Naomba ushauri wa namna ya kuanzisha mgahawa

nusuhela

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Messages
4,376
Points
2,000
nusuhela

nusuhela

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2014
4,376 2,000
Habari zenu wandugu.
Samahani, leo nimeamua kuja kwenu baada ya muda mrefu kufanya mpango wa kuanzisha biashara.
Hivi karibuni nimefanikiwa kupata mtaji kiasi cha sh milioni tano (5,000,000) za kitanzania.
Hamu yangu kubwa ni kumiliki mgahawa.
Maeneo niliyopo ni dar es salaam.

Kabla sijaanza hii biashara ningependa kujua machache kutoka kwa wazoefu wa hii biashara.

Kati ya mambo ambayo ningependa kuyajua ni
1. Je, kwa mtaji huo nitaweza kuendesha biashara hiyo na kupata faida?

2. Ni changamoto zipi nitakutana nazo pindi tu nitakapoanza hii biashara.

3. Ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kuendesha hii biashara.

4. Ni maeneo gani kwa mtaji huu yatafaa kuendeshea hii biashara nikapata faida ya kuridhisha.

Ahsanteni sana
 
jisanja

jisanja

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Messages
1,117
Points
2,000
jisanja

jisanja

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2013
1,117 2,000
Kila la kheri ngoja wajuvi waje
 
Dharra

Dharra

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2017
Messages
1,412
Points
2,000
Dharra

Dharra

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2017
1,412 2,000
Habari zenu wandugu.
Samahani, leo nimeamua kuja kwenu baada ya muda mrefu kufanya mpango wa kuanzisha biashara.
Hivi karibuni nimefanikiwa kupata mtaji kiasi cha sh milioni tano (5,000,000) za kitanzania.
Hamu yangu kubwa ni kumiliki mgahawa.
Maeneo niliyopo ni dar es salaam.

Kabla sijaanza hii biashara ningependa kujua machache kutoka kwa wazoefu wa hii biashara.

Kati ya mambo ambayo ningependa kuyajua ni
1. Je, kwa mtaji huo nitaweza kuendesha biashara hiyo na kupata faida?

Jibu ni ndio kwa mtaji wa milioni tano unaweza kuendesha biashara na kupata faida

2. Ni changamoto zipi nitakutana nazo pindi tu nitakapoanza hii biashara.

Kwanza uwe tayari ku run biashara yako kwa siku kadhaa bila ya wateja, pili kama huna certificate ya FDA tegemea kusumbuliwa sana, tatu tegemea kukosa hiki na kile wakati wa kuanza (hii unaweza kununua vifaa kidogo kidogo kadri muda unavyoenda), tegemea malalamiko kwa hao wateja wachache watakao tumia huduma.

3. Ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kuendesha hii biashara.
Zingatia, sana sana usafi, usafi wamazingira na watoa huduma hii ni muhimu sana, huwezi kuendesha biashara ya mgahawa bila ya kuwa na mpishi ambae ni muelewa na ako na uzoefu wa kutosha, tatizo watu wa aina hio wengi tayari wana ajira zao kwa hio ni kitu cha kumtoa sehemu alipo na kumleta kwako itakugharimu kidogo, tahadhari hapa usichukue wapishi wa vichochoroni ama wale wanaopika pilau kwenye sherehe mitaani itakugharimu sana biashara nzuri kwa chakula ni ile inayo range kati na kati

4. Ni maeneo gani kwa mtaji huu yatafaa kuendeshea hii biashara nikapata faida ya kuridhisha.

Popote pale unaweza kuanzisha biashara ya mgahawa na ikaenda vizuri kutegemea na kundi gani unalilenga. Maeneo yenye movement kubwa ya watu kama mbangala, tandika, temeke mwisho na mengine kama hayo unaweza kuanzisha hio kitu. Zingatio, jikurupushe sokoni, feri na maeneo ya minada kwa kupata vitu bei nafuu alfajiri mapema
Ahsanteni sana
 
E

essy sensei

Senior Member
Joined
Feb 11, 2017
Messages
134
Points
250
E

essy sensei

Senior Member
Joined Feb 11, 2017
134 250
Tatizo sio mtaji kuwa wa kutosha au kutotosha,
Kitu muhimu ni taarifa muhimu/sahihi kwa unachotaka kukifanya, na taarifa utazipata kwa kuzifanyia utafiti wa hicho unachotaka kufanya,
Nakushauri
1)jua aina ya biashara unayotaka kufanya na kwa ubora gani,
2) jua walengwa wako kina nani,
Na wanapatikana maeneo gani, na hapa ndio utajua ukafungue wapi biashara yako.
3) wafuate walengwa wako japo kwa uchache ujue wanahitaji nini
4) Pita kwenye biashara za wengine jua wanafanyaje
5) Pitia social media za biashara za wenzio pitia comments itakusaidia kujua pia nini kinalalamikiwa au kusifiwa nawe ukavifanyie kazi katika maandalizi yako ya kwanza hiyo biashara.
Nakutakia heri.
 
Ahsante sana
 
milionea wa kesho

milionea wa kesho

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Messages
280
Points
500
milionea wa kesho

milionea wa kesho

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2015
280 500
Tafuta location ambayo utaweza kuuza chakula kwa bei ya juu mfano wali nyama kuanzia 3000/=

Chini ya hapo usifanye biashara hii kabisa.
 
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Messages
2,132
Points
2,000
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2018
2,132 2,000
Mtaji unatosha kabisa, issue hapo location....
Kama utapata sehemu nzuri ambayo chakula unaweza kuuza Tsh 2000 , ongeza na vinywaji baridi, pia weka na kijana wa chips maana wadada wengi ndo chakula chao
 
nusuhela

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Messages
4,376
Points
2,000
nusuhela

nusuhela

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2014
4,376 2,000
Mtaji unatosha kabisa, issue hapo location....
Kama utapata sehemu nzuri ambayo chakula unaweza kuuza Tsh 2000 , ongeza na vinywaji baridi, pia weka na kijana wa chips maana wadada wengi ndo chakula chao
Nashukuru
 
adakiss23

adakiss23

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Messages
3,414
Points
2,000
adakiss23

adakiss23

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2011
3,414 2,000
Kwa ufahamu wangu kikubwa ni usimamizi. Kuanzia manunuzi ie ubora wa materials, bei nk mpaka mauzo cz chakula hakina hesabu kamili inategemea idadi ya sahani (kama ndo kipimo). Bila hivyo andika maumivu
 
Perimeter

Perimeter

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2015
Messages
2,521
Points
2,000
Perimeter

Perimeter

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2015
2,521 2,000
Biashara sio mtaji mkubwa..

Biashara ni kujua wanunuaji/wateja wako

Unaweza kua na huo mtaji lakini ukapigwa gepu na mama ntilie mwenye mtaji wa laki 1,MAMA ntilie akalaza kila siku faida ya 50k wewe ukalaza 20k ukijitahidi sana 30k

Muhimu ni Kujua wateja wako wanahitaji mtaji huo 5M?? Yawezekana wateja wako wanahitaji mtaji wa 1M tu..

Biashara ya CHAKULA/MGAHAWA ukitaka upige hela biashara yako iwe katika makundi haya mawili

1.Kawaida/chini: hapa ndio kuna kina mama ntilie na wauzaji wengine kibao wenye migahawa local na wateja wa kundi hili ndio wengi katika nchi yetu ya Tanzania.

2.Juu/kubwa:hapa kuna ma expert wanaoijua hii biashara so investment yao si ya kitoto toto na wateja wa kundi hili ni Madon wenye nchi yao wazeee wakufyatu hela..Mfano wa mgahawa wa kundi hili ni wa IRENE UWOYA "last minute"

Chagua kundi moja kati ya hayo mawili then FANYA BIASHARA.

Biashara ya mgahawa haina cha kuonja onja eti uweke mgahawa in a way LOCAL PEOPLE waingie na wale PRO LEVEL waingie HAMNAGA HIYO...lazima uchague aina ya wateja wako kama ni LOCAL au PRO then wape mamboz.

Ukisema uweke mgahawa haueleweki huu ni wa madon au raia wa kawaida aseee Utamaliza siku nzima umeuza sahani 1 ya chakula na soda mbili.

Mil.5 ni nyingi kwa mgahawa wa kawaida tena nyngi sanaaaaaaaa(hauihitaji hela nyingi ivyo)...ila Mil.5 ni ndogo sana kwa mgahawa wa kundi B so kabla hujaendelea SEMA unawalenga wateja gani ktk hiyo biashara.
 
Forum statistics

Threads 1,325,458
Members 509,127
Posts 32,193,069
Top