Taratibu za kupata cheti cha kuzaliwa kutoka RITA Tanzania

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Taratibu za kupata cheti cha kuzaliwa:
RITA Tanzania

Kwa mujibu wa sheria unaweza kupata cheti katika Wilaya uliyozaliwa au katika ofisi za Msajili Mkuu, Makao Makuu ya RITA katika jengo jipya la wakala la Rita Tower lililopo Mtaa wa Makunganya maeneo ya posta mpya mkabala na Club Bilcanas, Dar es Salaam.

Tafadhali fika katika ofisi zetu, utatakiwa
  1. kujaza fomu BD 15
  2. halafu utaambatisha kiambatishi kimoja kati ya hivi: kadi ya kliniki, cheti cha kupigia kura (2005), pasi ya kusafiria, cheti cha kumaliza elimu ya msingi au secondary (leaving certificate), cheti cha ubatizo. Kimoja wapo kati ya vilivyo tajwa hapo utakiambatanisha kwenye fomu yako utakayoijaza
  3. halafu msajili atapitia maombi yako
  4. yakiwa sawa utaandikishwa.
Je kama mtu hana Kimoja wapo kati ya vilivyo tajwa je inatakiwa afanye nini?
Nenda katika wilaya uliyozaliwa, chukua barua kutoka kwa afisa mtendaji kata wa sehemu uliyozaliwa ambayo ukiiwakilisha kwa msajili wa wilaya hiyo na msajili kujiridhisha utasajiliwa na kupata cheti. Karibu sana

Je, kama cheti cha kuzaliwa kimepotea, kupata cheti kingine natakiwa nifanyeje na ni shiling ngapi natakiwa kuwa nayo?
Tafadhali fika katika ofisi ya RITA ukiwa na taarifa zako sahihi (viambatishi vinavyoonyesha majina yako na tarehe ya kuzaliwa kama inavyosomeka kwenye cheti kilichopotea mfano nakala ya cheti hicho - Toa maelezo sahihi yafuatayo: Jina la mtoto, Jina la baba, Jina la mama, Mahali pa kuzaliwa, Tarehe sahihi ya kuzaliwa na usajili, Tarehe kilipotolewa iwapo kuna uwezekano) kisha tutaangalia kwenye kumbukumbu zetu na rekodi yako ikipatikana utalipa Tshs. 3,500 na kupatiwa cheti kingine.

Ghalama zikoje?
Tafadhali tuambie una umri gani na ulizaliwa wilaya gani, na kama una tangazo la kizazi ili tuweze kukutajia gharama ya cheti.

Ofisi ziko wapi?
Tuna ofisi kila wilaya ila makao makuu ya RITA yapo katika jengo jipya la wakala la Rita Tower lililopo Mtaa wa Makunganya maeneo ya posta mpya mkabala na Club Bilcanas, Dar es Salaam.
Ofisi ya RITA Kinondoni ipo jirani na Magomeni traffic light ukiwa unaenda Morocco. Utaona jengo limeandikwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni.

Masaa ya kazi:
siku za kazi ni kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 9.00 jioni.

Kwa maswali zaidi
Contacts ------>>> bonyeza hapa


Chanzo: RITA
 
Good. Taasisi zote za umma mnatakiwa kutoa taarifa kama hizi kila wakati
 
mkuuu kama una bango ( kile kicheti anapozaliwa mtoto ) nenda nacho tawi la RITA la wilaya husika ambapo ipo hospitali..watakutengenezea in a week
 
Kama nilidangaya mahali nilipozaliwa na umri pia kwa sababu tu ya kupata cheti kwa haraka na kuepusha usumbufu mfano badala ya kuandika Tanga nilipozaliwa nikadanganya na kuandika Mbeya nilikokulia! je, naweza kurekebisha hizo taarifa na kwa utaratibu upi?
 
Tunashukuru kwa taarifa njema mkuu

naomba nikuulize...

Nyumbani kwetu kuna wadogo zangu wapata 12 hivi. ( mzee ameoa wake 4)...sasa swali langu ni kuwa ...kwa kuwa hao madogo wote hawana cheti cha kliniki/hospitalini waliko zaliwa.....Je nnaruhusiwa kuwachukulia vyeti vyao vya kuzaliwa kwa wakati mmoja (cku moja)?..

na Gharama ya kila mmoja ni sh.ngapi
 
Aksante Saana Mtoa Taarifa!! Sasa Hicho Kitambulisho Cha Kupigia Kura Kilichotolewa 2005, Wengi Wetu Tuliojiandikisha 2015, Walivichukua Hivyo Vya Zamani!!

Kama Ikiwa Sote Tuliojiandikisha 2015 Na Kupewa Vitambulisho Hivi Vya Kidigital, Inasemekana Na Tuliambiwa Ni Watanzania!! Sasa Kwanini Vitambulisho Hivyo Tena Havitambuliki Na Taasisi Hii!!!?? Je, Vile Vitambulisho Vya NIDA Navyo Havitambuliki!!!!???
 
WanaJF naombeni mnipe utaratibu wa kubadilisha cheti cha kuzaliwa, kuna makosa mengi katika cheti, jina limekosewa wameandika Erija badala ya Erijo.
 
Aksante Saana Mtoa Taarifa!! Sasa Hicho Kitambulisho Cha Kupigia Kura Kilichotolewa 2005, Wengi Wetu Tuliojiandikisha 2015, Walivichukua Hivyo Vya Zamani!! Kama Ikiwa Sote Tuliojiandikisha 2015 Na Kupewa Vitambulisho Hivi Vya Kidigital, Inasemekana Na Tuliambiwa Ni Watanzania!! Sasa Kwanini Vitambulisho Hivyo Tena Havitambuliki Na Taasisi Hii!!!?? Je, Vile Vitambulisho Vya NIDA Navyo Havitambuliki!!!!???
Ana maana vitambulisho vyote vya kupigia kura vinatambulika toka 2005
 
WanaJF naombeni mnipe utaratibu wa kubadilisha cheti cha kuzaliwa, kuna makosa mengi katika cheti, jina limekosewa wameandika Erija badala ya Erijo.
Soma uzi juu utapata jibu------
Kama nilidangaya mahali nilipozaliwa na umri pia kwa sababu tu ya kupata cheti kwa haraka na kuepusha usumbufu mfano badala ya kuandika Tanga nilipozaliwa nikadanganya na kuandika Mbeya nilikokulia! je, naweza kurekebisha hizo taarifa na kwa utaratibu upi?
Tunashukuru kwa taarifa njema mkuu...
---------
naomba nikuulize.....
Nyumbani kwetu kuna wadogo zangu wapata 12 hivi. ( mzee ameoa wake 4)...sasa swali langu ni kuwa ...kwa kuwa hao madogo wote hawana cheti cha kliniki/hospitalini waliko zaliwa.....Je nnaruhusiwa kuwachukulia vyeti vyao vya kuzaliwa kwa wakati mmoja (cku moja)?..
------
na Gharama ya kila mmoja ni sh.ngapi
Naweza kupata cheti kwa mtoto aliyezaliwa Zanzibar?
Piga simu hii upate jibu siku za kazi: +255 (22) 2924181
 
Mimi nilienda HQ muhimbili sasa nilitaka nipewe cheti kingine sabab cha mwanzo kilipotea nikajaza na form na kulipia research fee na kupewa risiti .sasa baada ya hapo nikaambiwa niende nikachukue cheti baada ya wiki 2 posta ilikua 2015 November sasa ilipofika ile siku nilipata dharura nikasafiri nimerudi dar Feb 20 .Swali je nikienda na hii risiti nitapewa cheti changu au lah maana naona imepita mda au kunaaja yakujaza form tena ahsante.
 
Mkuu umeongelea cheti cha kuzaliwa tu vipi utaratibu wa cheti cha KIFO.
 
Hongereni kwa huduma hii
 

Attachments

  • Screenshot_2016-03-23-17-18-23.png
    Screenshot_2016-03-23-17-18-23.png
    16.1 KB · Views: 700
Back
Top Bottom