Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Mabinti wa Ngara sijui mnamatatizo gani! Wahangaza full,maigizo nakujiona wao ni wazuri sana, huko uendako tegemea mengi na sio kama unavyodhani! Unaweza enda ukarudi mguu umevimba, usichezee kabisa akili za watu,wanaweza kukufanya ndondocha!
Hawajui watu wa Mbeya huyu asiende kabisa huko maana atarudi na kiwiliwili tu kichwa wanabaki nacho.
Asijaribu kwenda.
 
Jamani mambo zenu, Niko katika wakati mgumu
Mimi ni binti wa miaka 29 kwa sasa, nimempata mwanaume ambaye tulipanga mengi sana hadi kupanga jinsi ya kufunga ndoa,

Mwaka fulani niliingia kwenye mahusiano na kijana mmoja toka Mbeya, ila kwa sasa anaishi Afrika ya Kusini kwa shughuli zake ,
Tulikubaliana kuanza kutambulishana kwao, na kwetu

Nakumbuka alinilipia nauli ya ndege nikaenda kwao kutambulishwa nikamshukuru Mungu kwamba nimepata mme sasa,

Tumeendelea na utaratibu na mshenga akatumwa kwetu kusema, baada ya kuondoka nikamweleza mama kuwa kijana sawa ananipenda ila hapendi jambo fulan ambalo kwa ukweli sitalisema hapa, mama akasema kama ndo hivo sitak habari zako za kuolewa,

Ikabidi mchakato uendelee kawaida, wakaleta kishika uchumba mama akawa hataki kushiriki hata kidogo, anasusa, sasa shangazi yangu akaniambia kwamba kwakuwa huna baba naomba ili suala tuwashirikishe baba wadogo na wajomba tuendelee na nchakato,

Baada ya muda tukapanga wataletaje mahari na siku ya send off tukaipanga,

Sasa kabla ya send off siku moja kabla tukapata habari kupitia kwa mjomba kwamba Mwanaume anayeenda kunioa kumbe ana mke mi naenda kuwa mke wa pili, taarifa hii ikawachanganya wote hata wajomba wakasema ngoja wajiweke pembeni, maandalizi ya send off yakavurugika wakati huo wakwe wakiwa njiani kuhudhuria sherehe hiyo , walikodi Costa na magari kadhaa kutoka mbeya hadi Ngara,

Wakanikimbia ndugu zangu wote nami nikachanganyikiwa kwa hasira sikutokea kwenye send off na maandalizi ikawa hasara, wakapiga simu nikazima nilikuwa na hasira sana,

Baadaye nikawasha simu nikakuta mama mkwe mtarajiwa amenitumia meseji kwamba "Sikutegemea kama ungetufanyia haya, sisi tunajiandaa kesho tunarudi lakini baki na amani"

Niliumia sana Akaendelea kunitumia meseji za machungu nikijua naye anajua kuwa Mwanae ana mke na mama huyu tumeongea kila siku niliumia,

Sasa yule mchumba wangu akawa ananitafta sipokei nikamwambia sina Muda mchafu wa kuolewa na wewe, hapo sikumwambia kwanini nimebadili mawazo,

Sasa nakumbuka siku kadhaa baadae naitwa nyumbani kwamba kuna kikao,

Kumbe kuna taarifa kwamba yule kijana hakuwa ameoa ila alichumbia sehemu akalipa mahari ila kumbe hakuoa,

Habari zilisononesha sana

Nikaenda kwa askofu mmoja akanishauri

1.Ama tuombe radhi kwao kuendelea na mchakato

2.Ama tuwape kishika uchumba chao maana mahari alikuwa bado angetoa siku ya send off asubuhi yake,

Naomba ushauri wenu plz

Nimeikosea Sana familia ile, pia hasira baada ya kupungua natamani niolewe naye japo nashindwa naanzaje

-----------------------------------

Nimeamua kuwaambia ukoo wangu, Kuanzia Mama sina Baba R.I.P
Mashangazi, Baba Mdogo na wajomba nia yangu ya dhati kuiomba msamaha familia ya ambaye alikuwa mchumba wangu,

Naenda kuomba msamaha nikitegemea maswali magumu,

Naenda Kuomba msamaha nikijua maumivu na uchungu hata hasara waliyopata kutoka Mbeya hadi Ngara,

Hatua ya Kwanza
Nimeamua niangalie upepo ndani ya familia yangu, idadi ya wanaonisapot,

Niangalie mtazamo wao juu ya kwanini nasukumwa kuomba msamaha,

Tatu naangalia dhamira yangu na msukumo wa moyo wa dhati,

Nne Nimeamua kuwashirikisha ndugu na kuwaambia sitaenda moja kwa moja kwa wakwe ila ntaenda kwa mshenga

Tutaenda timu ya watu 7 watu wazima sita na mimi nikiwa wa saba, katika timu hiyo mama aneendelea kugoma kutoshiriki, Nimepata shangazi mama mdogo na baba mkubwa,na wengine

Tutaelekea kwa mshenga kuomba radhi, na kueleza sababu za kutokuwapo kwenye send off alafu tumuombe atuombee msamaha,

Baada ya wao kujua tunaomba msamaha kup kwa mshenga

Nimeandaa kishika uchumba walicholipa na nimeandaa wazee 5 na wanisindikize Mbeya kutoka Ngara kwenda kuomba msamaha na pia kabla ya kufika kwenye familia ya wakwe, tutapitia kwenye parokia iliyokaribu kumuona kiongozi wa dini atupe mwongozo na kumuomba atupe ushirikiano kufika kule, pia tutaomba aambatane na wazee wa heshima wa Kanisa, hii nitaifanya tu hata wasipotoa jibu pitia kwa Mshenga

Nikifika nitakuwa na maombi mawili

1.Kuomba kusamehewa na kurudisha kishika uchumba chao

Ama

2.Kuomba kusamehewa na kuendelea na mchakato wa harusi kama watakua bado hawajapata mtu.

Naombenii mawazo yenu mengine pia

asante
Dada pole sana,kaombe radhi ni sawa lakini usiombe kurudia mchakato,huyo mwanaume hakuwa rizki yako,ni uungwana kuomba radhi na rudisha kishika uchumba,then rudini kwenu,Mola atakuletea mume wako

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
japo muda umepita lkn wacha nikwambie

una miaka 29,
halaf single mama

ulivyosikia mwenzako kaoa ukashikwa na hasira

asa cha ajabu ni kipi hapo??
mbona wewe ulishazaa. hata km haukuolewa.

unataka mume wa peke yako na wakat wewe ulishakuwa mke wa mtu??

we siyo mstaarabu hata kdg
kwanza hufai kuwa mke..

bora hilo lilijitokeaza
 
Singo maza huo ujasiri uliutoa wapi!? Mtu keshamlipia mwanao na kakubali kumhudumia kama wake, possibly na kwenu alikuwa anawahudumia, huo ujasiri wa kuchagua ulichokichagua kwa hatua za mwisho uliutolea wapi hata kama nduguzo walijiweka kando nawe!? Mazafaka
Huyu dada naomba niseme pia mamaake nae akili ndogo, tena ndogo sana...tusimlaumu tu yeye
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom