ni kama ikulu ya huku, n.k kaka anaweza kuajiriwa tra na mdogo wake zrb ya zenji, kaka anaweza kuajiriwa tff na mdogo wake zff ya zenji, kaka anaweza kuajiriwa tanesco na mdogo wake zeco ya zenji... yaani 2 in 1.

Kiufupi katika swala la ajira, kuwa mzanzibari ni baraka kubwa mno asikwambie mtu, wana kipaumbele cha hali ya juu mno.
 
Nachojua Zanzibar wana mgao wao wa ajira asilimia 21 na bara tuna asilimia 79.

nafasi ziktangazwa mfano 100 basi wabara wanachukua nafasi 79, wazenji 21

sasa katika hizo nafasi 79, bara wanaweza kuomba watu elf 50, hapo uwezekano wa mtu kupata ajira ni asilimia 0.15%

katika nafasi 21 za wazenji, wanaweza kuomba watu 200 tu maana wengi wanakua washaajiriwa na pia wazenji ni idadi yao wanaoitimu vyuo ni ndogo, hapo uwezekano ni asilimia 10, hata akikosa leo basi uwezekano ni mkubwa kupata siku nyingine.

kumbuka pia wao wana serikali yao yenye taasisi, mashirika, n.k. huko wanaajiriwa wazanzibar tu. kuna mashirika kama zrb ni kama tra ya huku, zff ni kama tff yya huku , zssf ni kama nssf ya huku, ikulu zanzibar ni kama ikulu ya huku, n.k wakifeli kupata kazi za serikali yao wanakuja huku kupewa mgo wao kwenye kazi za muungano huko tra, tanesco, polisi, jwtz, atcl, bot, nandarini, ikulu, n.k

Kiufupi katika swala la ajira, mzanzibar ni kama keki na hili halipingiki
Na Zanzibar huajiriwi SMZ kama huna kitambulisho cha Mkaazi
 
Na Zanzibar huajiriwi SMZ kama huna kitambulisho cha Mkaazi
Swala ukosefu wa ajira ni ajenda maalum kwa watz bara, na hivi degree zimekuwa kama njugu shida itaongezeka, watu wapo mitaani na degree zao tangu 2012 na bado wanaendelea kuomba, ukiwakusanya hao wote hadi sasa ni lundo kubwa sana.

Kwa mzenji labda ishu nyingine za mungano zitamtibua lakini huku kwenye ajira hana stress kama mbongo.
 
Population ya wazanzibari sio kubwa sana na Wapemba wanaosoma ni wachache sana kwahyo kwenye kipengele cha ajira wenyewe ni kama kushuka mlima kitonga iwe kwa hapa Bara au kwao visiwani
Kule elimu hakuna kabisa akienda na degree Fasta akiomba ajira huku bara wakiwe,a zile haki sawa anapata haraka

Sisi wawili waliacha chuo mwaka wa pili mmoja kapelekwa ofisa huko bandari kwao mwingine mwanajeshi na hawakumaliza chuo walipewa advanced diploma walipofika mwaka wa pili huko kwao ikawa dili wakapata ajira Fasta kama waliitwa vile kuna upungufu wa maofisa
 
Mkuu mimi nachotaka ni ajira tu niweze kujikimu pia niwe na mda walau wa kupumzika hata masaa machache.

yani hapa nilipo nipo ofisini tangia saa moja nafunga saa tatu na nusu usiku. hii ni kila siku.

siku nyingine biashara inabuma hata msosi unakuwa shida.

Nina mwenzangu nae ni machinga ana degree yake, jua linampiga acha tu.

kuna kipindi naona wazikabisa kujiajiri ni utumwa.
😤😤Ndo life mkuu utapata inshallah
 
Njoo Dubey napatikana Burj khalifa Nina hela Sana una Visa kwanza nikutumie planeticket!
 
Back
Top Bottom