Naomba Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais waweke akaunti zao na majina halisi hapa JamiiForums ili wapewe taarifa mbalimbali

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
673
859
Ninampongeza sana Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani hivi karibuni kupitia ukurasa waofisi yake na ule wa msemaji mkuu wa serikali imeweka akaunti yake ya Instagram inayojulikana kama kassim_m_majaliwa.

Hiyo ni hatua nzuri kwani wananchi walio wengi watamfikishia taarifa mbalimbali kwa usiri, ukaribu na haraka zaidi lakini ninaomba viongozi wakuu serikalini wawe na akaunti zinazotambulika hapa JF ndio itakua rahisi zaidi kuwaambia mambo kinagaubaga.

Hivyo basi waziri mkuu, makamu wa Rais na Mh. Rais waweke akaunti zao na majina halisi hapa ili wapewe taarifa mbalimbali.

Viongozi wanaojiamini waadilifu na watenda haki hawaoni tabu kuweka mawasiliano yao hadharani ili jamii ishiriki nao kwapamoja kusukuma gurudumu la maisha.

Raia wakiwa wanatendewa haki na wakiwa wastaarabu watatumia njia hizo kistaarabu bila tatizo
 
Ningeshauri waweke account zao ili kupewa taarifa na wananchi. Lakini waondoe comment section ili kulinda heshima ya viongozi. Ni wazo zuri. Ila comment section inaweza haribu
 
Hiyo ni hatua nzuri kwani wananchi walio wengi watamfikishia taarifa mbalimbali kwa usiri, ukaribu na haraka zaidi lakini ninaomba viongozi wakuu serikalini wawe na akaunti zinazotambulika hapa JF ndio itakua rahisi zaidi kuwaambia mambo kinagaubaga.

Hivyo basi waziri mkuu, makamu wa Rais na Mh. Rais waweke akaunti zao na majina halisi hapa ili wapewe taarifa mbalimbali.
Haohao wahalifu watatengeneza akaunti za majina ya hao viongozi mwisho wa siku utajikuta unawasilisha tuhuma kwa unayemtuhumu
 
Hapa zinakuepo rasmi kama zile za idara za serikali kama tanesco,idara za maji nk. Zinajulikana kiofisi modes. Mbona hata leo unaweza ukajiita majaliwa,katibu,balozi nk lakini inaweza nijina halisi.
Pia hatupeleki barua ofisini,tunatuma mtandaoni hamna siri hata anayetuhumiwa akiona sawatu
 
Back
Top Bottom