Naomba ushauri wenu wa kisiasa.

Mkomawatu

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
267
118
Habari zenu wadau wenzangu wa JF, kwa kuthamini mchango wenu katika masuala mbalimbali ya kisiasa hapa nchini, nimeamua kuandika waraka huu kuomba ushauri wenu kwenu namna ambavyo naweza nikaendesha harakati zangu za kisiasa kwa lengo la kuwakomboa watu wa tabaka la chini ulimwenguni kote, nimemaliza chuo kikuu cha Dodoma ambako kule nilishika nafasi ya Mbunge serikali ya wanafunzi, lakini pia nilikuwa miongoni mwa wadau waandamizi katika Jumuiya ya Vijana Umoja wa mataifa tawi la UDOM na pia mdau mwanzilishi wa Anti corruption society pale chuoni, naomba ushauri wenu ni taasisi gani naweza nikajiunga nayo na kuweza kufanikisha ndoto zangu? Nataka Watanzania na dunia ifaidike na uwepo wangu.
 
Habari zenu wadau wenzangu wa JF,kwa kuthamini mchango wenu katika masuala mbalimbali ya kisiasa hapa nchini,nimeamua kuandika waraka huu kuomba ushauri wenu kwenu namna ambavyo naweza nikaendesha harakati zangu za kisiasa kwa lengo la kuwakomboa watu wa tabaka la chini ulimwenguni kote,nimemaliza chuo kikuu cha Dodoma ambako kule nilishika nafasi ya Mbunge serikali ya wanafunzi,lakini pia nilikuwa miongoni mwa wadau waandamizi katika Jumuiya ya Vijana Umoja wa mataifa tawi la UDOM na pia mdau mwanzilishi wa Anti corruption society pale chuoni,naomba ushauri wenu ni taasisi gani naweza nikajiunga nayo na kuweza kufanikisha ndoto zangu? Nataka Watanzania na dunia ifaidike na uwepo wangu.

...kabla hata ya kupata ushauri,je wewe umeishafanya utafiti wa kujua hao unaotaka kuwakomboa wanahitaji ukombozi wa aina gani?...ukisha lijua hilo itakuwa rahisi kujua ni chama gani kinakufaa kufikia malengo yako ya kuikomboa jamii uliyopo...
 
kama wewe ulikuwa mshiriki mzuri wa siasa za chuo na hizo civil right movement basi wewe mwenyewe utakuwa unajua wapi uelekee ambapo pana endana na ideology ulizonazo

kwa mfano nikikwambia nenda ccm ukikataa maanake unajua wapi panakufaa
 
Ushauri wa kisiasa:

Jiunge na wanaharakati pamoja na chama kinachoonyesha dhamira ya dhati katika ukombozi wa pili.

Karibu CHADEMA
 
udom kwa nafasi yako ww kama kiongozi uliwakomboaje wanafunzi wenzako ktk matatizo ya chuo hafu then angalia jamii yako ikoje
 
Nashukuru kwa nyote mlionipa ushauri wenu,naahidi kuufanyia kazi kwa maslahi ya taifa letu,Afrika na Dunia kwa ujumla.Wasalaam.
 
Back
Top Bottom