Naombeni kufafanuliwa juu ya ujio wa marais wa Chad na Zambia kwa wakati mmoja!

mliverpool

JF-Expert Member
Jan 6, 2015
1,506
2,830
Wataalamu wa diplomasia naomba mnisaidie juu ya ujio wa marais wawili nchini Tanzania, rais wa chad na wa Zambia na wote mwenyeji wao mi mmoja rais wa Tanzania,hizi ziara zimegongana kwa bahati mbaya au ni maksudi?? Inawezekana vipi rais kuhold ugeni wa marais wawili wenye ajenda tofauti kwa muda mmoja?maana sijawahi kushuhudia, mmoja anakaa siku mbili mmoja siku tatu!!
 
Lazima uvamie treni kwa mbele ambako kuna dereva, na injini yake, ukivamia nyuma utakuwa fara sawa na UKAWA uliovamia treni kwa nyuma wakaishia kusoma Namba.
 
Tatizo post ya kwanza imefanya uzi ote uvulugike,hahahahahahahahahaha,duh! Unajikuta unacheka kwasauti watafiti wanakuchulia ndio kati ya wale wa4.
 
Wataalamu wa diplomasia naomba mnisaidie juu ya ujio wa marais wawili nchini Tanzania, rais wa chad na wa Zambia na wote mwenyeji wao mi mmoja rais wa Tanzania,hizi ziara zimegongana kwa bahati mbaya au ni maksudi?? Inawezekana vipi rais kuhold ugeni wa marais wawili wenye ajenda tofauti kwa muda mmoja?maana sijawahi kushuhudia, mmoja anakaa siku mbili mmoja siku tatu!!

Raisi wa Chad kwasasa ni mwenyekiti wa AU hivyo ziara yake ni ya kujitambulisha kwa raisi mpya wa Tanzania na pia kuna mambo mengine ya kiufundi ambayo watajadili.

Pili, Raisi Edgar Chagwa Lungu anafanya ziara kumfahamu raisi Magufuli maana wanashabihiana sera zao khasa za kuhusu kodi, ukizingatia kwamba raisi Lungu pia ametimua kazi baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali akiwemo bosi wa idara ya mapato ZRA.

Hivyo sio vibaya kama wakiongozana kumuona raisi wa JMT mkulu mwenyewe, JPM.
 
Ni bahati kubwa kutembelewa na marais 2 kwa mpigo wenye madhumuni tofauti. Haijawahi kutokea hapa nchini kwetu. Huko kwenye mataifa makubwa ni kawaida kutembelewa na marais hata 10 kwa mpigo wenye madhumuni tofauti.

JPM alikuwa ahudhurie kwenye sherehe ya kumwapisha rais mpya wa Zambia. Hili lilishindikana kwa sababu ya janga la tetemeko la aridhi lililotupata. Ni raha ilioje kuona rais huyo kajileta mwenyewe tuongelee kuimarisha uhusiano wetu wa kiuchumi hususani reli yetu ya TAZARA na bomba letu la mafuta/ gesi la TAZAMA pamoja na ufanisi wa bandari yetu ya Dar.
 
JPM ubishi anauweza hata wakija 38 anaweza kujadiliana nao na mambo yakaenda akashushia Uhai tu
 
Ni bahati kubwa kutembelewa na marais 2 kwa mpigo wenye madhumuni tofauti. Haijawahi kutokea hapa nchini kwetu. Huko kwenye mataifa makubwa ni kawaida kutembelewa na marais hata 10 kwa mpigo wenye madhumuni tofauti.

JPM alikuwa ahudhurie kwenye sherehe ya kumwapisha rais mpya wa Zambia. Hili lilishindikana kwa sababu ya janga la tetemeko la aridhi lililotupata. Ni raha ilioje kuona rais huyo kajileta mwenyewe tuongelee kuimarisha uhusiano wetu wa kiuchumi hususani reli yetu ya TAZARA na bomba letu la mafuta/ gesi la TAZAMA pamoja na ufanisi wa bandari yetu ya Dar.
Tetemeko kwenyewe hakwenda mpaka leo
 
Back
Top Bottom