Jamani naomba ushauri. Mimi ni kijana mdogo tu. Nilikuja Marekani kwa taabu sana mwaka 2000 na kwa kudra za mwenyezi mungu niliweza kumaliza shule baada ya miaka nane. Sio kua masomo yalinishinda ila mambo ya fedha. Semester hii nimeingia, inayofuata inabidi nikusanye ada. Nashukuru nimeweza kupata shahada yangu. Kwa jinsi nilivyomaliza, nilifanikiwa kupata offer za kazi kadha lakini mambo ya makaratasi ni magumu sana. Nilijaribu kuongea na kumlipa mama mmoja wa kinugu lakini kila wiki anataka hela sasa nimeshindwa.
Nyumbani kwetu Dar es Salaam ndugu zangu wananishauri nirudi kwasababu kwa vile nina degree ya biashara kazi sitokosa. Naomba ushauri ndugu zangu. Kwani nimejaribu sana mbinu zote ninazozijua America lakini naona system inanibana. Laiti kama ningekua nina green card, ningekua ninapeta vibaya mno. Je, wanaforum, mnanishauri vipi?