Naomba Ushauri wa Kina Kuhusu Kilimo cha Maembe na Minazi

Kakuyu

New Member
Jan 22, 2017
3
2
Natumaini nyote hamjambo!

Mie naitwa Kakuyu, naomba ushauri mahsusi kutoka kwa waliokwishafanya Kilimo cha Maembe na Minazi.
Nina shamba lipo Kisarawe maeneo ya Masaki (Mji Mpya) lenye ukubwa wa Hekari 25. Niko kwenye kigugumizi kuhusu nilime zao gani ili nipate faida maana najua hakuna zao ambalo halina changamoto ila yapo mazao ambayo hayana changamoto kubwa sana.

Kiukweli ninahitaji ushauri kutoka kwa mtu ambaye ameshalima na kupata uzoefu kuhusu Maembe na Minazi. Ninataka ushauri wa uhakika kuwa kama mazao hayo (maembe na nazi) nikilima nitapata faida na vipi kuhusu changamoto zake kutokana na uzoefu mlioupata. Ninafikiria kulima nazi za kienyeji 400 na za kisasa 200) na miembe ya kisasa walau 1000 ila sijajua kiuhalisia kama nimazao ambayo yataweza kuninyanyua au nitakuwa mkulima jina tu.

Nitashukuruni sana kwa ushauri nitakaoupata kutoka kwa wanajamvi wenzangu ili niweze kufanya uhamuzi maana mvua za masika ziko karibuni ila bado sijafanya maamuzi kamili hivyo ushauri wako utakuwa muhimu sana.

Ahsanteni sana kwa ushauri na MUNGU awabariki sana....!
 
kama upo Dar nenda AMAGRO watakupa details za embe aina ya embe wapi utazipata na soko likoje. Mtafute Mzee Mkopi 0715 312036 ni wa msaada sana

Kuhusu nazi nenda ARI Mikocheni kama unaenda cocacola Mwenge, watafute wataalamu wa minazi watakupa aina ya minazi mizuri mbegu zinapatikana wapi na profit margin zake zikoje

acha uvivu ukitaka kufanya biashara ya kilimo fanya tafiti za kutosha maana ukikosea utajuta sana.
 
Thanks Kichakoro..! Nimempata mzee Mkopi na tumewasiliana vizuri.
 
Thanks Kichakoro..! Nimempata mzee Mkopi na tumewasiliana vizuri.[/QUOTE S)

Bado nahitaji ushauri wa mzoefu.

Pili naomba uzoefu kuhusu upatikanaji wa karatasi ya kuweka kwenye bwawa kwa ajili yakuvuniamajina kuhifadhi.
 
Tunaomba mrejesho kinacho endelea... Maeneo hayo ni mazuri kwa minazi...? nkitaka eneo uko naeza pata kwa sh ngapi boss.. unisaidie pia
 
Natumaini nyote hamjambo!

Mie naitwa Kakuyu, naomba ushauri mahsusi kutoka kwa waliokwishafanya Kilimo cha Maembe na Minazi.
Nina shamba lipo Kisarawe maeneo ya Masaki (Mji Mpya) lenye ukubwa wa Hekari 25. Niko kwenye kigugumizi kuhusu nilime zao gani ili nipate faida maana najua hakuna zao ambalo halina changamoto ila yapo mazao ambayo hayana changamoto kubwa sana.

Kiukweli ninahitaji ushauri kutoka kwa mtu ambaye ameshalima na kupata uzoefu kuhusu Maembe na Minazi. Ninataka ushauri wa uhakika kuwa kama mazao hayo (maembe na nazi) nikilima nitapata faida na vipi kuhusu changamoto zake kutokana na uzoefu mlioupata. Ninafikiria kulima nazi za kienyeji 400 na za kisasa 200) na miembe ya kisasa walau 1000 ila sijajua kiuhalisia kama nimazao ambayo yataweza kuninyanyua au nitakuwa mkulima jina tu.

Nitashukuruni sana kwa ushauri nitakaoupata kutoka kwa wanajamvi wenzangu ili niweze kufanya uhamuzi maana mvua za masika ziko karibuni ila bado sijafanya maamuzi kamili hivyo ushauri wako utakuwa muhimu sana.

Ahsanteni sana kwa ushauri na MUNGU awabariki sana....!
Ni miaka 2 sasa hebu leta mrejesho ndugu Kakuyu
 
kama upo Dar nenda AMAGRO watakupa details za embe aina ya embe wapi utazipata na soko likoje. Mtafute Mzee Mkopi 0715 312036 ni wa msaada sana

Kuhusu nazi nenda ARI Mikocheni kama unaenda cocacola Mwenge, watafute wataalamu wa minazi watakupa aina ya minazi mizuri mbegu zinapatikana wapi na profit margin zake zikoje

acha uvivu ukitaka kufanya biashara ya kilimo fanya tafiti za kutosha maana ukikosea utajuta sana.
Mkuu....nilete shukrani....I saw this nikafanyia kazi. Nimepanda miembe 500 since November last year.

Ubarikiwe sana.
 
Hata Mimi hiki kilimo huwa nakipenda sana kwa sababu huwa ni Cha kudumu.
Ngoja tuendelee kufuatilia mirejesho ya wadau humu.
 
Nimepanda Apple na Keit....250 each. Mwaka huu naongeza 250 Kent ifike 750 jumla.

Hizo ndiyo varieties ambazo AMAGRO inashauri members wake kupanda.
Mkuu wanakutafutia na soko?me nimepanda dodo.Mche wanauzaje?
 
Mwembe wangu bado mdogo sana na mwembamba auhimili uzazi ila tayari umetoa maua, niuache tu au kuna hatua ya kitaalam ya kufanya?
20210803_090826.jpg
 
Mwembe wangu bado mdogo sana na mwembamba auhimili uzazi ila tayari umetoa maua, niuache tu au kuna hatua ya kitaalam ya kufanya?View attachment 1878376
Kata hayo maua, uache mti uendelee kukua mpaka upate kimo na uimara wa kutosha kubeba maembe ndiyo utaachia maya, hiyo ni miaka 2 hadi 3 hivi...
Tumia mkasi kukata maua

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom