Naomba Wizara ya Nishati na TANESCO mtuweke sawa, kuunganishiwa umeme ni Sh. 27,000 au 57,000?

Thread Ya Moto Sana Hii
Nadhani Tanesco Toeni Ufafanuzi Kuhusu 27 Ama 57
Bei kwa maeneo ya vijijini ni Tsh 27000 tu kwa wateja waliopo ndani ya mita 30 kutoka kwenye miundombinu ya umeme.Mteja anapaswa kutoa taarifa kamili kwa tuhuma anazotoa ili kusikilizwa nankuchukua hatua kamili
 
Ndugu mpendwa mteja wetu

Tumepokea lalamiko lako aitha tupo tayarinkukusikiliza na kuchukua hatua stahiki kuhakikisha ubapatiwa huduma kwa bei halisi.Kwa taarifa ni kwamba mteja analipa kiasi halisi cha kufungiwa umeme kupitia bank na sio kwa mtu au mfanyakazi na anapatiwa ujumbe wa maneno kutoka bank kuwa kiasi hicho kinepokelewa, Mteja anapasea pia kumlipa mkandarasi wake aliyefanya wiring kiasi ambacho wamekubaliana wenyewe

Je ulimlipa nani?

Wilaya gani?

Namba yako ya simu?

Je ulipatiwa stakabadhi(risiti)

Je ulipewa gharama za makadirio ya kulipia na ofisi? Tunaomba taarifa hizo tufanyie kazi swala lako tafadhali
mhusika atafika... Thanks for a positive response
 
Ahsante kwa maelezo mazuri, umeme wa Rea ulipita kijijni kwetu miaka 3 iliyopita lkn ulipita barabara kuu tuu, kama mim niko pembeni kidogo kama mita 800 kutoka barabara kuu nafanyaje kuupata huo umeme wa REA, Najua nikienda tanesco wataanza kunihesabia gharama ya nguzo.
 
Hiyo 30 ni ya kuthibitisha/kujaza fomu pamoja na mchoro wa nyumba husika unayohitaji huo umeme
Ndivyo the so called contractor alivyo niambia.Lakini sasa kwa nini tuambiwe kuingiza umeme ni Sh.27,000 badala ya 57,000.That is the question.Kwa nini tusiwaambie wananchi ukweli tuna piga piga corner?
 
hili jamaa ni sawa na mke anamshitaki mume polisi ,anaulizwa lete ushahidi wa kupigwa anagoma anasema anaogopa akisema mume atafungwa ,imagine that
Acha upuuzi wewe,unapeleka taarifa zako halafu baadae wanapeleka taarifa unakuwa uhasama mtupu.Yameshatokea kwa wengine,so I don't want to make the same mistakes,wanalindana hawa.
 
Bei kwa maeneo ya vijijini ni Tsh 27000 tu kwa wateja waliopo ndani ya mita 30 kutoka kwenye miundombinu ya umeme.Mteja anapaswa kutoa taarifa kamili kwa tuhuma anazotoa ili kusikilizwa nankuchukua hatua kamili
Sawa
 
Ndivyo the so called contractor alivyo niambia.Lakini sasa kwa nini tuambiwe kuingiza umeme ni Sh.27,000 badala ya 57,000.That is the question.Kwa nini tusiwaambie wananchi ukweli tuna piga piga corner?
Ndio mara ya kwanza unafunga umeme inaonekana, la sivyo utakuja pia na hesabu la vifaa ulivyotumia kufanyia wiring kuwa linapingana na maagizo ya wizara.
 
Ndio mara ya kwanza unafunga umeme inaonekana, la sivyo utakuja pia na hesabu la vifaa ulivyotumia kufanyia wiring kuwa linapingana na maagizo ya wizara.
Mimi ni mzoefu sana wa kuweka umeme,nina nyumba zingine nne ambazo nimeweka umeme kwa hiyo najua gharama.Sijui kama umeelewa swali langu la msingi.Ni kwamba serikali imeagiza Sh.27,000,hii 30,000 ingine inatoka wapi,si TANESCO inakiuka maagizo ya serikali?Naomba tuelewane,unless serikali nayo imedanganya wananchi,jambo ambalo nalikataa.
 
Umeeleza vyema na nimekuelewa, tukirudi nacho hizo nyumba nyingine ulijaza fomu?
 
Nadhani jamaa alikuwa kafunga wiring ila ramani ya wiring hakuwa nayo maana Tanesco hawaingizi umeme mpaka uwe na ramani ya wiring ambayo inachorwa na mkandarasi (Contaractor) maana tanesco hawahusiki na kukucholea ramani bali wanaithibitisha tu kama iko sawa kwahiyo atakayekucholea ramani utaelewana naye bei.
 
Nashukuru kwa response yenu.Hata hivyo itakuwa vigumu kuwapa details mlizotaka kwa kuwa hatimaye hii inaleta uhasama kati ya mteja na kampuni.Ukweli ni kwamba hatimaye ofisi husika inajua nani alipeleka tuhuma.Bygone is bygone.

Nilichotaka ni ufafanuzi wa yale niliyo weka kwenye malalamiko yangu,ili nijue ukweli na ninyi muweze kurekebisha mambo kwa kuwekea maagizo msisitizo.Please do that,inatosha.
Kuna jambo linawachanganya wengi sana kati ya tanesco na mkandarasi.
Ni hivi
Mara uchukuapo form (bure) tanesco,hiyo form kuna details ambazo mkandarasi anapaswa kujaza,na sio kujaza tu bali pia anapaswa afike nyumbani kwako,kama tayari ulifanya wayaringi zako basi apime vitu vyote vinavyotakiwa.

Mara baada ya yeye mkandarasi kupima,kuchora na kujiridhisha kwamba mfumo wako ni mzuri na waweza fungiwa umeme ndipo anasaini Na mteja anasini hiyo form tayari kwa kuirudisha tanesco.

Ifahamike kwamba contractor wote ni nje na tanesco,hivyo unapaswa kubagain naye kwa gharama ambazo zitahitajika,na anapaswa akupatie efd risiti maana wapo kisheria na wamesajiriwa kwa mujibu wa sheria.
Pia wanalipa kodi kwa kazi hiyo.

Endapo form imerudishwa tanesco,ni jukumu la tanesco kusavei eneo lako kwa ajiri ya kukuandalia gharama unayopaswa kulipia.
Ikumbukwe kuwa gharama zote zinatufautiana kulingana na urefu wa kutoka nguzo ilipo na mteja.

Kuhusu REA na TANESCO

Rea ni mfadhiri wa miradi ya umeme VIJIJINI namaanisha ndiye mtoa pesa za miradi hiyo inapojengwa ambapo Kuna Wakandarasi wamepewa tenda za ujenzi kimkataba wakati huo TANESCO ni wasimamizi wa hiyo miradi.

Inapotokea muda wa mkandarasi umeisha na amefanya kazi yake ikiwemo na kuwaunganishia wateja kama mkataba wao unavyotaka (huwa wanapewa idadi ya watu kwa kila Kijiji/scope) wanatakiwa kuukabidhi rasmi kwa tanesco.

Wakikabidhi tu,unakuwa chini ya uendeshaji na uangalizi wa tanesco,hivyo ofa ya Rea inakuwa imepita na kinachofuata ni kufuata taratibu na kanuni za tanesco.

Mwisho,
Serikali kwa maeneo ya vijijini hata kama tayari mradi ulikabidhiwa TANESCO, Bei imeshuka na kubakia 27000/= na wengi wananufaika.
Asante.
 
Back
Top Bottom