Naomba ushauri wa namna ya kuihudumia Nissan March

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Habari zenu wana jukwaa? Mimi kwa sasa ni Mkaazi wa Zanzibar, niliporudi nyumbani nilivitiwa na Muonekano wa Nissan March nikaamua niinunue, ila Marafiki zangu wa karibu wamekua wananilaumu sana kwa nini nimenunua Nissan March na nisinunue gari za Toyota kama IST?

Hivo wana jukwaa nawaombeni msaada wenu jinsi gani naweza kukihudumikia hiki kigari, na pia nawaombeni mnifahamishe uzuri wake na udhaifu wake.

Naamini nitapata mashirikiano kutoka kwenu.

1606982791792.png

Nissan March
 
wanalalamika kwa sababu spea nyingi za nissan ni ghali,

Pili ukitaka kuuza nissan haiuziki haraka kama toyota..

Vinginevyo ni gari nzuri.
Shukran sana kama tatizo spea ni ghali ilo sio tatizo kwangu, nilitaka tu nijue madhaifu makubwa ya hizi gari
 
Jee zina matatizo gani hizi gari? Na kwanini wenzangu wanalalamika??
Ni gari nzuri sana.Hazina matatizo yoyote yale ila wenye matatizo ni binadamu/wewe.Wenye matatizo ni binadamu/wewe kwa sababu unapaswa:

1.Kuzingatia sana services yake kwa wakati.

2.Kuzingatia sana kuweka recommended oil ambayo ni original.

3.Kuzingatia sana kuweka ATF yake kama ilivyo recommended na iwe original.

4.Kubadili oil kwa wakati pamoja na ATF yake.

5.Kupeleka gari yako kwa mafundi walioenda shule na wenye vyeti kama vile waliosoma NIT na DIT na siyo kupeleka gari kwa mafundi wagonga nyundo,makanjanja wa mtaani pamoja na vishoka.

6.Kusoma manual yote ya gari,kuielewa na kuizingatia.

7.Kununua na kuweka vifaa original pekee wakati wa kufanya services na siyo kuweka vifaa fake.

Ukitii yote hayo gari haitakuwa na shida yoyote ila ukizingua unaipoteza fasta.
 
Back
Top Bottom