Naomba Ushauri Wenu Wajuzi Wa Sheria Au Waliowahi Pitia Ishu kama hii

AVO28

Senior Member
Jan 4, 2018
140
240
Salaam Wakuu.
Naomba ushauri kwa wajuzi wa sheria au hata wasio wajuzi wa sheria lakini wamepitia ishu kama yangu.

Kufupisha Stori,

Nilinunua Viwanja viwili maeneo ya tabata, viwanja hivi vipo kwenye eneo la sqm 6000+ (Lina hati ) mimi nimenunua maeneo mawili ndani ya eneo hilo kubwa, na maeneo niliyonunua mimi yana ukubwa wa sqm 800 kwa ujumla, Moja sqm 500 lingine sqm 300. Huu hapo

ni mkataba wa mauziano baina ya mimi na mwenye hilo eneo

Ishu iliyokuja kutokea wakuu ni kwamba baada ya malipo ya kukamilika huyo mwenye eneo tulikubaliana kwa mdomo tu kwamba haraka iwezekanavyo baada ya malipo process ya sub-division ianze ili eneo langu litoke kwenye eneo lake kubwa kisha nianze mchakato wa kuomba survey na kisha hati yangu. Sasa huyu muuzaji amekuja kua msumbufu sana kufanya process ya sub-division tena baada ya kupokea pesa.

Ili sub-division ifanyike kwa mujibu wa maafisa ardhi ni kwamba hatua ya kwanza ni muuzaji kuandika barua ya kuomba kufanya sub-division na kuambatanisha hati yake original kwenye hiyo barua pale ardhi kisha hatua nyingine zinafata, sasa huyu muuzaji huu ni mwezi wa pili hataki kupeleka hati na kuandika barua ya ku surrender hati ili mchakato wa sub-division uanze.

Huyu muuzaji ni mzee wa miaka 70+ na namuheshimu mno wakuu, lakini nimejaribu kila namna kumueleza kwamba mimi nataka kuanza ujenzi mapema iwezekanavyo hivyo nahitaji hyo hati ipelekwe ardhi ili ifutwe na mchakato wa sub-division ufanywe ili niweze kujenga lakini naona hanielewi kila siku ananambia kesho kesho kesho.

kama wiki 2 zilizopita ilinibidi niende polisi kumfungulia kesi ya kutaka kunizulumu (Kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu) kwakua majibu yake aliyokua ananipa niliona kabisa kuna dalili za kutapeliwa hapo, akaitwa polisi na alipoulizwa kwanini mpaka leo hataki kupeleka hati kule ardhi anasema anataka utaratibu ufwatwe na alipoulizwa utaratibu gani akasema sub-division na alipoulizwa ili sub-division ifanyike hatua ya kwanza inapaswa kufatwa ni ipi akasema anataka surveyer wake (Personal) aje kufanya survey kwanza kisha ndo apeleke hati, kwa bahati nzuri nna rafiki yangu naye yuko kwenye ofisi ya surveyor pale ardhi manispaa nikampigia mda huo huo mbele ya polisi ili atupe utaratibu wao kama ardhi. akasema kumuita surveyer kufanya survey eneo ambalo lina hati tayari (Means lilishafanyiwa survey) ni uongo. pia akatuambia kwamba huyo mzee pia anamakosa kwakua ameuza eneo ambalo tayari lipo ndani ya eneo kubwa lenye hati means alitakiwa afanye sub-division kwanza ndio auze (Mimi sikua nafahamu haya ningejua mapema nisinge mpa hela mpaka afanya sub-division kwanza), so baada ya mvutano mvutano mwisho wa siku akakubali na aka ahidi mbele ya polisi kesho yake ataenda ardhi aandike barua na apeleke na hyo hati lakini mpaka leo tunavyozungumza wakuu huyu mzee ananipiga chenga tu na huko ardhi hataki kufika.

Sasa nisiwachose sana, ninachoomba hapa ni ushauri kwenye ishu kama hii ambayo kusema ukweli ndio mara yangu ya kwanza kununua ardhi kwa mtu na nilikua sina experience sana na pia kwa nilivyomuona huyu mzee mara ya kwanza kua ni mzee wa dini mno na mstaarabu na umri umeenda mno sikujua kama angebadilika na kua mtu wa sound kiasi hiki. so wakuu kwa ishu kama hyo mnanishauri nifanye nini ili kupata haki yangu?

Maana pia niongezee mwenzi mmoja baada ya kununua eneo nilivyoona dalili za utapeli nikaenda nikazungushia ukuta eneo lote nilililonunua nikiwa na lengo kwamba pengine atakuja pale kwenye eneo kuonana na mimi ili tulimalize hili swala lakini wapi (nimeishia kufatiliwa tu na serikali za mitaa wakitaka kibali cha ujenzi ambacho sina ila bahati nzuri baada ya kuwaelezea situation walinielewa) nimekuja kumuona huyo mzee juzi juzi tu tena ni baada ya kuitwa na polisi, yani tangu ninunue eneo ndo nimemuona hyo juzi juzi nnayosema.

sasa naona kabisa kuna dalili za kutapeliwa hapa wakuu japo mpaka sasa siamini kwamba mzee kama yule anaweza fanya utapeli kizembe namna hii maana hata polisi wala hakani kwamba hajaniuzia anakubali. Ila nlichogundua ni kwamba huenda ana jutia kuuza eneo lake kwakua limekaa vizuri na pengine angekua na subira angeuza kwa bei kubwa zaidi aliuza kwakua alikua ana deni somewhere so alikua hana jinsi, na ndio maana kuna kipindi kama wiki 2 baada ya mauziano alikua anasema natafuta hela nikurudishie kwasababu unanisumbua sana, mi nikamwambia nataka kiwanja sitaki pesa, sasa pengine nahisi aliniuzia ili kupooza deni lake analodaiwa huku akiwa na mategemeo kwamba sitajenga pale (Kama mkataba unavyosema) alaf baada ya mda akiipata hyo hela aseme imeshindikana kufanya sub-division so nakurudishia pesa yako.

Wakuu embu nishaurini niende nae vipi mtu wa namna hii maana na mimi nahitaji kuanza ujenzi wa nyumba pale haraka muda unazidi kwenda lakini sitaki kuanza bila lile eneo kutolewa kwenye eneo lake kubwa.

Nilifikiria nimpeleke mahakamani lakini nimegundua hata yeye anataka niende mahakamani kwa maana ana watu wazito huko juu na wanasheria kibao so anajua huko atanibana kwa namna yake. mke wake tu ni judge mkubwa tu na watoto wanasheria so nimeona nisikimbilie huko kwanza ndo maana nimeleta hapa hili bandiko nipata mawazo ya wadau juu ya namna bora ya kuisolve hii issue.

Poleni kwa kuwasomesha uzi mrefu hivyo. ni kwamba nimekereka sana na nna hasira mno na huyu mtu kiasi kwamba nikiendelea nae mimi kama mimi bila mawazo mapya kutoka kwenu nnaweza kujikuta namzabua makofi nikitukata nae tena.
 
Kabla ya yote naomba utambue kwamba huyo mzee hajakutapeli kwani kuna mkataba hapo. Pia Polisi hawashughuliki na masuala ya ardhi mkuu. Huko utapoteza muda tu na pesa zako.

Kadhalika, why have you disclosed the document showing the names of the Advocate who witnessed your sale agreements? Siyo uungwana hata kidogo mkuu.

MAPUNGUFU YA MKATABA WENU.
Kwanza mkataba huo una mapungufu kibao mkuu. Mkataba ilibidi ueleze ni kwa muda gani hiyo subdivision itafanyika. But mkataba wenu upo silent juu ya hilo. Aidha, ilibidi ueleze kwamba baada ya kutia saini au dole katika mkataba inabidi MNUNUZI upewe nyaraka zote zinazohusu hicho kiwanja ila mkataba upo kimya.

Pili, wewe kuna kifungu hicho cha mkataba kinakubana kwamba hautafanya maendeleo yoyote mpaka subdivision iwe imefanyika hati zimepatikana na una kibali cha ujenzi.

Tatu, kuna kifungu kinasema kwamba yote hayo yakishindikana utarudishiwa pesa yako. Kitu ambacho kwa upande wangu hakija kaa sawa hicho kifungu.

Kadhalika, mkataba unakubana sana mkuu maana muda wowote huyo muuzaji akipata mtu akampa hela nzuri hakika atakurudishia pesa zako kwa kuegemea kifungo cha mkataba kinachosema kwamba subdivision ikishindikana itabidi akurudishie pesa.

SULUHISHO.
-Acha uoga mkuu nenda mahakamani. Kuwa na jaji au wanasheria siyo kigezo cha kutaka kukufanyia dhuruma ya kiwanja chako. Nawe tafuta mwanasheria ambaye atakuongoza katika hili. I'm ready for that if you gonna agree with my terms.

- Mfungulie kesi mkuu. Katika kumfungulia kesi omba mahakamani ikupe zuio( stop order) ili MUUZAJI asije uza au kufanya chochote katika kiwanja hicho.

- Pia omba mahakamani itoe amri huyo jamaa akupe nyaraka zote zinazohusu hicho kiwanja na pamoja na hiyo barua ya kufanya subdivision.

- Omba mahakama itoe amri kwa MNUNUZI kutenda majukumu yake katika mkataba ikiwa ni pamoja na kuharakisha hiyo subdivision.

-Omba mhakama itamke kwamba wewe ndiyo mmiliki halali wa kiwanja hicho kufuatia makubaliano mlioingia wa mauzo ya kiwanja hicho.

ENDAPO HUTAKI KIWANJA.

- Nenda mahakama ya kawaida anbayo ni Ilala pale kinyerezi umfungulie kesi ya madai. Ukidai fedha zako taslimu ulizomlipa na fidia.

AU

Kaa na huyo mzee ongea nae vizuri in a friendly way acha jaziba, kiburi etc mwambie upo tayari kugharamia hiyo subdivision ifanyike ili hati zitoke haraka iwezekanavyo mkuu. Chukua hata 50k mpatie hiyo mzee na siku mnaona mwambie aandae hiyo barua ya kuomba kufanya subdivision ili iweze kurahisisha hiyo subdivision mkuu.
 
Shukran kwa mchango wako mkuu, Kuhusu kuonyesha jina la mwanasheria ni kweli nilipaswa kuziba hapo ndio maana nimezifuta kwanza hizo documents ntazipandisha tena nikisha ziba hapo.

Kuhusu mapungufu ya huo mkataba kama nilivyosema sikua na experience na mambo hayo so hata mwanasheria alipotuletea huo mkataba sikuweza kuona mapungufu yake kwa haraka haraka. Nilikuja kugundua baadae sana kwamba mkataba unanibana mimi mnooo kuliko muuzaji.

Swali kuhusu sulihisho: Kwa experience yako nikifata ushauri wako nikaiomba mahakama hayo uliyonieleza (Ili kupata kiwanja) je inaweza kuchukua muda gani mpaka mahakama kutoa maamuzi ya mwisho?

Kuhusu hilo swala la kuongea na mzee na ku offer kugharamia sub-division nilisha jaribu kulifanya lakini sikufanikiwa mzee aliniitikia tu lakini kwenye kutekeleza ndio usumbufu.
 
Back
Top Bottom