Naombeni mawazo yenu, nimenunua simu Kariakoo nimekuta ina matatizo na muuzaji anagoma nikiirudisha

Habarini waheshimiwa.
Nina shida,
Naomba msaada wenu.

Nilienda kununua simu Kariakoo juzi,
Baada ya kuichaji na kuanza kuitumia, nimeona ina matatizo mawili.
La kwanza, haikai na chaji hata masaa mawili,

La pili, nikiwasha data au nikimpigia mtu kwa mazungumzo ya kianzia dakika 3 tu,
Simu inakuwa na joto kali sana.

Shida yangu ni kwamba,
Nimempigia muuzaji (alinipa namba yake),
Ananijibu kuwa simu ikishatoka nje ya duka hawarudishi hela.

Nikamwomba anibadilishie,
Anadai kuwa simu za aina hiyo zimeisha dukani kwake na hawana utaratibu wa kumpa mteja aina nyingine,
Labda nisubiri
Mpaka atakapofuata mzigo mwingine (na hasemi ni lini).

Naomba msaada wenu,
Nichukue hatua gani stahiki ili kurudishiwa hela yangu au kubadilishiwa simu ingine?

Kwa kuwa majibu ya muuzaji hayana ushirikiano,
Nilifikiria kwenda polisi ila kwa bahati mbaya risiti shemeji yenu aliifulia kwenye mfuko wa shati kwa bahati mbaya.

Naombeni ushauri na mawazo yenu wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni aina gani.Tuanze hapo labda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee kama Huna risiti ni ngumu sana maana polisi watakuuliza risiti Ndo swali la Kwanzaa ila unaweza enda na polisi hapo akikiri alikuuzia tyu baaas imekula kwake uwe na pesa ya kuwatoa polisi lkn
Habarini waheshimiwa.
Nina shida,
Naomba msaada wenu.

Nilienda kununua simu Kariakoo juzi,
Baada ya kuichaji na kuanza kuitumia, nimeona ina matatizo mawili.
La kwanza, haikai na chaji hata masaa mawili,

La pili, nikiwasha data au nikimpigia mtu kwa mazungumzo ya kianzia dakika 3 tu,
Simu inakuwa na joto kali sana.

Shida yangu ni kwamba,
Nimempigia muuzaji (alinipa namba yake),
Ananijibu kuwa simu ikishatoka nje ya duka hawarudishi hela.

Nikamwomba anibadilishie,
Anadai kuwa simu za aina hiyo zimeisha dukani kwake na hawana utaratibu wa kumpa mteja aina nyingine,
Labda nisubiri
Mpaka atakapofuata mzigo mwingine (na hasemi ni lini).

Naomba msaada wenu,
Nichukue hatua gani stahiki ili kurudishiwa hela yangu au kubadilishiwa simu ingine?

Kwa kuwa majibu ya muuzaji hayana ushirikiano,
Nilifikiria kwenda polisi ila kwa bahati mbaya risiti shemeji yenu aliifulia kwenye mfuko wa shati kwa bahati mbaya.

Naombeni ushauri na mawazo yenu wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole

Bila Shaka itakuwa Samsung Galaxy S6 note plus

Simu haikuwa na warrant au Guarantee yoyote??

Umeharibu risiti, ishu itakuwia vigumu Mzee.

Hapo cha kufanya jichange ununue simu nyingine pia liwe fundisho kwako.

Pole Sana asee dah inauma kwakweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ulipoppteza risiti ndo na haki yako umepoteza!
maana hicho ndio kingekusaidia kupata haki yako
 
Wacheki jamaa wanaitw fair trade competition japo sina hakika sana na jina ila kwa ujumla hawa jamaaa wanadeal na haki za mlaji au mtumiaji wa bidhaa kutoka kwa muuzaji ...haki yako utaipata na lazima jamaa aliye kuuzia arudishe pesa na faini juu ..hawa jamaa wana mandate kufikisha hata mahakamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama una risiti ya tfda kambebe na polisi huyo fala
Habarini waheshimiwa.
Nina shida,
Naomba msaada wenu.

Nilienda kununua simu Kariakoo juzi,
Baada ya kuichaji na kuanza kuitumia, nimeona ina matatizo mawili.
La kwanza, haikai na chaji hata masaa mawili,

La pili, nikiwasha data au nikimpigia mtu kwa mazungumzo ya kianzia dakika 3 tu,
Simu inakuwa na joto kali sana.

Shida yangu ni kwamba,
Nimempigia muuzaji (alinipa namba yake),
Ananijibu kuwa simu ikishatoka nje ya duka hawarudishi hela.

Nikamwomba anibadilishie,
Anadai kuwa simu za aina hiyo zimeisha dukani kwake na hawana utaratibu wa kumpa mteja aina nyingine,
Labda nisubiri
Mpaka atakapofuata mzigo mwingine (na hasemi ni lini).

Naomba msaada wenu,
Nichukue hatua gani stahiki ili kurudishiwa hela yangu au kubadilishiwa simu ingine?

Kwa kuwa majibu ya muuzaji hayana ushirikiano,
Nilifikiria kwenda polisi ila kwa bahati mbaya risiti shemeji yenu aliifulia kwenye mfuko wa shati kwa bahati mbaya.

Naombeni ushauri na mawazo yenu wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ndio maana unajibiwa jeuri ashabaini kuwa risiti huna,risiti ni ushahidi kuthibitisha kuwa mlifanya biashara kati yenu,
NIPE ufafanuzi zaidi pale unaposema namba alikupatia na hadi leo unawasiliana wakati namba mara nyingi huandikwa katika risiti ambayo ushaipoteza
natanguliza pole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo hakupewa risiti! Sijui shemeji kaifulia, sio kweli. Na ndio maana MUUZAJI anajiamini, kwa sababu jamaa hana ushahidi wa kununua kwake.
Na aangalie, asije akatengeneza kesi ya kununua simu bila kudai risiti!
Mkuu usimlaumu hiyo tabia ya kutotunza risiti hata mimi ninayo niliwahi kupoteza haki yangu nilijifunza kutunza risiti.
 
Kariakoo ukienda kununua simu kuna bei mbili kuna bei halali unapewa na risiti na kuna bei ambayo hupewi risiti.hiyo ambayo hupewi risiti huwa ni ndogo mfano mi kuna mtu nlienda mnunulia ile TECNO CAMON X ilikuwa yauzwa 350k lakn bila risiti ni 270k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ndio maana unajibiwa jeuri ashabaini kuwa risiti huna,risiti ni ushahidi kuthibitisha kuwa mlifanya biashara kati yenu,
NIPE ufafanuzi zaidi pale unaposema namba alikupatia na hadi leo unawasiliana wakati namba mara nyingi huandikwa katika risiti ambayo ushaipoteza
natanguliza pole

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,

Namba niliichukua kutoka kwenye hiyo risiti ya EFD ambapo aliiandika nyuma Kwa peni, nikaisaisevu kwenye simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom