Naomba ushauri: Nimeshinda kesi ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu lakini nataka kukata rufaa

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,058
Habari za kazi wapendwa,

Kuna jamaa mmoja aliniuzia kiwanja mwaka jana mwezi julai ambapo makubaliano yalikuwa nimlipe awamu mbili ambapo awamu ya kwanza nilimlipa nusu na awamu ya pili nusu yake nikamalizia.

Sasa baadae nikawapeleka watu wa ardhi na kugundua kwamba bikoni zilizokuwa shambani hazikuwa za watu wa ardhi bali Huyo jamaa aliuza mara mbili eneo hilo yaani alimuuzia mtu mwingine.

Majaribio ya awali ya kusuruhisha yalishindikana ambapo nilimfungulia kesi.

Hukumu iliyotoka ni kwamba jamaa anatakiwa alipe faini ya elfu hamsini au afungwe jela mwezi mmoja.

Harafu baada ya mwezi mmoja jamaa anilipe hela wakati mie nilidhani aliyeuziwa mara ya pili ndio anatakiwa arudishiwe hela kisha mimi nibaki na kiwanja. Je haki imetendeka au nimuone wakili tukate rufaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rufaa nakata mahakama ya wilaya ama sivyo?
Kuna mtu kanichanganya anadai hata mahakama ya wilaya haina jurisdiction ya kunimilikisha ardhi.
Amenishauri kwamba kuna mabaraza ya ardhi, hii imekaaje?

Sent using Jamii Forums mobile app

Yes
Ambapo kama mliuziana chini ya mwenyekiti au mtendaji wa serikali ya mtaa husika, nae ataitwa na baraza la ardhi

Mliuziana kivipi kwanza? Chini ya serikali ya mtaa? Wenyewe binafsi tu? Au chini ya advocate?
 
Kama unataka kupinga adhabu aliyopewa na primary court (assuming ndo ilitoa hukumi) kata rufaa DC. Ila kama unataka possession ya kiwanja nenda baraza la ardhi na nyumba la wilaya uliopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya mtaa, na mwenyekiti aliyehusika alipigwa chini kutokana na kusababisha matatizo mengi ya ardhi na kukosa uaminifu.

Back
Top Bottom