Naomba ushauri wenu wana JF

Kichasi

Member
Aug 30, 2011
61
13
Kwanza natanguliza shukran zangu kwenu.Nina iman kubwa kwamba nitapata ushauri wa kunijenga kutoka kwenu. Mimi ni kijana niliye hitimu masomo yangu mwaka huu kwa ngazi ya shahada.Katika kipindi chote cha masomo tangu darasa la kwanza mpaka hapa nilipofika,nilikuwa napata support kutoka kwa mama yangu na ndugu wa upande wa mama yangu tu.Najua watu watajiuliza kwanin,ila hili lilisababishwa na kutokuelewana kati ya baba na mama yangu ambako kulipelekea kuvunjika kwa familia.Kwa hiyo kipindi naanza darasa la kwanza niliandikishwa kwa jina la ukoo wa mama yangu ambalo ndio jina ninalitumia mpaka sasa. Sasa tatizo langu liko kwenye jina,mfano unaweza kufika mahali ukajitambulisha kama kama mchaga lakini jina lako la ukoo unalotumia ni la kisukuma,Je hamuoni kama inachanganya watu? Au nibadilishe jina?. kwa hiyo wana jf naomba ushauri wenu uwe specific kwenye jina kwa sababu hayo mambo mengine ya migogoro nimeshayafanyia kazi.
ASANTENI.
 
Hakuna tatizo bana, mbona kuna watu wanaita John lakini ni swala tano. Au Said kumbe anapata sakramenti bila tatizo.
Tena hilo ni la kiimani sembuse habari ya jina la kikabila ambalo halina "complication?"

BTW hao uanowahofia kwani wanataka kujua kabila lako ili mkatambike?
 
Tanzania hatuulizani makabila na kama wanakuuliza nadhani ni wakabila hao. kwani ungezaliwa kwenye desturi za koo zinazotumia majina ya upande wa mama ungeomba kufanya vinginevyo? Achana na mambo ya jina songa mbele.. La ukipenda kaape mahakamani kuwa wewe ni John Masanja Masawe
 
Unaonekana wewe una ukabila ndani ya nafs yako ndiyo unaokusumbua, kwangu mi naona ni ujinga kwa msomi kama ww kuumizwa na ukabila, lete jamvin mambo ya mcng na siyo kutuletea habar zako za ukabila hapa.
 
Nyanidume kama hukuwa na ushauri ungempotezea tu kuliko kutumia maneno makali.

Kichasi mie nadhani kinachokusumbua si kabila bali unahisi umekosa identity kwa upande wa baba yako. Ili uwe na amani unaweza kwenda kwa Wakili kuandaliwa kiapo (DEED POLL ON CHANGE OF NAME) cha kubadili jina kwa kuongeza jina la ukoo la baba yako mbele ya majina yako ya sasa (hii itasaidia majina yasiwe tofauti sana na unayotumia sasa). Baada ya kusaini hicho kiapo unapeleka kwa Msajili wa Hati kwa ajili ya kusajiliwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali. Hapo utakuwa na majina yanayotambulika kisheria mahali popote. Wengi huapa kisha hawasajili lakini kisheria kuapa kubadili jina bila kusajili ni sawa na zero.
 
ukijitambua wewe binafsi...

ukajikubali kujipenda kujithamini....

hutohangaika kuhusu jina, ubini, kabila wala mitazamo ya wengine
 
mbona haina tatizo hiyo.inatakiwa ujiamini bwana.mimi jina langu na nilipotoka ni tofauti.na lipo tofauti na dini yangu,na wala hainisumbui kabisa.na nilipewa na wazazi wangu.
 
sasa we unaishi kwa kuridhisha watu au unaishi kwa uhalisia wa maisha yako? achana na mambo ya jina ooh hili ni la kichaga, kisukuma, muhimu ni kuangalia ukweli halisi wa vipi wewe jina lako likawa hivyo! mi sioni tatizo kuhusiana na jina, usiwe na mashaka kwani haina tabu kabisa..pole kwa usumbufu huo, ila sio ishu endelea tu jina lako ulilopewa.
Kwanza natanguliza shukran zangu kwenu.Nina iman kubwa kwamba nitapata ushauri wa kunijenga kutoka kwenu. Mimi ni kijana niliye hitimu masomo yangu mwaka huu kwa ngazi ya shahada.Katika kipindi chote cha masomo tangu darasa la kwanza mpaka hapa nilipofika,nilikuwa napata support kutoka kwa mama yangu na ndugu wa upande wa mama yangu tu.Najua watu watajiuliza kwanin,ila hili lilisababishwa na kutokuelewana kati ya baba na mama yangu ambako kulipelekea kuvunjika kwa familia.Kwa hiyo kipindi naanza darasa la kwanza niliandikishwa kwa jina la ukoo wa mama yangu ambalo ndio jina ninalitumia mpaka sasa. Sasa tatizo langu liko kwenye jina,mfano unaweza kufika mahali ukajitambulisha kama kama mchaga lakini jina lako la ukoo unalotumia ni la kisukuma,Je hamuoni kama inachanganya watu? Au nibadilishe jina?. kwa hiyo wana jf naomba ushauri wenu uwe specific kwenye jina kwa sababu hayo mambo mengine ya migogoro nimeshayafanyia kazi.
ASANTENI.
 
Nyanidume kama hukuwa na ushauri ungempotezea tu kuliko kutumia maneno makali.

Kichasi mie nadhani kinachokusumbua si kabila bali unahisi umekosa identity kwa upande wa baba yako. Ili uwe na amani unaweza kwenda kwa Wakili kuandaliwa kiapo (DEED POLL ON CHANGE OF NAME) cha kubadili jina kwa kuongeza jina la ukoo la baba yako mbele ya majina yako ya sasa (hii itasaidia majina yasiwe tofauti sana na unayotumia sasa). Baada ya kusaini hicho kiapo unapeleka kwa Msajili wa Hati kwa ajili ya kusajiliwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali. Hapo utakuwa na majina yanayotambulika kisheria mahali popote. Wengi huapa kisha hawasajili lakini kisheria kuapa kubadili jina bila kusajili ni sawa na zero.

Nakushukuru sana mkuu,kwa ushauri wako uliojaa hekima.
 
.....Inaelekea hulipendi hilo jina la ukoo la upande wa mama yako vinginevyo sioni sababu ya kutaka kulibadili hata kama ni jina ni la kisukuma na wewe kabila lako ni mchanga. Kama linakukera basi fanya taratibu husika ili ulibadili.
 
Back
Top Bottom