Naomba ushauri wa kisheria kuhusu hili suala la kutopewa mkataba na changamoto hizi za kazini

thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,459
1,428
Mimi naomba kufahamu juu ya hii case yangu nitaweza kusolve vipi, nilipata kazi kwenye kampuni fulani inaendeshwa na wahindi lakini ni zaidi ya miaka miwili sijapatiwa mkataba wa kudumu na hata malipo ninayoyapata hayaendani na viwango kisheria.

Nina bachelor degree lakini nalipwa chini ya laki 6, mshahara naweza nisiangalie sana lakini nakosa haki za msingi. Mfano likizo sipati, sipo kwenye mifuko ya kijamii hata Ikitokea nafukuzwa kazi sina cha kujitetea.

Lakini kabla ya hayo yote kutokea naomba nipate darasa nini nifanye ili miaka yangu miwili ya kuwatumikia hawa watu isipotee bure, na sio kwangu tu kuna wafanyakazi wenzangu pia wanatatizo kama hili.





don't waste your time on lecturing me, this is 2020
 
Ukitaka kuacha iyo kazi niambie ntakupa kiasi cha fedha ,mtoto wa dada mmoja naye apate sehemu ya kujipatia kipato.
 
Mkuu pole sana hata Mimi majanga hayohayo wakati nasoma wenzangu wengine waliishia form 4 wengine 6 walikimbilia ualimu na upolisi lkn leo hata mishahara wamenizidi na wale degree wenzangu ndio sigusi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa unafurahisha sana, kwamba hiyo signature yako ina maana gani sasa?. Endelea kufikiri unajua kumbe hujui, muhindi ana haki ya kula kichwa chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom