Naomba Ushauri

Bilionea

Member
May 16, 2008
17
0
Jamani naomba ushauri. Mimi ni kijana mdogo tu. Nilikuja Marekani kwa taabu sana mwaka 2000 na kwa kudra za mwenyezi mungu niliweza kumaliza shule baada ya miaka nane. Sio kua masomo yalinishinda ila mambo ya fedha. Semester hii nimeingia, inayofuata inabidi nikusanye ada. Nashukuru nimeweza kupata shahada yangu. Kwa jinsi nilivyomaliza, nilifanikiwa kupata offer za kazi kadha lakini mambo ya makaratasi ni magumu sana. Nilijaribu kuongea na kumlipa mama mmoja wa kinugu lakini kila wiki anataka hela sasa nimeshindwa.
Nyumbani kwetu Dar es Salaam ndugu zangu wananishauri nirudi kwasababu kwa vile nina degree ya biashara kazi sitokosa. Naomba ushauri ndugu zangu. Kwani nimejaribu sana mbinu zote ninazozijua America lakini naona system inanibana. Laiti kama ningekua nina green card, ningekua ninapeta vibaya mno. Je, wanaforum, mnanishauri vipi?
 
Ningekua na hao magodfather ndugu yangu hata ushauri nisinge omba. Ningekusanya nauli tu ya kurudi nyumbani. My situation is really fucked. This is one hell of a predicament. The sacrifices that I had to go through all in the hope that I just might see the light at the end of the tunnel seems like a freaking pipe dream. Jamani, kama magodfather mpo humu, please hear a brother out.
 
Haku na kwenyewe Tabu tupu, wala usiamini zile ahadi za Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, hazijatimia wala hata kunukia.

Cha msingi parangana usome zaidi, ukija huku angalau na Masters au Phd, angalau unweza kuwa na uhakika na mkate wako wa kila siku. Parangana ndugu, ili usijaribu tendo lolote la uhalifu, jinyime omba mungu na utashinda
 
Angalia moyo wako wakuambiaje, kwa mfano mie nilikuwa aussie nilisoma huko na kufanya kazi kwa muda kidogo nikapata pesa yangu kiasi, ki ukweli sikupenda maisha ya nje kabisa....... nilichoka sana.... nikajiwazia je nikirudi nyumbani na kufanya shughuli zangu binafsi itakuwaje?, nikarudi, kusema kweli ndugu wengi walinicheka but sikujali , ckuenda kuomba kazi kokote nikaanzisha biashara na mpaka sasa naona Biashara zangu zinakua zaidi na zaidi.................. nafikiri ni nia yako tu wewe na effort zako zitakufanikisha kuishi vizuri hapa Tanzania.
 
Nashukuru sana mawazo yako. Tatizo kwetu mimi pekee ndio wananitegemea kwa kila kitu na nilikua naambiwa toka mdogo kua elimu ndio ufunguo wa maisha. Don't get me wrong, I still believe that. I just expected that after all those sleepless nights after 12 hour shifts and graduating Summa cum Laude, I'd be in a better position to help my family out.
They say good things come to those who wait but I'm freaking overdue. I just anticipated greener pastures but what lies behind us and before us are tiny matters compared to what lies within us.
 
Angalia moyo wako wakuambiaje, kwa mfano mie nilikuwa aussie nilisoma huko na kufanya kazi kwa muda kidogo nikapata pesa yangu kiasi, ki ukweli sikupenda maisha ya nje kabisa....... nilichoka sana.... nikajiwazia je nikirudi nyumbani na kufanya shughuli zangu binafsi itakuwaje?, nikarudi, kusema kweli ndugu wengi walinicheka but sikujali , ckuenda kuomba kazi kokote nikaanzisha biashara na mpaka sasa naona Biashara zangu zinakua zaidi na zaidi.................. nafikiri ni nia yako tu wewe na effort zako zitakufanikisha kuishi vizuri hapa Tanzania.

Asante ndugu, maana naona hiyo ndio plan nyingine. Kama nitakosa ajira atleast nina business plan kadhaa kwa nchi yetu ninazojua zitaitika lakini mambo ya mkopo ndio mpaka nyumba naambiwa.
 
Jamani naomba ushauri. Mimi ni kijana mdogo tu. Nilikuja Marekani kwa taabu sana mwaka 2000 na kwa kudra za mwenyezi mungu niliweza kumaliza shule baada ya miaka nane. Sio kua masomo yalinishinda ila mambo ya fedha. Semester hii nimeingia, inayofuata inabidi nikusanye ada. Nashukuru nimeweza kupata shahada yangu. Kwa jinsi nilivyomaliza, nilifanikiwa kupata offer za kazi kadha lakini mambo ya makaratasi ni magumu sana. Nilijaribu kuongea na kumlipa mama mmoja wa kinugu lakini kila wiki anataka hela sasa nimeshindwa.
Nyumbani kwetu Dar es Salaam ndugu zangu wananishauri nirudi kwasababu kwa vile nina degree ya biashara kazi sitokosa. Naomba ushauri ndugu zangu. Kwani nimejaribu sana mbinu zote ninazozijua America lakini naona system inanibana. Laiti kama ningekua nina green card, ningekua ninapeta vibaya mno. Je, wanaforum, mnanishauri vipi?

Bilionea - kwani status yako ya sasa hivi ikoje?
 
Vumilia fanya fanya kazi kwa muda ili udundulize pesa kwa ajili ya biashara unayotaka then njoo uanzishe hata kwa hicho kidogo ulichopata mwishowe kitaongezeka
 
My status is pending. Wameniita interview in three weeks lakini ndio mwanamke anavisa kichizi mazee. Yaani nikianza kusimulia itakua issue. Hata kwenda kwa wajomba hataki tena bila mkwanja zaidi. A position that I'm not able to accomodate.
 
Nashukuru ndugu, nadhani itabidi nifikirie kijasirimali zaidi ya kiajiriwa.
 
Jamani naomba ushauri. Mimi ni kijana mdogo tu. Nilikuja Marekani kwa taabu sana mwaka 2000 na kwa kudra za mwenyezi mungu niliweza kumaliza shule baada ya miaka nane. Sio kua masomo yalinishinda ila mambo ya fedha. Semester hii nimeingia, inayofuata inabidi nikusanye ada. Nashukuru nimeweza kupata shahada yangu. Kwa jinsi nilivyomaliza, nilifanikiwa kupata offer za kazi kadha lakini mambo ya makaratasi ni magumu sana. Nilijaribu kuongea na kumlipa mama mmoja wa kinugu lakini kila wiki anataka hela sasa nimeshindwa.
Nyumbani kwetu Dar es Salaam ndugu zangu wananishauri nirudi kwasababu kwa vile nina degree ya biashara kazi sitokosa. Naomba ushauri ndugu zangu. Kwani nimejaribu sana mbinu zote ninazozijua America lakini naona system inanibana. Laiti kama ningekua nina green card, ningekua ninapeta vibaya mno. Je, wanaforum, mnanishauri vipi?

Bilionea, nadhani majibu ya maswali yako unayo mwenyewe hata katika maelezo yako.
1. sioni sababu ya wewe kuingia matatizo ya kumlipa mtu ili uishi sehemu isivyo halali hadi upate makaratasi ilhali tayari una elimu inayokuwezesha kupata kazi nzuri. Kama una kazi tayari ina maana upo katika kipindi cha OPT/CPT na kwa sasa wameongeza muda kufikia miezi 24. Sasa kwa nini umlipe mtu fedha wakati una muda wa kutosha kutazamia whether unaweza kubaki hapa kwa kuiomba hiyo kampuni ikuombee the right documents?

2. Kwa nini uishi kama fugitive wakati una kwenu? Je umeambiwa kuwa kwenu kazi hamna? Je umejaribu kutafuta kazi kwenu ukakosa? Hiyo degree si umesoma wewe ina maana huamini uwezo wako ku-compete for a job back home? Kijana, time is precious and there is no way you prove the impossible bila kujaribu. Usikae hapa ukatumikishwa kwa ajili ya documents, if you really want a job, you can get it anywhere as long as you are
a. determined to get a job
b. ready to compete for a position
c. believe that you are able to get a job
d. you really need a job.

Ni heri uishi mahali kwa njia halali kuliko kuishi kama mfungwa. At least you are educated. Mambo ya kuwa na god father yamepitwa na wakati na ni mbinu inayotumiwa na wasiokuwa na qualifications ya kupata ajira. Qualifications zako ndio godfather wako period!

Siku hizi institutions back home zina webpages ambazo zinatangaza ajira kwa watanzania waliopo nje ya nchi. Jaribu NBC www.nbctz.com tafuta link ya ajira utapata taarifa zaidi.
 
My status is pending. Wameniita interview in three weeks lakini ndio mwanamke anavisa kichizi mazee. Yaani nikianza kusimulia itakua issue. Hata kwenda kwa wajomba hataki tena bila mkwanja zaidi. A position that I'm not able to accomodate.

Kwanza kumbe status yako iko kwenye mkondo mzuri. Kwa hiyo una kila nafasi ya kuiweka sawa.

Now, umeitwa kwenye interview ndani ya wiki 3, lakini bibie analeta ukorofi.....ana dai mkwanja. Bilionea, hivi unajua ni watu wangapi ambao wameharibu status wana wish wangekuwa kwenye situation yako? My point is, katika muda huu wa wiki hizo tatu, inabidi ufanye lolote lile kuweza kumweka huyo bibie kwenye good mood. I mean, kama kweli unataka hayo makaratasi, basi una budi kuhandle your business kisawasawa. Kwa hiyo mzee, kama huna hela ya kumhonga huyo kimwana, basi ingia mtaani kaisake -piga ma-overtime, kakope kwa washikaji, tembelea payday loan stores.... Mzee, fate ya kukamilisha makaratasi yako iko mikononi mwako. Usiruhusu room for errors...
 
Hiyo degree si umesoma wewe ina maana huamini uwezo wako ku-compete for a job back home? ...Usikae hapa ukatumikishwa kwa ajili ya documents... Siku hizi institutions back home zina...

In the interest of fair disclosure, ili tujue kwamba ushairi huu ni wa mtu anaejua situation za kikazi za sehemu zote mbili, na mtu ambae hata yeye angefuata ushauri huu huu kama angekuwa katika situation hii, je, Bimkubwa wewe uko nyumbani ?

Na kama hauko, kwa jinsi inavyoonekana onekana hapo juu, je, ni busara ndugu Bilionea na yeye ahangaike kufa na kupona kupata kazi "hapa" ili avune matunda yaliyokubakiza wewe "hapa" ?
 
Bilionea, nadhani majibu ya maswali yako unayo mwenyewe hata katika maelezo yako.
1. sioni sababu ya wewe kuingia matatizo ya kumlipa mtu ili uishi sehemu isivyo halali hadi upate makaratasi ilhali tayari una elimu inayokuwezesha kupata kazi nzuri. Kama una kazi tayari ina maana upo katika kipindi cha OPT/CPT na kwa sasa wameongeza muda kufikia miezi 24. Sasa kwa nini umlipe mtu fedha wakati una muda wa kutosha kutazamia whether unaweza kubaki hapa kwa kuiomba hiyo kampuni ikuombee the right documents?

2. Kwa nini uishi kama fugitive wakati una kwenu? Je umeambiwa kuwa kwenu kazi hamna? Je umejaribu kutafuta kazi kwenu ukakosa? Hiyo degree si umesoma wewe ina maana huamini uwezo wako ku-compete for a job back home? Kijana, time is precious and there is no way you prove the impossible bila kujaribu. Usikae hapa ukatumikishwa kwa ajili ya documents, if you really want a job, you can get it anywhere as long as you are
a. determined to get a job
b. ready to compete for a position
c. believe that you are able to get a job
d. you really need a job.

Ni heri uishi mahali kwa njia halali kuliko kuishi kama mfungwa. At least you are educated. Mambo ya kuwa na god father yamepitwa na wakati na ni mbinu inayotumiwa na wasiokuwa na qualifications ya kupata ajira. Qualifications zako ndio godfather wako period!

Siku hizi institutions back home zina webpages ambazo zinatangaza ajira kwa watanzania waliopo nje ya nchi. Jaribu NBC www.nbctz.com tafuta link ya ajira utapata taarifa zaidi.

Bimkubwa, you have no idea the kind of boost you gave my morale. You are the first person to explicitly tell me that you can secure a position based on your qualifications back home. Anybody and everybody I talk to with the exception of my immediate family contends that it’s virtually impossible to get a job without knowing “somebody”. I know u believe what u said, I also believe that it should be that way. I just hope that it is.
Kuhani, great point………..
 
Kusema kweli kupata kazi hapa ni kwa kujuana unakuta nafasi za kazi zinatangazwa wakati tayari kuna watu washapewa............. hivyo ni bahati ya mtu na ukitegemea kuna watu wengi sasa wana degree kwa hapa na hawana kazi......... inabidi wanafunzi wa kwetu sasa wafundishwe ujasiliamali pia.. ili kama kwenye kuajiriwa kukibuma basi ajiajiri mwenyewe
 
Maana ya neno BONGO hapa kwetu ni kutumia akili kwa kila kitu. TZ kuna watu hawana kazi lakini wanasomesha watoto shule za ghalama kubwa, pia wana nyumba kubwa na nzuri huwezi hata kuamini kuwa nyumba hiyo inamilikiwa na mtu utakaemuona maana hana kazi na nyumba hiyo siyo ya urithi. Kwa hoja hii nakushauri urudi utaishi sawa na hao waliopo wanavyoishi.

Kuhusu familia kukutegemea BONGO hapa kila mtu anategemewa na familia yake tena wewe na elimu unayo? ndo kabisaaaa!!! maana hapa waliowengi wanaotegemewa ni darasa la saba na wanategemewa na familia kubwa ajabu.

Lakini Msomi yeyote hawezi kushindwa maisha hata kidogo labda awe alinunua cheti, maana mtu yeyote aliyefika chuo kikuu anajifunza pia kutawala, na si kutawala watu tu, hata na kipato anachokipata anajua jinsi ya kukitawala.

Zaidi ya hayo ukija kidini Mungu hamtupi mja wake atakufungulia njia tu utafanya kila kazi hata uvuvbi maana wavuvi nao wanamsemo wao kuwa mgaagaa na upya hali wali mkavu!!!! Karibu BONGO,.
 
Jamani naomba ushauri. Mimi ni kijana mdogo tu. Nilikuja Marekani kwa taabu sana mwaka 2000 na kwa kudra za mwenyezi mungu niliweza kumaliza shule baada ya miaka nane. Sio kua masomo yalinishinda ila mambo ya fedha. Semester hii nimeingia, inayofuata inabidi nikusanye ada. Nashukuru nimeweza kupata shahada yangu. Kwa jinsi nilivyomaliza, nilifanikiwa kupata offer za kazi kadha lakini mambo ya makaratasi ni magumu sana. Nilijaribu kuongea na kumlipa mama mmoja wa kinugu lakini kila wiki anataka hela sasa nimeshindwa.
Nyumbani kwetu Dar es Salaam ndugu zangu wananishauri nirudi kwasababu kwa vile nina degree ya biashara kazi sitokosa. Naomba ushauri ndugu zangu. Kwani nimejaribu sana mbinu zote ninazozijua America lakini naona system inanibana. Laiti kama ningekua nina green card, ningekua ninapeta vibaya mno. Je, wanaforum, mnanishauri vipi?

1):Mr. Billionea, kama uko Marekani jaribu na jitahidi kutafuta kazi yeyote ya kukupa $3000.00 kwa mwezi kusanya tractor kama 4 used na irrigation equipment ambazo gharama zake ni kuanzia $1500 mpaka $5000.00 Tafuta shamba kubwa la hecta 100 hapa Tanzania Morogoro/Mbeya/Pwani/Mtwara lima (Mpunga/Matunda kama Mangoes/Nanasi/ etc) kwa miaka 2 utakuwa billionea kweli kweli.

2): Chukua Machine ya kutengeza Ice cream/Sausage gharama zake ni ndogo sana (kwa $5000.00) utapata kiwanda kizuri cha kuanzia kuchinja ng'ombe kama 5 kwa siku kwa ajili ya Sausage. Baada ya Miaka 2 utakuwa billionea.

3): Chukuwa machine za kutengeza mikate (gharama zake ni $3,000.00 mpaka $5,000 ya kutengeneza mikate 10,000 kwa siku. baada ya miaka 2 utakuwa billionea.

uo ni ushauri wa bure, kusoma kwa ajili ya kuajiliwa kumepitwa na wakati.
 
Dogo Bilionea, I even like your ID lakini yaelekea unaanza kuchemsha mapema wakati una ndoto za kuwa bilionea. Look here boy! acha kuruka ruka huko kama huna mpango mi nina imani kwa kuwa nyenzo muhimu unayo (your degree) rudi bongo kazi zipo na michongo mingine kibao huwezi kufa njaa. Jamani hebu acheni utani mbona sisi tulioteremka tu kutoka pale mlimani maisha ni mswano na ajira hazikututoa jasho sana kiasi cha kuanza kuulizia na god fathers wakati uko ghaibuni.

Mi nakushauri fungasha rudi bongo haya mambo yanayoendelea huku wala yasikutie pressure ukaanza kuogopa afterall sasa hivi dunia ni kijiji ukiona bongo hakieleweki unasogea maeneo mengine kibao watu sasa wanapata ajira hata katika nchi jirani za africa kama DRC, Uganda, Zambia, Botswana, South Africa (forget what happened recently). Muhimu ni shule yako kama ni kiwango unapeta mdogo wangu!!!! Tena hata hiyo option ya ujasilia mali still u' can make it in Bongo na ukafanya vizuri tu. Unataka mshahara wa kiasi gani mpaka unaogopa hata kurudi kwenu??? Utaaibikia ugenini sijui utajificha wapi????
 
Back
Top Bottom