Naomba Wizara ya Elimu itoe muongozo juu ya muda wa kukaa darasani kwa watoto wetu

nanilii

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
275
500
Nitakwenda moja kwa moja kwenye mada bila kupoteza muda.

Naomba Wizara ya Elimu itoe muongozo juu ya muda wa kukaa darasani kwa watoto wetu. Ni kweli shule zina Bodi, lakini tukumbuke hakuna taasisi ambayo hairatibiwi, Usafiri ipo SUMATRA, nishati ipo EWURA, hotel sijui TFDA nk, sasa hivi mfano kuna shule za sekondari wao wamejipangia watoto waende shule mpaka Jumamosi, na mwanafunzi anaingia (yaani anahesabu namba) saa moja kamili asubuhi (yaani nyumbani atoke saa 12.00 kamili) afu kutoka darasani saa 11.30 jioni.

Naomba niulize swali hata wewe afisa uliopo hapo wizarani ukienda''Masters Degree program'' ukaambiwa unaingia saa1.00 asubuhi unatoka saa 11.30 jioni na break ndogo tu ya dk 30 pale saa 4.00 asubuhi utaweza ? afu hili suala la kila mkuu wa shule anaamua na Bodi yake " wanafunzi muje mpaka Jumamosi" kwanini, inafika wakati sasa watoto badala ya kwenda Ibada za Jumapili , Jumapili ndo imekuwa siku ya kufua na usafi mwingine na sio kwenda ibadani , jamani tunaelekea wapi (we 're too mechanical when it comes to education, we don't use our brains) sijui kwanini.

Kitu kingine kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi , ni kwamba mwanafunzi anapopata muda wa kufanya reflection'' ya yale aliyosoma, ndo anaelewa vizuri kuliko ku-overdose'' ambako ndo mwendo wa sasa karibu shule nyingi.

Nakumbuka zamani tulikuwa na mifumo miwili, either, shule wanafunzi wanatoka saa 8.00 mchana chakula cha mchana wanakula kwao, au wanatoka saa 10.00 lakini kunakuwa na mapumziko kuanzia saa 6.30 hadi saa 7.45 ya kwenda kula, LAKINI sio non-stop kuanzia saa 1.00 asubuhi mpaka saa 11.30 jioni, jamani hii ni tatizo.

Naombeni muwe na MUONGOZO (tutumie maarifa zaidi kuliko kuwa too mechanical)

Asante
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom