Naomba yanga ishushwe soka la tz lipande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba yanga ishushwe soka la tz lipande

Discussion in 'Sports' started by mzeelapa, Apr 4, 2012.

 1. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Soka la Tz limekuwa halipandi kwa sababu za kuingiza siasa za Uyanga na Usimba katika mechi za kitaifa na kimataifa. Ninachoomba kwa sakata hili la Yanga kuhusiana na adhabu walizopewa, Yanga iendelee na mgogoro mpaka ifikie hatua ya kushushwa daraja. Yanga ikishushwa daraja (Hata Simba lakini aahh.. hamna pa kuwakamata) hali itakuwa hivi:1. Kwa kuwa siku zote timu hizi mbili zinajengewa mazingira ya kuchukua nafasi ya kwanza au ya pili ( wakati mwingine kwa kudidimiza timu zinazochipukia) basi timu nyingine zitapata nafasi hiyo na kuleta ushindani katika ligi kuu.2. Katika mechi za kimataifa uzalendo wa ushangiliaji (Sio kweli kwamba ni utashi wa mtu binafsi kushangilia timu za nje) utajengeka maana hakutakuwa na Usimba wala Uyanga.3.Wachezaji wanaochipukia katika timu nyingine za ligi kuu watapata uzoefu zaidi maana sasa hivi wachezaji wengi wananyakuliwa na timu hizi matokeo yake kuishia benchi.4.Ligi Daraja la kwanza itachangamka zaidi na kupata washabiki maana Yanga itakuwa inafurukutia huko, na kupanda daraja toka daraja la kwanza kuingia ligi kuu sio lele mama.5. Migogoro na mivutano kati ya vilabu na/au TFF itapungua, kwa vipi......akili kwa kichwa....! (chanzo ni hivi vilabu)Mwisho nawaomba Wanakabumbu waondokane na kasumba ya kuwa bila Yanga au Simba ligi haitakuwa na msisimko. Najua kuna watakaosema mapato kutokana na viingilio yatashuka, hivyo viingilio vimesaidia nini mpaka sasa kama sio ulaji tu wa watu wachache??NAOMBA KUTOA HOJA
   
 2. assa von micky

  assa von micky Senior Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  acha unazi wewe changia vitu vya maana sio unakurupuka ,,,umetoka usingizini au alilala na mning'inio ? soka la tanzania linaporomoshwa na TFF wenyewe simba na yanga,serikali na wadau kama wewe wenye kupaka kinyesi jam
   
 3. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  huyu ndo wale form4 waliopitia form2 bila mtihani....tumsamehe:hat::tape2:
   
 4. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Acheni jazba..Huo ndio ukweli, nimesikia mwanachama mmoja anadai rufaa ya Yanga ikishindwa watakwenda mahakamani kusimamishi Ligi Kuu, hivyo ndio kuendeleza soka? Nasema huu mgogoro Yanga msipokuwa makini mtaangukia pua!! Mwingine anasema wanachama wataandamana, sasa hii ni siasa au michezo?
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Kalale wewe mtoto.
   
Loading...