Naombeni mnisaidie hili tatizo la masikio. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni mnisaidie hili tatizo la masikio.

Discussion in 'JF Doctor' started by Tx 500, Feb 2, 2012.

 1. T

  Tx 500 Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hodi jamvini!
  Nina sumbuliwa na masikio tangu 2003,
  sikio langu la kushoto linatoa milio isiyozimika toka mwaka 2003 na pia usikivu wake ni hafifu sana.
  La kulia nalo usikivu wake ni wastani na huwa kama lina geuka kwa ndani na kusabibisha kutokusikia mf.kama nikimeza chakula,au kupiga chafya.
  Nimeshazunguka hospitali zote kubwa hapa Dodoma na mikoani,nimetumia dawa za maji na vidonge but sijapata hata nafuu.
  Nimeshatumia dawa za wachina hospital ya mkoa wa dodoma hazijasaidia.
  Nilishaenda Muhimbili (ENT) wakasema kuna mishipa ya fahamu masikioni kama imesinyaa, wakanipa Hearing aid lakini badala ya kunisaidia ikawa inaua zaidi usikivu pindi nikikivua.
  Nimenda KCMC (ENT) wakanichunguza wamekuta masikio ni mazima,hayajatoboka,hakuna bakteria ila wakanipa dawa wakisema kuwa kuna kama compresion ndani ya masikio.wakanipa dawa za vidonge nimetumia ila tatizo bado kupona.
  Masikio hayatoi usaha wala uchafu wowote,pia hayaumi.
  Hali hii imeninyima amani ktk nafsi yangu kwa muda mrefu sasa.
  Naamini hapa jamvini wako wataalam wa afya wanaweza kunipa jibu la kuondokana na hii hali.
  Wajameni napata wakati mgumu sana hasa wakati nafanya Oral interview.
  Any kind of help plz.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa tatizo hilo.
  Kwa vile upo dodoma, tafuta ofisi ya labor (kazi), uwaulize ofisi ya wakala wa afya na usalama kazini. Utakayemkuta muambie tatizo lako. Nina wasiwasi tatizo lako linahusiana na kazi unayofanya, haswa kelele. Endapo utatokea kuwa dar, ni-pm nikuelekeze ofisi ambayo utapewa msaada wa kutambua tatizo na kuelekezwa marekebisho/rehabilitation.
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu...................... kuna vitu masikioni vinaitwa sensory hair.................. hivi viko katika sikio la kati................ na vingi sana .......................na hufanya kazi ya kusafirisha mawimbi ama mirindimo ya sauti toka kwenye ngoma kwenda sikio la ndani lenye nerves za kupeleka kwenye ubongo.............

  kwa mujibu wa maelezo yako inaonekana baadhi ya vitu hivyo (sensory hairs) vimekufa................. na vikishakufa haviwezi kufufuka kamwe na wala haviambukizi vingine zaidi................ bali hubaki kama makovu tu............... kwa hiyo ondoa hofu kuwa tatizo lako litaendelea kukua na kuwa kubwa zaidi....................

  kuna sababu mbalimbali ambazo husababisha hizo sensory hairs kudhoofika au kufa ................... kama .................. too much exposure to excessive noise mfano kelel za viwandani, viwanja vya ndege, stesheni za treni nk.................. na hata madarasani, misituni (mfano kelele za ndege)..................... ila kuna case nyingi nyingi vilevile za matatizo hayo kusababishwa na lishe na upungufu/ukodefu wa madini (kama chuma) ........... na vitamini (kama vitamin B)..................... nk......................

  kimsingi.............. hearing aids hupewa mgonjwa ambaye ana tatizo kwenye ngioma ya sikio au kama sensory hairs zimedhoofika lakini hazijafikia hatua ya kuwa "dead"............... sasa kwa case yako,.................... hearing aids hazitakusaidia kitu na nakushauri achana nazo................... kwani sensoiry hair zikifa huwa hakuna tena namna ya kuzihuisha.................. mshukuru Mungu kuwa huna tatizo la nta au usaha kujaa masikio .................... vinginevyo hizo hearing aids zingekuwa zinaacha mawimbi yakirindioma ndani ya ubongo hata zaidi ya siku mbili baada ya kuvua................... na hali yako ingekuwa mbaya zaidi............... na kama ukisafiri kwa ngege ile milio ya ndege inaweza kubaki masikioni hata kwa wiki nzima baada ya safari...................

  ushauri wangu, ................. jikubali tu katika hali uliyonayo sasa..................... achas kuhanmgaika na mahospitali................... yanakupotezea muda na hela zako bure................ furahia maisha na usiwazie sana mamabo hayo ya masikio................... jiamini zaidi na usiwaambie watu ovyo ovyo tatizo lako.................. na wengine hawaqtakuja kugundua kamwe kama utajiamini..................... epuka kuwaza jamabo lolote kwa muda mrefu.................. jiburudishe m,ara kwa mara kwa muziki wenye sauti yachini na hata kwa vinjwaji visivyo na kilevi kikali mara kwa mara (kama unatumia)......................

  pole sana mkuu .........................na nakutakia maisha mema yenye furaha........................
   
 4. T

  Tx 500 Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ushauri,
  ila kwa sasa sija ajiriwa, nimemaliza chuo hivi karibuni.
  Je naweza kwenda hiyo ofisi ya labor kwa sasa?
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kweli kabisa dada King'asti......................

  mkuu tx 500...................... ukifika dar m-PM sister hapo kwa msaada zaidi....................... ila unaweza kwenda moja kwa moja buguruni malapa pale kwenye shule ya viziwi................. utamkuta mtaalam mshauri wa viziwi na muombe ushauri anaweza kukusaidia.................. ila angalia anaweza kukuchomoa mchuzi wa bure kabisa.................... kuwa makini na niamini nilichokueleza kwenye post yangu iliyotangulia.................

  once again, .........................pole sana na jikaze kiume ......................usonge mbele na maisha.................... kuna watu wanaishi na hilo tatizo lako for decades na maisha yanakwenda kama kawaida ................. na hata huwezi kumshtukia asipokuibia siri kuwa hasikii vizuri................. unapaswa kujiamini tu..................
   
 6. T

  Tx 500 Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru sana ndugu kwa huu ushauri,nitaufanyia kazi.
  Hearing aids nimesha ziacha baada ya kuona zinaongeza ukubwa wa tatizo.
  Thanx.
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Tafuta pesa uende India, yaliyoshindikana hapa mengi wao huyaweza, kajaribu na huko. Usione watu wanakimbilia huko burebure kuna manufaa huko.
   
 8. T

  Tx 500 Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx mkuu!
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Siku hizi kuna tiba/tiba mbadala hata mabubu, ambao naturally huwa ni viziwi, wanasikia.

  Usikate tamaa, hakuna ugonjwa usio na tiba nenda India. Hao wanaokwambia hakuna tiba ndio madaktari uchwara, watu wamesha "break through" kwenye matatizo ya masikio.
   
 10. T

  Tx 500 Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duu! Nashkuru kwa ushauri,
  kwenda India inategemea na uwezo.
  Wengine ni watoto wa mkulima pure,tunategemea kuishi kwa jembe la mkono.
  Thanx da'Faiza fox,mungu akibariki nitaenda India.
   
 11. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  FF utaratibu gani mtu afuate ili aweza pelekwa India kwa ufadhili wa serikali?
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Zamani ilikuwa unaenda ustawi wa jamii, unaanzia hapo, kwa sasa sina uhakika lakini ukienda Wizara ya Afya utapata maelekezo. Halafu haya ni maswala ya wewe kumuona Mbunge wako akushughulikie ndio kazi zao hizo.
   
 13. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu Tx500. Naomba nikushauri yafuatayo; (1) Jikubali na hiyo hali ulionayo kama ulivyoshauriwa na mchangiaji mmoja.Kuwa mwenye furaha kwani kuna wenzako wanamatatizo zaidi yako,eg kiziwi na bubu, au mapacha walioungana,wewe huoni unanafuu? (2) Nenda kwenye maombi au hata shika tv wakati pale huduma ya uponyaji inapotolewa. Mimi nilishawahi kuwa na tatizo la kifua,nimeangaika hospitali zote za nje na ndani na sikupona, nikaamua kujikubali,kutokunywa dawa yeyote na kuhudhuria maombi ya live na ya kwenye tv mara nyingi. Sikuona aibu kuweka mkono pale ninapoumwa hadharani wakati mchungaji anapotuambia. Imani iyo imeniponya kabisa huu mwaka wa 8 sasa kifua kilichokua kinanifanya nishindwe kutembea au hata kuinua kilo 1,hakijaumwa kamwe, PRAISE THE LORD. (3) Usipende kutumia headphones au kukaa karibu na tv au radio kusikiliza kitu. Hii itafanya masikio yako yazoee sauti ndogo na kuongeza vichocheo vya usikivu. Mwangalie mtu usoni/mdomoni anapokua anatamka hasa unapokua kwenye interview. Hii pia hutumiwa na viziwi waliokua wanasikia zamani. (4) Muone mbunge wako kama alivyoshauri FF, kwa msaada wa kwenda India.
   
 14. T

  Tx 500 Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushuru kakajambazi kwa mawazo yako,
  kweli nimefarijika kwa michango yenu.
   
Loading...