Naomba ushauri wenu juu ya mambo haya, maana mwenyewe imefika mahali nimeanza kukata tamaa

Hakuna mtoto wa tajiri anacheza Forex, FX sio ishu yakitoto inaumiza akiri na kuitesa naona umeandika uvivu mtu aliyefanikiwa kwenye Forex ni mtu alikita akiri kisawasawa kichwa kilichoelewa FX sikichwa cha kawaida cha kivivu ndio maana nikakwambia usitegemee kumuona mtoto wa MO anakaza medulla yake kuisoma FX yanini nawakati Mtaji tiari anao.

Elewa hiki Forex ni Hustle ya kuRise Fund sasa mtoto wa tajiri tiali iyo Funding power teyari ipo anachohitaji yeye ni ku-start Business tu ila wewe mtoto wa Mzee Dulla lazima uminye mishipa kuRise Fund.
Mkuu matajiri wa forex wataanza kuinekana baada ya miaka 5. Achana na huyo mbishi, watu wanafikiri forex ni sawa na kulima tembele, kwamba leo unapanda baada ya wiki 2 unaanza kuchuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah pole sana mkuu. Mi imani yangu inaniambia wanaofanikiwa zaidi kwenye forex ni wale wasiotumia pesa za mawazo, ukiwa na biashara zako kadhaa zinazunguka then ukakomaa na forex inaweza kuwa rahisi kumake kuliko upo na forex only ndo utokee hapo hapo lazima utapoteza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu pole sana, hii biashara bwana usipokua makini unaweza kuwehuka....
 
Mkuu ninazo biashara zinazoniingizia kipato cha kununua ninachotaka. Hiyo forex mtu anapoteza 70M, 20M, 10M acheni masihara na pesa, pesa inataka heshima. Usiinvest pesa kwa jambo ambalo hulifahamu.
Sent using Fly in any Weather.
CASH MONEY FOREVER hawa watoto wanaotaka mihela ya ndotoni huwa natamani nikawapige hawaelewiwanaweza iba mipesa ofisini yote akayaingiza kwenye Internet
 
nakubaliana na wew asilimia nyingi wanataka wafanye forex tu wanasahau kama wakipata faida inawabidi wafanye na biashara nyingine wanaishia kueka lot tembo kinachuwakuta ni kuchoma account na kutumia lot sisimizii😀😀😀
Dah pole sana mkuu. Mi imani yangu inaniambia wanaofanikiwa zaidi kwenye forex ni wale wasiotumia pesa za mawazo, ukiwa na biashara zako kadhaa zinazunguka then ukakomaa na forex inaweza kuwa rahisi kumake kuliko upo na forex only ndo utokee hapo hapo lazima utapoteza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ka pitie trading psychology.Tamaa inakuponza.Na kwa namna unayopoteza pesa kwa staili ile ile kila mara inamaanisa hujifunzi kutokana na makosa yako kwenye market.
By the way wekeza sehemu nyingine pia usiegemee fx tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeanza kusikia forex since 2017 nikazama quora nione majibu yaliyotolewa kutokana na maswali kuhusu forex nikaona negative answers nyingi Sana jibu la kawaida ilikua ni so difficult na is not easy hapa ndipo nikapata jibu Kama watu wanaoshi huko globalization iliko anzia wanasema ngumu sasa inakuaje kwa sisi watu walimwengu wa tatu jibu ikawa ni ngumu. Sasa kwa mm maoni kwa vijana wenzangu mm naona mda ambao watu wanautumia kusoma forex na pesa zinazopotea kwenye hii ishu zinaweza kugeuzwa kuwa kitu kikubwa ambacho kinashikika kinarithishika kinasomeka lakini forex ina scam nyingi. Mm naona biashara ni nyingi mno hata humuhumu mtandaoni fursa ni nyingi Sana ukiachana na hii inayowapa vijana matumaini makubwa kumbe ngumu hatari. Pamoja na hayo kutegemea Sana biashara za mitandaoni kuwa first priority ni utumwa. Mungu ametupa aridhi ya kutosha kuna milima, mabonde, tambarale na inaweza kufanyia shughuli kibao hata simu tunazo tumia zinatoka aridhini Sasa kwanini tuone kuwa fursa ni mpaka tununue bidhaa nakuwapa pesa watu wengine kizembezembe nakati unaweza tengeneza Cha kwako ambacho kinarithishika
 
Umeandika vyema...Mimi pia siifaamu FOREX Ila kila nikitaka nijifunze Kuna Roho inaniambia kua Makini na Mshahara wako wa kila mwezi unaoupokea....
Negative Comments zimekua nyingi kuliko Positive feedback.
 
Daaah ya mkuu usidanganywe tafuta biashara halisi ukomae nayo.
Forex kama betting ni ikutoe au ikifilisi kabisa. Sasa ili kuepuka hilo inabidi usiifanye kama chanzo kikuu cha mapato.

Embu mtafute sirjeff denis instagram kuna vichache waweza jifunza.
[/QUOTE Lazima anamjua sirjeff mkuu angalia mwaka alioanza ku trade!!
 
Mnamo mwaka 1990 ndipo nilipoliona jua kwa mara ya kwanza na najua mungu alikuwa na makusudi na mimi ndiyo maana nikazaliwa, ilipofika mwaka 1992 baba yangu mzazi akafariki dunia akibahatika kuacha watoto 4 yaani kaka yangu,dada zangu wawili pamoja na mimi ndiyo nilikuwa kitinda mimba yaani mtoto wa mwisho.historia inaniambia baba yangu alikuwa akijiweza ki fedha kwa miaka hyo ya 80-90s.

Kwa sababu kuwa na gari na TV kwa kipindi hicho haikuwa mchezo na hii ilitokana na shughuli na biashara alizokuwa nazo kipindi hicho yaani maduka,kununua mchele kwa jumla kutoka mikoani na kuleta mjini pamoja na kusafirisha magogo kwa njia ya treni mpk hapa town kwahyo inavyosemekana kwa kipindi hicho chote tulikuwa hatuna shida za hapa na pale na alikuwa akitupenda mno kwa maelezo ya mama.baada ya mzee kufariki ndipo matatizo yakaanza kwa ndugu kutaka kuchukua zile mali na kweli walifanikiwa na kwa bahati mbaya mzee hakuacha nyumba bali viwanja tu na vingi wadogo zake ndy walijua vipo wapi ila kitu ambacho alifanya ni kuikarabati nyumba ya mtu kwa kuweka kila kitu yaan umeme na maji then tukawa tunakaa bure.

Sijui ni kutokana na kupenda eneo ambalo anaweza fanya biashara zake au lah? Japo bi mkubwa anadai mzee alikuwa na plan ya kujenga lakini ndy hvyo hakubahatika mpk umauti ukamfika na alivyofariki tulikaa pale kwa miaka miwili tu then tukaambiwa tuame.Maisha mapya yalianza kwenye moja ya kiwanja chetu tukabahatika kujenga vyumba 3 na maisha yakaendelea.

Kiukweli tuliishi kwa upendo na furaha tukiwa na mama yetu na alionesha kutupa sana moyo kwa maneno mazuri sana yaan kila kukicha alipenda kutwambia wanangu hata hali ya maisha iwe vipi lakini ni lazima msome maana mimi namuamini sana mungu na najua ataendelea kutupigania.kaka yangu dada zangu walionekana sio kivile kupenda shule sijui ni kutona na mazingira waliozoea kitambo na sasa yame change au vipi?

Maana wote waliishia kidato cha 4 lkn mimi nilionesha kupenda sana shule japo nimepita kwenye misukosuko sana tangu shule ya msingi mpaka chuo maana sijaenda straight.nakumbuka mwaka 2004 matokeo ya darasa la saba yakatoka na niliyapokea kwa shauku kubwa nikijua nimo maana nilikuwa najitaidi jpo sio saaaana lakini nilikuwa nimo kwahyo sikuwa na hofu ya kuwa sintofaulu tena nakumbuka nilichagua AZA BOY nilikuwa naipenda sana hii shule lkn nilipokuja kuona matokeo sikuwepo ilibidi niende shule kucheki mkeka wa maski imekuaje mm sipo na nakumbuka waliofauru walikuwa watu 8 tu na mimi kwenye riport ndy nakuaga 9 inamaana mstari ulipita kwangu na kweli kwenda kucheki nikakuta nimepungukiwa maski chache sana mwalimu akaniambia subiri unaweza chaguliw second selection lakini mimi nilishakuwa na machungu.

Basi ilibidi nitafutiwe shule morogoro nianze form one sasa pale nikakutana na rafiki zangu wanaopenda kusoma kama mimi tukaanza kupiga misuri ya kufa mtu yaani mpk form 4 wakatujua wakawa wanatukubali sana yaan utaskia madogo hawa kazi kazi.sasa ukiwa mtu wa misuri tena kwa shule za bodi ni lazima upishane na ratiba za shule kwa mfano kuamka asubuhi kufanya usafi au kwenda shamba sisi tukawa hatuamki maana unakuta umelala saa 9 au 10 alafu 11:30 kwenda shule mpk saa1 assemble sisi hatukuwahi kuonekana kwenye ratiba hyo sasa ugomvi ukawa haushi na baazi ya walimu wa zamu hakika fimbo ikawa rafiki yetu kila kukicha,baada ya walimu kuona ni kama viburi vyetu vimekisili sna nakumbuka nilipofika form 3 wakaniambia nimuite mzazi,na nilipofanya hvyo wakamueleza ya kuwa mtoto wako kwenye masomo anafanya vzr lakini anakula bangi siku hzi maana hasikii haambiwi unavyoona hapa walimu wote wamemshindwa kwahyo mama unaweza beba mzigo wako uende nao.

Sasa muda wote huo mwalimu anaongea mimi namuonea sana huruma bi mkubwa kumbuka anapenda watoto wake tusome alafu mimi ndy wamwisho then anaona dalili za mtu kuishia form 3 nikawa najiuliza maswali mengi sana moyoni bhc ikagongwa kengere ya kuita watu assemble then nikaa fimbo zangu za kuagiwa tukapewa masaa 24 tusionekane mahali pale nakumbuka mama hakusema chochote.kesho yake tukaanza safari ya kurudi Dar huku tukiongea kwenye gari mama akawa ananiuliza sasa unataka kwenda shule gani au nikupeleke jitegemee.

Sasa kwa wakati ule sio kama alikuwa na pesa sema imani yke ilikuwa kubwa sana haaminigi kwenye kushindwa nikambwambia mbona unataka kunipeleka shule kubwa sana ww nipeleke Nurulyakini pale mimi nitafauru tu mbona flani kasoma pale kafauru nikawa nampa mifano huku nikiju kwa ada ya pale ndy utakuwa unafuu wake,bhac wote kwa pamoja tukakubariana n safari ikawa nzuri tu mpk nyumbani,michakato ikafanyika nikaamia na shule ikaendelea sasa kulingana na hzi shule zetu ndogo ndogo sometime zinakuwa na walimu wachache so inakulazimu kuangaika na tuition so nikawa nashinda mchikichini kupiga mapindi siku moja mother anaenda kulipa ada anakuta jina langu limebandikwa ukutani nimefukuzwa kwa kutoenda shule siku 150 mama akashituka sana akaniita tukaenda wote ofisini sema tulivyoona ada jambo likapita na nikaambiwa nianze kwenda shule.

Nakumbuka siku nyengine ya mtihani wa moko nishapiga misuri a kufa mtu alafu natolewa kwenye paper kisa ada moyo wangu uliuzunika sana nikawahi nyumbani kuja kumwambia mother kama tunaweza kuwahi ile paper lakini tulivyofika mama akaongea na mwalimu mkuu lakini mwalimu alikataa katu katu bhac mimi na mama tukawa kwenye uzuni mkubwa sana hasa mimi nilikuwa nikimuonea huruma sna mama lakini ndy sikua na jinsi.nashukuru mungu nikamaliza vizuri kwenye kipindi cha likizo likaaza kupiga mishe za kuuza nguo yaani napoint nguo karume naanza kutembeza na nikipiga pesa narudi home na vi machungwa kumfurahisha kidogo mama au sometime namnunulia ka kuku anakula na ugali bhc mimi nafurahiiiiiiiiiii na kupata nguvu ya kesho kwenda tena......

Basi nilishi hvyo kipindi chote cha kusubili majibu na yalipotoka nilikuwa nimefeli dah hii ndy ilikuwa simanzi kubwa kwa familia maana juhudi zangu waliziona na walishindwa kujua nakwama wapi maana wanangu wote niliokuwa nakaa nao gheto walifauru kasoro mimi na baazi yao mimi ndy nilikuwa nikiwafunisha nao wapepasua kasoro mimi nakumbuka siku hyo nilikaa nje stationary nikitafakari juu ya maisha yangu baada ya kujua matokeo ni mabovu na ndy nikapata jibu ya kuwa ni bora nirudie paper kuliko kufanya chochote nikamuomba na mungu pia anisaidie kwa kipindi kile.nikarudia paper nikapita nikaenda form six nikapita nikaenda chuo nikamaliza sasa hapa ndy kuna story mpya.

MAISHA BAADA YA CHUO
Nimemaliza chuo mwaka 2015 chuo cha usimamizi wa fedha(IFM) kozi ya banking nd finace ngazi ya degree.kutokana na biashara nilikuwa napenda toka kitambo nikaaza kwnda zanzibar kuchukua simu za mtumba na kuja kuuza ni kweli nilianza kupata pesa lakin kipindi kile uchaguzi ulikaribia baada ya kwenda kama mara mbili ndy watu wakanza kusema ooooh kipindi hk sio kizuri kusafi unaweza onekana unaend kupiga kura ndy nikasitisha kununua simu nikaenda vijijini kununua kuku nije niuze christmass na mwaka mpya kwa bahati mbaya pesa niliyotumi kwenye kuku mpk kusafisha kuja kukodi bada soko la tandika kuanza kurudi pesa haikurudi kama ilivyokuwa ndy nikaona bora niongezee mtaji nikarangue korosho mtwara na kuanza kukuza gurioni kweli nilifanya hvyo na nikapaa pesa kidogo japo mtaji haukuwa mkubwa lakini faida ilionekana mpk baadae koosho zilivuokuja kuzingua ndy nikasitisha nikasema acha ninde zangu jeshi.

Nikatafuta nafasi kwenye wilaya nikakosa nikakutaa na rafiki yangu akaniambia ya kuwa kuna rafik yake anamjomba wake ni mkubwa jeshini so anaweza tusaidia kweli tukaonana nae jamaa anaonekana yupo vzr gari kali nn kumbe tapeli na amemlagai kijana mpk amuone kama mjomba wake kwa kuwa wote wanatokea sehemu moja mwisho wa siku tukaishia kuzurumiwa sh 1000,000 mpk leo kesi ipo polisi kigamboni baina ya yule kijana aliyesema ni mjomba wake na mjomb mwenyewe maana alimtumia kijana kuleta watu wengi kwa kudai kuna form zinauzwa za kwenda jeshini.baada ya jeshi kugoma ndy nikakutana na FOREX hapo ndipo nilipoanza maisha ya changamoto mpk hii leo kiasi kwamba naomba ushauri ndugu zangu maana naisi kulemewa peke yangu.nimeanza forex mwaka 2017 nikajifunza mambo mengi kuhusu hii biashara baada ya kuona nimeilewa nikaweka pesa nianze kufanya kazi nakumbuka pesa ya kwanza ilikuwa 500$ ambayo nilichukua toka kwa sister wngu nikimwambia nitampa kabla ya week kuisha ile pesa ikaenda likawa janga pale nyumbani kiasi kwamba nikatoka home nikaenda kuishi kwa mwanangu dom nikakaa uko baadae uwezo wangu ukaonekana kuongezeka na jamaa m1 akanitafuta na kuniuliza maswali kuhusu hii business jpo na yeye alikuwa trader sema alipenda uwezo wangu.

Basi tukawa tunawasiliana sana huku nikimsaidia biashara na alikuwa akipata faida anaweza nirushia laki maana mimi hpo nilikuwa sina kitu bhc maisha yakaenda nakumbuka siku moja kuna dada m1 akanicheki via teregram mambo vipi?nikawambia poa akasema nimeona trading skills zako unaonekana uko poa?nikamwambia kidogo tu akasema upo vzr.....

Sasa kuna jambo nataka kukwambia kuna mtu nimempa acc yangu lakini kapata hasara sana kiasi kwamba inaweza ungua muda wowote alafu pesa yenyewe nilikopa sehemu sasa nimechangangikiwa sijui nifanyeje.nikamuuliza ww uko wapi?akanijibu dar nikamwambia mm pia home dar ila kwa sasa nipo dom so unataka tufannye nini? Akaniambia kama unaweza nisadia kuifanyia biashara hii acc maana pesa hii ni ya mkopo.....

Ndugu zangu ngoja nifupishe kidogo maana mimi sio mtaalamu sana wa kuandika kiufupi yule dada nikamkutanisha na yule rafiki yngu ambaye tulikuwa tunashirikiana kweny biashara kwa kuwa wote walikuwa wapo dar wakayajeng then yule dada akatuletea na marafiki zake wakaweka pesa kwa mara ya kwanza tulipata faida kiasi kwamba yule dada akarudisha rejesho na kufurahi sana.na hyu dada wa pili akamwambia na mume wake ya kuwa kuna vijana wanapiga kazi jamaa anapiga kazi mbele na yeye anaweka pesa yke kwa ufupi jamaa na mke wake wamepoteza zaidi ya mil 70 kwenye mikono yangu na rafiki yngu,wakaniambia mr tunashukuru tumefanya kazi pamoja kwa muda wote lakini haikuwa bahati acha sisi tujaribu issue nyengine,hapo kati kati walitokea inverstors wa kuweka $5000 nazo zimepotea si chini ya acc 4.

Sasa stress ambazo zinatokea baada ya pesa za watu kupotea ni za hataree sana vikao vya kuwaeleza pesa imepotea vinakuaga vigumu kiasi kwamba utamani siku hyo iwepo.baada ya inverstors kukata mguu tukajadili mimi na rafiki yangu kwmba tunapata wapi mtaji wa kupiga business, mwanangu(rafiki)akaniambia achukue gari yke tuweke bondi tuchukue sh 5mil nikamwambi poa sema akaenda home akasema wife wake kakataa so tuanye nn? Ndy akaniambia kuwa yy anmdogo wake anagari angoja akachukua tuweke bondi kwli tulichulia pesa ile gari kumbe ile gari sio ya yule dogo baada tu ya kuchukua mwenyewe akataka gari yake sekeseke likawa kubwa kiasi kwamba tukachukua gari nyengine tukapeleka kule kwenye mkopo na kumrudishia ile gari yke kwenye mkopo ni kw washkji zetu sio company so ile gari ya pili baada ya week wakaikataa na kusema ni mbovu sio kama ile ya kwnza ni IST.ngoja nifupishe kwa kifupi hii gari ya pili nayo tukaichukuili mkopo so jumla tukawa tunadaiwa sh 12mil kwa maana y mil 5 kila sehemu plus riba n gari moja hapo ndy maisha yakawa ya utata tukawa tunadaiwa kila sehemu kwa bahati nzuri sehemu moja tukalipa tena mpk riba ikabaki moja pamoja na gari mwenye gari akaenda polisi tukakatwa kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu tukawekwa ndani.

Huwezi amini nilipofika ndani yaani kituoni sikuwa na hofu yoyote wala kujilaumu kwa kuwa sikuwahi kutafut pesa kupleka bar au kwa wanawake yaan mimi naangika ili ndugu zangu waishi vizui maana kwa sasa mimi ndy tumaini lao mara nyingi nimekuwa mtu wa kuwapa san moyo ya kuwa mungu yupo na atatupigania na nilikuwa nikipata pesa lazima nimpe mother pamoja na masister maana furaha yao naiona kwenye moyo wangu.tunamshukuru mungu hawa nao tumewalipa bado 1mil...

Kitu ambacho kinanipa shida kwa sasa ni bi mkubwa na watu wote wa hapa nyumbni kutoamini kitu ambacho nakifanya na kuwa na hofu kubwa juu ya biashara ambayo nafanya maana waaona ni kama inanitesa alafu wanakuwa kwny hofu kubwa kila wakati wanaona ni kam majanga yatanikuta kwahyo mother kawa mtu wa kunichunguza kila wakati kujua nipo kwenye hali gani maaa ni kama anajua sasa kila kitu kinachoendelea kw kuniangalia usoni yaan akiniona sina raha tu anajua mmbo sio mazuri hata nikijaribu kuficha yeye anajua.

Ameshanishauri sana kuacha hii biashara lakini mimi naona kama kuna mpenyo vile wa kutokea na kitu ambacho kinanifanya nisitoke home najiona kama sijaweza riiha fadhira yoyote kwa mother,kuna kipindi nilitka kuondoka hata inchi za mbali lakini niliona nawezaje kumuacha mother.

Sasa juzi hpo nikapata tena pesa kutoka kwa mtu h 5mil nikaja nazo home hakika wote tulifurahi hapa nyumbani kwa kusema safari hii tumetoka yaani nitaenda nayo kwa umakini mkubwa lakini sivyo ilivyokuw kwa sababu baada tu ya siku tatu ile pesa ikapote yote n nilishatengeneza faida ya sh 1mil sasa msaada ambao nataka kutoka kwenu wana jamvi jinsi ya kuwaeleza watu walionizunguka ya kuwa na hii pesa imepotea ndy nashindwa maana ilikuwa ni kama pesa ya mwisho.

Namwambiaje aliyenipa pesa ile maana inaitajika rejesho lakini pia nini hatima ya mambo haya maana akili yangu imeik mwisho kiasi kwmba baada ya hasara hii kutoke nilishindwa cha kufanya mpk nikakimbia home kwa siku mbili maana sikutaka mtu yeyote hajue kama imekuwa hvyo.nilikuwa mchumba wangu kakimbia baada ya kuona sitimizi lengo yangu,rafiki zangu wamesong sana mbele lakini mimi bado nipo pale pale........

Please sisters and brothers naomba ushauri wenu juu ya mambo haya maana mwenyewe imefika mahali nimeanza kukata tamaa japo haikuwa slogani yangu.
Shida yako kubwa unafanya forex kama chakula, change habit zako ili upunguze risk plus tafuta issue nyingine ya kufanya forex iwe namba mbili ikiwezekana tatu, nenda ata kalime afu forex ufanye ukiwa na shughuli nyingine maalumu. Utanishukuru badae
 
Back
Top Bottom