Naomba ushauri wa namna ya kutatua tatizo la kushindwa kujiamini

nover

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
235
174
Habari wana JF, mimi ni kijana umri miaka 30. nina familia mtoto mmoja na nimeajiriwa kazi nzuri tu. Kwa haraka haraka naweza kusema maisha yangu ni mazuri kwa hilo nashukuru Mungu. Kilichonifanya kuandika uzi huu ni tatizo langu ambalo nimekua nalo muda mrefu naweza kusema toka nimezaliwa, tatizo la kushindwa kujiamini (wazungu wanasema social anxiety).

Labada nielezee historia yangu kwa kifupi inaweza kusaidia. Mimi nilizaliwa kwenye familia ya kawaida tu na nimelelewa tu vizuri. ilitokea nlikua namuogopa sana mzee wangu sijui kwanini. nilikua nashindwa kuongea nae freely na nikisikia amerudi kutoka kazini nilikua naingia hofu kwelikweli. Shuleni pia pamoja kua nilikua mwanafunzi bora, nilikua siwezi kusimama kuuliza maswali au kuchangia kitu chochote darasani kutokana na hofu. kipindi cha presentations nlikua natetemeka sana na kutoka jasho hali ambayo ilinifanya kuchekwa na kutaniwa na wenzangu.

Mpaka leo nimeajiriwa nina miaka sita kazini bado hali hii ipo. Naona aibu sana kuongea na watu wapya, siwezi kuangalia mtu machoni, ikitokea mabishano mimi hua ni mtu tu wakukubali hata kama naona si sawa, kwenye social events naogopa kuudhuria nahisi naweza itwa mbele labda kutoa speech kidogo.

Kazini nadhani walishaona mapungufu yangu haya. Mara nyingi wakihitaji mawazo kutoka kwangu hua hawaniulizi tukiwa wengi manake wanajua ntaogopa kuongea, badala yake hua wananiambia niwapatie riport iliyoandikwa nikishauri nini cha kufanyika.

Japokua naonekana kama mfanyakazi bora na anayejituma, nakiri kua hali hii imeniruidisha sana nyuma katika carrier growth. uwezo wangu mdogo wa kushawishi mambo kufanyika, kuongoza wenzangu na kujiamini umesababisha viongozi wangu kutonipatia majukumu makubwa zaidi japokua wanafahamu wazi kua nayaweza ila ndo ivo yanaitaji social skills ya hali ya juu.

Mimi ni mzuri sana nikipewa kalamu na karatasi, lakini likija swala la kuongea siwezi kabisa. kuna baadhi ya wenzangu ambao nilikua nao nafasi moja, walizitumia kazi zangu kwa sababu mimi sikuweza kuzipresent kwenye vikao vikubwa na ziliwawezesha wao kupandishwa vyeo na mishahara.

Hili kwakweli liliniumiza sana na sasa nimeona nitoke out of my comfort zone na kujaribu kukabiliana na tatizo hili. kwa utafiti niliofanya mtandaoni wanasema suala hili linatibika kwa dawa pamoja na ushauri na saha. Kwa hapa Tanzania kwa sijajua kama kuna taasisi ambazo zinahusika na masuala haya. Kama ipo tafadhali naomba lkufahamishwa. Kama kuna mtu ana ushauri wowote naupokea pia. Asante
 
Hilo ni tatizo la kiroho zaidi, Shetani au adui anautumia huo mwanya wa kutojiamini kukurudisha nyuma.nafahamu jinsi ilivyo vigumu kuishi katika hali hiyo, Kumbuka kila jambo linalokupata linapunguza ujasiri wako, hivyo kuwa makini kuanzia sasa, fuatilia kwa karibu aina ya lifestyle inayochangia kwa kiasi kupoteza kujiamini.
 
Pole. Nadhani ni malezi ktk familia na shuleni. Ulikulia ktk mazingira ambayo watoto hawakutakiwa kuongea. Ni wasikilizaji tu. Vingenevyo, wanachapwa viboko. Na shuleni nako hivyo hivyo. Ni vigumu sana kubadilika ukiwa mtu mzima. Na mimi pia nimepitia mazingira hayo.

Hata ukipewa uongozi, hautakuwa kiongozi mzuri kazini. Kubali nafasi uliyo nayo. Ukipewa uongozi utachafua hali ya hewa. Na utateseka sana ndani ya moyo wako kwa sababu itabidi u-pretend sana. Halafu ni "career growth", siyo "carrier growth".
Japokua naonekana kama mfanyakazi bora na anayejituma, nakiri kua hali hii imeniruidisha sana nyuma katika carrier growth. uwezo wangu mdogo wa kushawishi mambo kufanyika, kuongoza wenzangu na kujiamini umesababisha viongozi wangu kutonipatia majukumu makubwa zaidi japokua wanafahamu wazi kua nayaweza ila ndo ivo yanaitaji social skills ya hali ya juu.
 
Tafuta mtu unayeona ni ngumu kuongea nae,, mfate mpige story for a course of month siku ya kwanza anza na conversation ya dk 5 tu,, siku ya pili ongeza zifike 10,, fanya hvo for 2 weeks.

Then ukianza kuona unaweza handle conversation na huyo mtu vizuri ongeza mtu mwingine wawe wawili mpige story anza for 10 minutes and ongeza as days goes by. Ukiona unaweza handle hao watu wawili then ongeza mtu na anza na muda mdogo

Social anxiety inaweza kuwa solved but it takes time. Muda mwingine ulichokiandika kwenye report nenda kakisome kwa watu unaowaandikia.

Unaweza usianze na kusoma report yote but fanya summary ya muda mfupi na utoe report. Siku nyingine ongeza muda wa presentation jinsi muda uendavyo basi tatizo litakuwa linapungua kwa kiasi chake..

Ukiona ni ngumu basi tafuta social group
 
Asante sana ndugu yangu... hili ntalifanyia kazi. Naomba unifafanulie kuhusiana na social grp, hii inakuaje?

Pole sana kiongozi nami nilikuwa hivyo mwanzo nilikuwa mtu wa aibu sana, siwezi kuchanganyika na watu na sio muongeaji pia, nilikuwa mtu wa kukaa ndani tu siku nzima naweza nisitoke nje ila sijui nini kilinibadilisha mpaka sasa na hang na yeyote aliye mbele yangu, FULL OF CONFIDENCE.
 
Pole sana kiongozi nami nilikuwa hivyo mwanzo nilikuwa mtu wa aibu sana, siwezi kuchanganyika na watu na sio muongeaji pia, nilikuwa mtu wa kukaa ndani tu siku nzima naweza nisitoke nje ila sijui nini kilinibadilisha mpaka sasa na hang na yeyote aliye mbele yangu, FULL OF CONFIDENCE.
Hongera sana aise. Mshukuru Mungu kwa hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom