Kwanza natanguliza shukran zangu kwenu.Nina iman kubwa kwamba nitapata ushauri wa kunijenga kutoka kwenu. Mimi ni kijana niliye hitimu masomo yangu mwaka huu kwa ngazi ya shahada.Katika kipindi chote cha masomo tangu darasa la kwanza mpaka hapa nilipofika,nilikuwa napata support kutoka kwa mama yangu na ndugu wa upande wa mama yangu tu.Najua watu watajiuliza kwanin,ila hili lilisababishwa na kutokuelewana kati ya baba na mama yangu ambako kulipelekea kuvunjika kwa familia.Kwa hiyo kipindi naanza darasa la kwanza niliandikishwa kwa jina la ukoo wa mama yangu ambalo ndio jina ninalitumia mpaka sasa. Sasa tatizo langu liko kwenye jina,mfano unaweza kufika mahali ukajitambulisha kama kama mchaga lakini jina lako la ukoo unalotumia ni la kisukuma,Je hamuoni kama inachanganya watu? Au nibadilishe jina?. kwa hiyo wana jf naomba ushauri wenu uwe specific kwenye jina kwa sababu hayo mambo mengine ya migogoro nimeshayafanyia kazi.
ASANTENI.
ASANTENI.