MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Hivi karibuni miongoni mwa dada zetu imezuka tabia ya akinadada wengi kuvaa nguo ambazo zinaonesha sehemu kubwa ya matiti yao, ikibaki kuwa wazi. Takriban asilimia 60 hubaki kuwa wazi, na wengi wao huacha hadi sidiria zao zikaonekana.
Kimsingi, tabia hii - hata kama wanasema ni "fashion" - inaenda kinyume na maadili ya Kiafrika, au ya Kitanzania. Sisi - kwa utamaduni wetu - si watu wa kujianika hovyo miili yetu. Hata awali, enzi za mababu zetu, akinamama walivaa mavazi rasmi yaliyowasitiri, na hata mabinti pia. Ukitazama filamu ya ..... nimesahau jina lake... imechezwa majuzi, waigizaji wamevaa mavazi ya kale, ambayo yaliwasitiri ipasavyo.
Ningependa kupata maoni yenu, ni kwa sababu zipi akinadada hawa wameamua "kujiachia kihasara" namna hii?
Asanteni.