Naomba Waziri wa Elimu pita hapa, shule za kutwa kuwe na utaratibu wa chakula

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,899
45,303
Mh waziri

Elimu inabidi kufanyiwa maboresho katika maeneo muhimu kama haya

Wazazi wanabidi kushirikiana na walimu katika kuandaa ustawi bora wa watoto wao ikiwemo swala la shule ambazo ni day schools Kupata chakula cha mchana na Uji.

Kwakuwa idadi ya Wanafunzi ni kubwa kila Mzazi/mlezi anabidi kuchangia hela ya chakula ili mwane Apate chakula Cha mchana shuleni gharama inaweza kuwa elfu kumi kwa mwezi 10k kwa kila Mwanafunzi.

Hii itainua Ari ya usomaji kwa wanafunzi na kuweka umakini mkubwa katika kuyafikia Malengo then kupitia Jambo hili watoto wengi wataondokana na swala la Mimba mashuleni kwani njaa mara nyingi husababisha Huwezo Mdogo wa kufikiria na kufanya maamuzi hasa kwa watoto wa kike.

Watoto wanabidi wapatiwe chakula mashuleni naomba kuwasilisha.
 
Wateka sera.

Baada ya muda watasema Uji mchachu, wazazi wapewe tenda.. Tuwe makini na maharamia wa Nchi hii.
 
Tatizo ni kwamba kuna wazazi hata hiyo 10k hawana cjui sasa itakuwaje!hali ya maisha kwa sasa ni mbaya sana hasa vijijini.watu wanaishi kwa mlo mmoja tu na hawawezi hata kununua kipande cha samaki.
 
tatizo ni kwamba kuna wazazi hata hiyo 10k hawana cjui sasa itakuwaje!hali ya maisha kwa sasa ni mbaya sana hasa vijijini.watu wanaishi kwa mlo mmoja tu na hawawezi hata kununua kipande cha samaki.
Tukaribu tunaweza na serikali inaweza kuweka ruzuku hapo
 
Mtoa mada unaishi nchivgani?
Mchakato wa chakula mashuleni ulishaanza na umefanikiwa ka 75%
Kazi iendelee..
 
Back
Top Bottom