Naombeni mawazo yenu tafadhari

Wa-kishua

Member
Apr 10, 2021
29
24
Mimi niko na shida niko na rafiki yangu yaani anaweza kukwambia kitu halafu ni cha kweli ukimuuliza anakwambia ni ndoto zangu huwa naota ni za kweli. Kwa mfano nilikua naumwa sikumwambia akanitafuta akaniambia nimeota unaumwa, nikamdanganya sio kweli ila ni kweli nilikua naumwa.

Hatari kuna siku nilienda sehemu akanipigia simu akaniuliza uko sehemu fulani nikamwambia ndio sasa nikijaribu kumuuliza anasema yeye huwa anaotaga vitu vya kweli yaan kusema kweli ni nimetokea kumuogopa.

Hivi hii kitu inawezekana kweli we kila siku unaoteshwa wewe tu?

FB_IMG_1626373242385_1.jpg
 
Imenitokea sana hiyo, na mara zote ni rafiki mmoja tu wa karibu ndio huwa anapata muono huo hata sijajua siri iliyopo baina yake.

Kipindi hicho kabla hatujaanza mitihani ya kidato cha 6, rafiki yangu wa karibu aliniambia kaota ufaulu wangu nitakaoupata kwenye matokeo.

Alinambia “ushafaulu ndugu yangu!”

Kanitajia DIV na point yake vile vile kama nilivyokuja kupata kipindi cha matokeo.

Sikutaka kuamini kwa muda ule, maana zilipofika dakika za mwisho ilikuwa hutakiwi kuichanganya akili na kitu chengine chochote.

Ila ilikuwa kama alivyosema.
 
Back
Top Bottom