Naomba ushauri wenu: Nipo kwenye process za mwisho kufungua kampuni yangu..

Mtapenda

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
1,115
2,055
Habari za majukumu ndugu zangu

Naamini jamii forums ni mtandao wa kijamii ambao umejaza watu wenye uelewa mpana na wenye shughuli mbali mbali...

Binafsi sipendi kuajiriwa Bali napenda sanaa kua na shughuli zangu binafsi.. na ndoto kubwa ni kua na kampuni yangu na sasahivi nipo kwenye hatua za mwisho kampuni isajiriwe... Kama tunavyojua kwenye kampuni unaweza fanya shughuli yoyote.. (kilimo, biashara, kutoa services)

Najua wapo watu humu wana kampuni zao na zinachapa kazi kweli kweli.. hivyo basi naomba nijifunze kitu kupitia kwenu pamoja na kupata ushauri wenu... Pamoja na kupewa fursa zilizopo

Naomba sanaa wajuzi na wabobezi mnipe ushauri ni biashara gani ambayo naweza anza nayo japo kwa mtaji mdogo kupitia hii kampuni yangu....

Ama nawezaji kupata tenders kwa hapa nchini ama nchi za nje ambapo naweza kuzifanya mfano wanao uza mazao ya chakula ama mazao ya biashara (korosho, kahawa, kokoa n.k) nje za nchi ni njia gani mtamumia japo nami nianze japo kwa kidogo ili nipate ujuzi...

TUPEANE FURSA WA NDUGU PAMOJA NA USHAURI.. NATARAJIA COMMENTS ZA KUNITIA MOYO NA SI ZA KEJELI AMBAZO HAZINA FAIDA YOYOTE..

NAKARIBISHA USHAURI WENU WAJUZI MIMI NI KIJANA WENU NAPENDA KUA KAMA NINYI...

AHSANTENI
 
Pia kwa wanao penda kunishauri private ni pm mnijenge... Najua zipo fursa ndogo ndogo kwa kampuni changa ambazo naweza anza nazo pia najua mpo watu wenye hizo fursa humu ndani..
 
Ushauri katika masuala mbali mbali hasa ya kibiashara, sheria, afya na n.k unalipiwa ndugu, huwezi kupata ushauri wenye tija bure bure tu, sawa sawa?
 
Kufungua kampuni kwani ni kazi ngumu?tuanze na mtaji Kwanza,uko vipi hapo?mtaji sio lazima cash money,ww una nini?
 
Mpk hapo umeshafeli.

Huwezi kufungua Co. bila kujua unataka kufanya biashara gani.

Na shida sio kufungua Co. ila shida ni kupata wateja/kuuza bidhaa/huduma.
 
Kwani wewe ulipanga kufanya nini? Pia, hebu tupe jina la kampuni uliyosajili ili tukushauri biashara ya kufanya inayoendana na jina. Kwa mfano, kama jina la kampuni ni "JIWE FOOD SUPPLY Co Ltd" unategemea utapata tenda ya vifaa vya ujenzi?

Ulitakiwa kwanza ufahamu unaenda kufungua kampuni itakayojishughulisha na nini!
 
Back
Top Bottom