Naomba ushauri: Ninapata Maumivu makubwa juu ya kifua, mgongo, mbavu na shingo

pulupu

Member
Aug 14, 2015
31
8
Tangu 2018 nilianza kusikia maumivu ya kifua nikaenda hospital nikafanya x ray wakasema Early stage of intestinal lung disease nikapewa dawa lakini maumivu yaliendelea.

Nikarudi tena kwa muda tofauti nikafanya x ray 2 kwa nyakati tofauti tatizo wakasema ni pneumonia nikatumia dawa nyingi lakini maumivu yaliendelea.

Mara ya mwisho january 2022 nimeenda tena nimefanya x ray wameniambia nina asthma nimepewa dozi ya wiki 2 bado sijamaliza.

Maumivu makubwa yapo juu ya kifua mgongo mbavu na shingo pia nilipima TB lakini haikuonekana kwa hiyo wataalamu wanaweza kunitoa ushauri wa nini cha kufanya
 
Pole kwa kuumwa.
Nadhani 2018 walimaanisha interstitial lung disease.

Kando ya hilo, ninashauri kama uko sehemu ambayo unaweza kufika hospitali kubwa zaidi ambayo kuna pulmonologist (daktari bingwa wa mfumo wa upumuaji) itakuwa ni vyema zaidi. Kama hakuna basi pata physician/daktari bingwa wa magonjwa ya ndani.

Kuna vipimo zaidi ya Xray, ambavyo vyaweza kusaidia kujua tatizo lako.

Lakini, ni vizuri kujiandaa vyema kuelezea historia ya tatizo, dalili uzipatazo, nini hufanya ujisikie vibaya zaidi, nini hukupa nafuu, kazi ulizowahi kufanya pia daktari atakuangalia kwa karibu/umakini zaidi na kuomba vipimo vitakavyosaidia kulijua tatizo la msingi ni nini?
 
Ni Intestial lung disease.... may be sarcoidosis, silicosis, kwani unafanya kazi mkuu? Lakini pia i would reccomend a CT scan of the chest
Tangu 2018 nilianza kusikia maumivu ya kifua nikaenda hospital nikafanya x ray wakasema Early stage of intestinal lung disease nikapewa dawa lakini maumivu yaliendelea...
 
Back
Top Bottom