Naomba ushauri wenu wakuu kuhusu kuzamia United kingdom

Mayor Slum

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
751
1,121
Mimi ni kijana mjasiriamali mdogo pia nimebahatika kisoma mpaka chuo kikuu
Nikatafuta kazi kwa miaka miwili hola sasa nimeamua kujiajiri hapa kwa kufanya biashara mdogo ndogo

Pia nilikuwa nalengo za kuzamia huko majuu kwa sababu biashara ndogo ndogo nayofanya naona hanilipi pia nimebahatika kusoma nyuzi humu za kuhusu kuzamia majuu nimevutiwa sana hasa baadhi ya watu humu walinimotivate sana kwenye uzi moja na mimi huwa nikiona fursa silali mbali kichwa kinaanza kusaka mchongo na shauku ya kufanya hicho kitu

Sasa juzi nimebahatika kufahamia na mbibi mmoja huko fb baada ya kuwa marafiki nikaona sms inakuja anasema amevutiwa na issue nazo fanya yaani kuhusu swala la maisha na biashara ndogo ndpgo .Nikamshukuru sana nikwambia asante ila sms anayofata nikashangaa ananiambia

Can i ring you?

Nikashutuka nikatulia sijamjibu kitu
Pia nimechunguza nimeona nayeye afanya maswala.ya ujasiriamali pia kaajiriwa yuko divorced na anamtoto mmoja mdogo ila ni mrembo

Sasa nimekuja humu naomba ushauri kidogo lengo langu kubwa hapa kama huu unaweza kuwa mwanya wa kuzamia majuu nikasake maisha

Sasa naomba mnishauri hapa
Huyu mbibi anavyoniambia Can i ring you ? Ndio anataka nini for sure anipe mwanya nizamie majuu au anivishe pete tuwe wachumba niende majuu japokuwa nimrembo ila mimi kudate na mtu (mbibi) alienizidi umri duuh naona kama laana tu ila sababu ya ugumu maisha nafikiria kokamaa nizamie

Au nimkatalie nimwambie tuwe marafiki nimwambie anifanyie mpango nipate kazi au scholarship au chuo chochote cha course ya kuzuga zuga au kwenye masemina anayofanya iliniweze kwenda huko mambo yakiwa sawa naondoka na kwake kabisa

Wajanja na mliofanyikiwa kuzamia majuu ebu naombeni mnipe akili zaidi hapa nifanye nini ??

Pia hata nikienda UK mimi nikishapata visa na kusoma ramani ajue tu nitakula kona moja matata sana
Hapa bongo nimekaa ajira hakuna miaka miwili.sasa nipo kitaa napata hela kidogo sana kwenye biashara hata kupiga hatua naona hakuna na dharaulika tu na kisoma kwangu

Na Mzee Magu kabana sana mtu unatumia miaka 17 kusoma.ukija mtaani unaanza upya tena na umri unakimbia tu






Sent using Jamii Forums mobile app
 
We kichaa kweli , yaani badala upokee simu unakuja kutuuliza sisi ni nini alitaka akuambie? Bado hujajielewa

Sent from my Device using Tapatalk
 
Mkuu hakuna sio Simu ni message hajapiga simu ni message kama unavyoona hapo chini matusi sio fresh Mkuu kuitana vichaa tena
Screenshot_20200111-131342-1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Usitupotezee muda.Yaani tukushauri kuhusu kupigiwa simu.Haya mwambie akupigie,halafu mtakachoongea,kilete hapa tukashauri.Umejuaje kwamba atazungumzia nini na wewe.Akikuambia ameona picha yako,Kati ya abiria waliokufa kwenye Ndege ya Iran?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mcheki mmalizane ndio uje hapa tuyajenge mzee.


Anyways.

Kila mtu ashinde mechi zake!
 
Can i ring you? = naweza kukupigia
Mtoa mada: can i ring you? = naweza kukuvalisha pete?? Mwanaume havalishwi pete...

Ushauri....
-usiwe na pupa ongea nae masuala hayo hayo yaliowaunganisha na wala usiwe na haraka -

-waafarika haswa magharaibi wanafahamika kama matapeli wa mtandaoni mara nyingine anataka kuhakikisha sio scammers ni mtu kweli anaepiga nae soga mtandaoni.

-Jenga urafiki wa kawaida usiweke tamaa mbele mengine yatafuata.

- mfanye ajione wa thamani na anaependwa kwa dhati na rafiki yake wa kweli. Kwa wasifu wake anaweza kuwa mpweke asie na mtu wa kuongea nae mambo ya moyoni au aisepata hits nyingi hasa kwakuwa ni mtalaka jua limeshamzamia. Hivyo ukiliziba hilo pengo utaenda majuu...usiwe na pupa.

- Mfanye akuzoee kama rafiki na mtu muhimu unaemjali, ukiweza mtumie hata vijizawadi kwa dhl visivyo na gharama.
 
Hilo ni Jibaba ndani ya Lagos Nigeria, linakuvuta tu , siku litakwambia inahitajika fee ya sijui permit mara sijui fee ya hii document, we ingia kingi tu
 
Back
Top Bottom