Natumaini nyote hamjambo!
Mie naitwa Kakuyu, naomba ushauri mahsusi kutoka kwa waliokwishafanya Kilimo cha Maembe na Minazi.
Nina shamba lipo Kisarawe maeneo ya Masaki (Mji Mpya) lenye ukubwa wa Hekari 25. Niko kwenye kigugumizi kuhusu nilime zao gani ili nipate faida maana najua hakuna zao ambalo halina changamoto ila yapo mazao ambayo hayana changamoto kubwa sana.
Kiukweli ninahitaji ushauri kutoka kwa mtu ambaye ameshalima na kupata uzoefu kuhusu Maembe na Minazi. Ninataka ushauri wa uhakika kuwa kama mazao hayo (maembe na nazi) nikilima nitapata faida na vipi kuhusu changamoto zake kutokana na uzoefu mlioupata. Ninafikiria kulima nazi za kienyeji 400 na za kisasa 200) na miembe ya kisasa walau 1000 ila sijajua kiuhalisia kama nimazao ambayo yataweza kuninyanyua au nitakuwa mkulima jina tu.
Nitashukuruni sana kwa ushauri nitakaoupata kutoka kwa wanajamvi wenzangu ili niweze kufanya uhamuzi maana mvua za masika ziko karibuni ila bado sijafanya maamuzi kamili hivyo ushauri wako utakuwa muhimu sana.
Ahsanteni sana kwa ushauri na MUNGU awabariki sana....!