Naomba ushauri wa kisheria kuhusu watu waliovamia shamba langu

Shetemba

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
872
871
Kuna watu wamevamia shamba langu na kulima kwa nguvu wakidai mimi mwenye shamba sijalilima siku nyingi. Nifanyeje au niwaachie?
 
1. Wasaidie uwaache walime.
2. Tumia nguvu kuwazuia.
3. Kama huna nguvu tumia sheria.
 
fanya uwezavyo wapige pini wasilime maana hawakawii kujimilikisha kama utawaruhusu walime mara 2-3 ama

wakodishie bure ila kwa maandishi,hata wakitaka likatalia iwe rahisi kuwabana (kwa kuonesha mkataba wa kuwakodishia)

tofauti na hapo badae itakuwa ni mgogoro mkubwa
 
Tumia taratibu za kisheria kuwathibiti,
Ukishafanikisha, usiliache tena bila kulimwa,unaweza fanya jambo moja kati haya.
1)panda miti,
2)kodisha eneo lako kwa kilimo nk.
3)jenga nyumba ndogo umuweke mtu akae bure akuchungie eneo lako,
4) kisha weka alama za kudumu kwenye mipaka yako
 
Nimeshuhudia watu wakinyang'anywa mashamba yasiyoendelezwa, yanaitwa mashamba pori . Kiukweli it's unfair kukalia eneo hulitumii wakati kuna watu hawana pa kulima. Tafuta mtu mpe shamba alime bure ilimradi isionekane pori.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom