Naomba ushauri wa dhati

Spssp

New Member
Jun 14, 2021
2
2
Habari za humu wana MMU,

Mimi ni memba mzoefu humu hivyo nimeamua kuja na id mpya ili niweze kueleza hili jambo kwa uwazi zaidi.

Kwanza natambua kuna watu watakuja na kejeli,dharau na kutaka kulaani na kulalamika ila ikumbukwe lengo lakuleta uzi nikutaka kupata ufafanuzi au msaada kama upo kwa watu ambao wamakua kwenye maisha ya aina hii.

Kufanya maelezo mafup nikua mimi ni mhitimu wa chuo kimoja kikubwa tu nchi na niliajiriwa kwa miaka kadhaa mpk nilipoamua kijiajiri mwenyew.

Shida inayonisibu nikua nimekua sio muaminifu kwenye biashara kiasi cha kutengeneza madeni mengi sana kwenye kila biashara.Ieleweke sio kwamba nakua moja kwa moja sio mwaminifu ila inatokea tu circumstances then najikuta nipo kwenye madeni.

Biashara niliyonayo sasa iv imekua hivyo hivyo kiasi kwamba naona biashara chungu,yaan unakuta unadaiwa ana milion 3-4 ambazo ni madeni mbali mbali ambayo yanahusiana na biashara.

Mwanzo wakati naanza biashara zote( kwa biashara zote nlizowahi kufanya) hua biashara inakua nzuri sana ila muda unavyoenda mambo yanaanza kwenda kombo kiasi cha kufanya nianze kuingia kwenye madeni na biashara nyingine nimeacha nikiwa namadeni yawatu.

Kuhus imani zakishirikina nisingependa kuziongelea sana mana sina uhakika kwamba nikwel au nitabia tu yangu.

Kwa sasa hali yangu yakifedha ni dhohof lhali na nna madeni ambayo natakiwa niyalipe ambapo kwa muenendo huu sidhan kama ntayaweza.

Ushauri:
Naomba nishauriwe kwenye mambo kadhaa:
1.Namna yakuepukana na madeni kwenye maisha
2.Kua muaminifu kwenye biashara
3.Kutokutengeneza madeni mapya
4.Naamin huenda ata mambo yanakua maggum kwa sababu kuna watu nimewazima/nimewadhulumu au sijawalipa haki zao uko nyuma (namna yakaudeal na hichi kitu)

Note:
watu wote wanaonidai nimewaandika kwenye daftar maalum,kiasi cha pesa na namba zao za simu,ugumu umekua kwenye kupata fedha zakuwalipa.

Mambo ni mengi ila kwa leo naomba niishie hapa,ntaendelea siku za usoni.

Asanteni
 
Ushauri:
Naomba nishauriwe kwenye mambo kadhaa:
1.Namna yakuepukana na madeni kwenye maisha
2.Kua muaminifu kwenye biashara
3.Kutokutengeneza madeni mapya
4.Naamin huenda ata mambo yanakua maggum kwa sababu kuna watu nimewazima/nimewadhulumu au sijawalipa haki zao uko nyuma (namna yakaudeal na hichi kitu)
1.Namna ya kuepukana na madeni ni kuacha kukopa na kulipa madeni uliyonayo
2.Ili kuwa muaminifu kwenye biashara ni kumjua/kuwa na hofu ya Mungu na kuwa na utu
3.Usikope,lipa madeni yaliyopo
4.Namna ya kudeal na dhuluma ni kulipa uliowadhulumu
 
Hahahah wewe jamaa umenichekesha sana,umeandika kwa hisia sana.

sasa la kufanya.
-Toa zaka na sadaka ikiwa ni mkristo.
-Epuka kukopesha ukiwa kwenye biashara.
-Epuka wanawake.
-Acha kununua vitu ovyo ambavyo havipo kwenye mpangilio.
-Weka mikakati ya kukuza biashara kila siko sio uweke ukomo kwa kuona biashara imekua.
 
Ukifanya risk management na kupata discipline hapo unamaliza kila kitu. Wafanyabiashara wengi tu sio waaminifu kwa asili ila wanalazimika kuwa waaminifu kwa sababu ndio msingi wa biashara, usipoweza hili basi kajisalimishe Kyela kulima mpunga.

Mikopo unakopa ili iweje? Ni mzigo kwa biashara kukopa mkopo ili ule maisha alafu huo mkopo uulipe kwa faida inayotokana na biashara. Kopa ili uendeleze biashara, au ukiwa na emergency ambayo usipoikamilisha kwa fedha itaathiri uwezo wako wa kufanya biashara. Mfano kufanya upasuaji.

Pendelea kutumia sehemu ya faida pekee kama njia ya kukuza biashara kama huna uwezo mzuri wa kukabiliana na mikopo. Hii ni njia ndefu ya watu 'dhaifu' kama wewe. Kulingana na biashara yako inavolipa faida unaweza ifanya kama hivi mfano 50/30/20. Kwamba 50 unazungusha kwenye biashara kama inventory na running costs, 30 ni matumizi yako (reward), 20 ni savings kwa kukuza biashara baada ya kila miezi 6 maybe.

Naotea biashara zako zinakufa kwa sababu hujui stages za trade cycle ya hizo biashara.
Hujui 1. introduction (moderate sales) 2. growth (high sales & high profit) 3. maturity (entry of competitors, moderate sales) 4. decline (low sales, hasara inaanza).

Nafikiri wewe ukifika stage ya 3 unaanza kuvuruga unabaki na matumizi ya juu kama ya stage ya 2. Ukifika stage ya 4 unakopa ili uweke mambo sawa. Alafu you should be PROACTIVE, sio unaanza kupata changamoto ndio unatafuta suruhisho. Kwa nini biashara zako tofauti zife na zilikuwa kwenye faida. Ukitumia akili changamoto nyingi unaziona kabla hazijaja na unajipanga kuzikabili.

Mwisho, nimetoa general assumptions kwa vile haujawa specific ila naamini ukichezea humu unapenya.
NB: Nimejibu kulingana na madesa, mlioko field mniambie hizi mambo zipo au naingizwa chaka.
 
umeniongezea kitu,asante sana
 
Back
Top Bottom