Naomba ushauri wa vyakula anavyoweza kula mama aliyejifungua.

fadtanji

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
767
999
Namshukuru Mwenyezi Mungu mke wangu amejifungua salama baada ya miezi kumi ya ujauzito. Wakuu naomba kufahamu vyakula gani anaweza kula mama aliyejifungua ili aweze kurecover haraka?
 
Jitahidi ale balanced diet tu, yaani mlo kamili ambao utakua na makundi yote ya vyakula. Ila moja ya vyakula vinavyohitajika kwa wingi ni

1)PROTEIN. apate protein za kutosha ili kusaidia tissue renewal na kuzalisha maziwa ya mtoto wake .(Nyama, maharage, karanga, samaki, maziwa, mayai)

2)IRON + VITAMINS. Vyakula vya madini ya chuma(iron) na vitamins kwa ajili ya kupambana na anaemia maana mama anaweza kua amepoteza damu nyingi kipindi cha kujifungua. (Maini,dagaa,matunda, mboga mboga za majani kama matembele, mchicha n.k )

3) Anywe maji mengi sana na apate mda wa kufanya mazoezi hata ya kutembea + apate muda wa kupumzika (kulala).
 
Back
Top Bottom