Naomba ushauri wa ujenzi kwenye eneo lenye asili ya udongo wa mfinyanzi

mojamo

Member
Jan 9, 2019
68
114
Wakubwa poleni na mjukumu na wezangu habarini za mihangaiko.

Kama mada inavyojieleza, nina kiwanja kipo eneo zuri tambarare kiasi hali twamishi maji yani kuna kamwinuko.

Asili ya udongo ni mfinyanzi, ninawaomba wajuzi wa ujenzi wanisaidie katika ujenzi nizingatie nini zaidi ili kuepusha nyufa kwenye nyumba kama mjuavyo huu udongo kipindi cha jua hupasuka.

Pia naomba wazo la kutumia mawe au kutotumia kwenye msingi nilipata mawazo ya watu wanasema kwenye huo udongo ni vizuri kutotumia mawe kwenye msingi Bali tofali za kulaza cozi kama nne chini.
 
Ukichimba msingi jaza mchanga walau kina/kimo cha futi moja kabla ya kuanza zege, tofali au mawe hii itasaidia madhara ya kubadilika tabia kwa udongo wa mfinyanzi ukiloa au kukauka yasifikie msingi kiurahisi
 
Rafiki yangu aliuziwa kiwanja, hiyo sehemu ilikua bonde la mpunga zamani. Lakini wakati huo mji umepanuka na barabara kuu inapita.

Wakati anachimba msingi mafundi walipata samaki pelege. Aliweka zege kama futi moja, baada ya miaka miwili ya kuhamia nyumba mpya mvua ikinyesha kuta zinajaa maji na kuweka ukungu.
 
Mkuu hakikisha baada ya kuchimba msingi unaweka mchanga walau futi moja kabla ya zege na backfill iwe ya mchanga
 
Thanks mkuu nadhani ni wazo nililopewa na mtu wa kawaida sana, unajua lazima ulize huku JF coz ukibase sana kwa fundi unakuta yeye ndio dalali wa material Fulani hivyo analazimisha ili auze
Ukichimba msingi jaza mchanga walau kina/kimo cha futi moja kabla ya kuanza zege, tofari au mawe hii itasaidia madhara ya kubadilika tabia kwa udongo wa mfinyanzi ukiloa au kukauka yasifikie msingi kiurahisi
 
Hivi wire mesh ni material sahihi kuitumia katika kumwaga jamvi la msingi?.
 
chota udongo wote kama mita moja na nusu katupe, kisha jaza udongo mpya wa vifusi safi mimina zege kali sana lanusu mita msingi upande juu wa matofali mazito nchi sita
 
Niba tatizo kama kako.. Weka mchanga, nikaweka zege pia tofali za kukaza.. Ufa ukajitokeza...
Kwa uzoefu wangu nimeona kinachopasua ukuta ni ule mfinyanzi unaorudishwa kam kifusi ndani ya msingi.
Unavosinyaa na kunyauka wkt wa jua kali, ndivo unavoleta ufa kwenye tofali.

Unaweza kutumia mchanga kama kifusi hasa kwa kuta za nje.
 
Wakuu ningeomba kufahamu aina ya udongo unaopatikana morogoro mjin hasa eneo linaloitwa kitungwa
 
Kwa uzoefu wangu nimeona kinachopasua ukuta ni ule mfinyanzi unaorudishwa kam kifusi ndani ya msingi.
Unavosinyaa na kunyauka wkt wa jua kali, ndivo unavoleta ufa kwenye tofali.

Unaweza kutumia mchanga kama kifusi hasa kwa kuta za nje.
Huu ndo ushauri wa kitaalamu. Nilikuta engineer mmoja anafanya hii kitu nikamuuliza akatoa maelezo kama yako

Vitu vingine vilivyotajwa juu na wachangiaji wengine pia vizingatiwe pia
 
Back
Top Bottom