Naomba ushauri, ninapata hali ya mapigo ya moyo kwenda mbio

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Ndugu zangu nina tatizo linalonisumbua sana siku izi ambalo sikuwa nalo apo mwanzo ili kuwa ijuma ine nilipata ajali nikiwa
Moyo wangu ukakata tamaa ya kuishi maana nilivyokuwa najisikia hakika ili kuwa hatari.

Kwanza nilikuwa nasikia maumivu makali, pili nilikuwa nasikia kama vile moto unawaka tumboni tumbo langu nikawa nasikia maumivu ya ajali na maumivu ya gesi tumboni nikawa naona kuwa ninataka kufa.

Nilivyokwenda hospitali doctor alinipima nikaonekana sina tatizo lolote bali ni maumivu tu ndo yanasumbua mwili wangu akanikataza kufanya kazi kubwa kubwa mpaka pale nitakapo pona kabisa sasa nikarudi nyumbani kufika Jumatano nikamuka yaani yale maumivu ya kawa yamesambaa mwili mzima mpaka kwenye mapafu nikawa nahisi kuwa mwisho wangu umefika nikawa nalia sana huku mawazo yakiwa mengi kichwani midamida nikawa fresh mawazo yakawa yameisha kabisa.

Sasa tulivyofika usiku nikasikia kichwa kizito sana kama vile ninataka kupoteza fahamu na kizunguzungu mida mida ikatulia kufika usiku mida ya saa 6 mapigo ya moyo yakawa yanaenda kasi nikawa naogopa saana familia yangu wakaita ambulance madoctor walivyofika moyo ukatulia tena wakaniuliza nini tatizo, nikasema tatizo mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kasi.

Wakanibeba hospitali wakaniweka île sehemu ya mangojeo maana nilikuwa siko mgonjwa baada ya hapo niliongea na Brother yangu kwenye simu akaniambia kama kuna chochote unachowazia achana nacho. Maneno ya bro wangu yakanipa nguvu.

Nikarudi nyumbani bila kuonana na doctor kufika Alhamisi asubuhi nikawa nahisi moyo tena unaenda kasi kama vile unataka kutoka nilivyotoka nyumbani kuzunguka mitaani nikahisi umepona kufika usiku ya Ijumaa mida ya saa saba usiku nikawa naona tena unaenda kasi kama vile unataka kutoka nikakosa raha saana nikajikaza nikalala kufika jioni ya saa kumi na moja ya Ijuma nikaona tena moyo unaanza kudunda kama vile unataka kutoka walivyokuja marafiki zangu wakanipa ushauri nikaona umetulia tena.

Sasa najiuliza ivi huu ni ugonjwa au

Maana nikiangalia sina kitu kinachokifikiria zaidi

Je, ile wasiwasi niliyokuwa nayo kipindi na pata ile ajali kuwa ninataka kutoka duniani ndo inaweza kuwa sababu au nini? Maana sielewi mimi.
 
Shetani ameyatawala mawazo yako, anachofanya anakuletea HOFU KUU katika kila hatua ya maisha yako.

Kukata mzizi wa fitna, Tubu dhambi zako zote mbele ya USO WA MUNGU kwa IMANI YAKO.

WASAMEHE wale wote waliokukosea na ujisamehe mwenyewe binafsi kwa maana huwezi kupata kibali cha MSAMAHA kama wewe huwezi KUSAMEHE.

Kama unatumia pombe, sigara na bangi acha mara moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu, naona umeeleza shida inayofanana na niliyopata miaka mingi iliyopita – 2007.

Ilitokea siku moja nikawa nahisi kana kwamba nakaribia kufa. Literally. Niliji-self diagnose nikajiaminisha nina matatizo ya moyo au presha kali sana. Mapigo ya moyo yalikuwa kasi isivyo kawaida na nilikuwa nahisi yanazidi kila ninapoyazingatia.

Hali hii ilikuwa ikitulia kidogo ninapokuwa na marafiki tunapiga stori, then nikiwa peke yangu (hususan kitandani) ndiyo hali inazidi kuwa mbaya. Nilikuwa nikikosa usingizi kwa mawazo mengi sana ya kufa kufa tu. Kila siku nilikuwa najihisi siwezi kutoboa siku inayofuata. Kuna siku hadi nikaona giza limenijia ila bahati nzuri nilikuwa karibu na kitu cha kujiegemeza.

Sina hakika kwanini sikuwashirikisha wazazi, ndugu na jamaa au daktari.

Nilikomaa na hali yangu hiyo kwa muda wa wiki kadhaa. Kitu pekee nilikuwa nikifanya ni kujichanganya na watu ili kupata ahueni.

Baadaye nilianza kujiambia tu mwenyewe kuwa “sina tatizo” na kwakweli ingawa ilichukua siku kadhaa, lakini nilijikuta naondokana na hali hiyo. Mpaka sasa ni zaidi ya miaka 10 na sijawahi ku-experience kitu cha namna hiyo.

Hivyo ndugu yangu, kama nimeelewa vizuri ulichoandika hapa, basi ninaelewa hali unayopitia. Inaweza ku-sound kama vile ni kitu kidogo sana kwa yeyote ambaye hajawahi kukutana na hali hii.

Endelea kuwa karibu na wataalamu wa afya, nduguzo na marafiki, ila zaidi ni wewe binafsi kujiondolea hiyo hofu – ambayo naamini hata wewe mwenyewe hujui inaletwa na nini. Mimi pia nilikuwa nikijaribu kukijua chanzo ila nilishindwa kupata jibu. Tena heri yako wewe angalau una pa kuegemeza hofu yako – hiyo ajali uliyopata.

Naamini hauna sababu ya kuendelea kujihisi hivyo. Tuliza tu huo moyo maisha yaendelee.
 
Achana na vyakula vyenye cholesterol nyingi, kama vyakula vya zao la wanyama, parachichi, na nuts. Eat good diet
 
Ndugu zangu nina tatizo linalonisumbua sana siku izi ambalo sikuwa nalo apo mwanzo ili kuwa ijuma ine nilipata ajali nikiwa
Moyo wangu ukakata tamaa ya kuishi maana nilivyokuwa najisikia hakika ili kuwa hatari.

Kwanza nilikuwa nasikia maumivu makali, pili nilikuwa nasikia kama vile moto unawaka tumboni tumbo langu nikawa nasikia maumivu ya ajali na maumivu ya gesi tumboni nikawa naona kuwa ninataka kufa.

Nilivyokwenda hospitali doctor alinipima nikaonekana sina tatizo lolote bali ni maumivu tu ndo yanasumbua mwili wangu akanikataza kufanya kazi kubwa kubwa mpaka pale nitakapo pona kabisa sasa nikarudi nyumbani kufika Jumatano nikamuka yaani yale maumivu ya kawa yamesambaa mwili mzima mpaka kwenye mapafu nikawa nahisi kuwa mwisho wangu umefika nikawa nalia sana huku mawazo yakiwa mengi kichwani midamida nikawa fresh mawazo yakawa yameisha kabisa.

Sasa tulivyofika usiku nikasikia kichwa kizito sana kama vile ninataka kupoteza fahamu na kizunguzungu mida mida ikatulia kufika usiku mida ya saa 6 mapigo ya moyo yakawa yanaenda kasi nikawa naogopa saana familia yangu wakaita ambulance madoctor walivyofika moyo ukatulia tena wakaniuliza nini tatizo, nikasema tatizo mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kasi.

Wakanibeba hospitali wakaniweka île sehemu ya mangojeo maana nilikuwa siko mgonjwa baada ya hapo niliongea na Brother yangu kwenye simu akaniambia kama kuna chochote unachowazia achana nacho. Maneno ya bro wangu yakanipa nguvu.

Nikarudi nyumbani bila kuonana na doctor kufika Alhamisi asubuhi nikawa nahisi moyo tena unaenda kasi kama vile unataka kutoka nilivyotoka nyumbani kuzunguka mitaani nikahisi umepona kufika usiku ya Ijumaa mida ya saa saba usiku nikawa naona tena unaenda kasi kama vile unataka kutoka nikakosa raha saana nikajikaza nikalala kufika jioni ya saa kumi na moja ya Ijuma nikaona tena moyo unaanza kudunda kama vile unataka kutoka walivyokuja marafiki zangu wakanipa ushauri nikaona umetulia tena.

Sasa najiuliza ivi huu ni ugonjwa au

Maana nikiangalia sina kitu kinachokifikiria zaidi

Je, ile wasiwasi niliyokuwa nayo kipindi na pata ile ajali kuwa ninataka kutoka duniani ndo inaweza kuwa sababu au nini? Maana sielewi mimi.
Kwa maelezo yako inaonyesha umekumbwa na pepo mchafu shetani mbaya ndio anaye kutia wasiwasi na moyo wako kwenda mbio hakuna dawa ya hospitali itakayoweza kukutibia na ukapona nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole kijana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom