Naomba watu wenye ujuzi wa katiba nzuri watujuze nini kiwepo katia katiba mpya

manenge

JF-Expert Member
Apr 30, 2008
279
17
Bila kujali itikadi za vyama ningeomba watu wenye uchungu na uzalendo na nchi hii watutengenezee muhtasari ambao utatumika kama dira kwa watu kutoa maoni yatakayotupa katiba nzuri. Najua watu wasioitakia mema nchi au kwa sababu tu za kupenda vyama vyao wanaweza kushawishi kundi kubwa la watu kutoa maoni ambayo hayatalisaidia taifa kuwa na katiba nzuri. Tujue kwamba hii ni fursa pekee na adimu ambayo itatuwezesha kuwa na katiba itakayotuwezesha kusonga mbele. Vyama vya siasa huzaliwa na kufa lakini nchi kama taifa litaendelea kuwapo. Naomba muhtasari huo uzingatie mambo muhimu tu na uwe rahisi kueleweka kwa watu wa kawaida na uweze kusambazwa kwa watu wengi. Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom