Naomba ushauri, nimekwama. Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Yna2

JF-Expert Member
Aug 18, 2018
22,636
2,000
Kwa sababu story ilikuwa mwanzo sana, na story ilikuwa inahusu bi mdogo, sikutaka sana kumzungumzia yeye, nimeona hata wengine wanasema muda mwingi nilikuwa natumia kwa bi mdogo, hapana nilikuwa nabalanci sana muda wangu ili kila upande ulizike, na kuwa kazi zangu zilikuwa ni za masaa tofauti tofauti, mala usiku mala mchana, mala weekend unaenda unapumzika katikati ya wiki (shift), mala safari, mala overtim e, hayo yote yalisaidia sana kuonekana pande zote na wakawa wamezoea hiyo mienendo yangu,

Kuhusu bi mkubwa kugundua alikuja gundua baadaye sana, kwanza baada ya bi mdomo kuniwekea chupi ya mtoto kwenye bag langu, wakati nimetoka safari,
Hapo pamoja na kujitetea ndio alipoamza kuweka Q mark,

Baadaye sana sasa ikawa wazi kabisa ,
Ila alinaambia yeye hataki mtoto kwake, kama ni nyuma niwajenge e huko huko
Kwahiyo kumbe bimkubwa alijua Kama ana mwenzie !?? 🙄 Aisee
 
Mwitore

JF-Expert Member
Feb 9, 2021
296
1,000
Ushauri wangu ni huu. Huyo mwanamke mwanzoni nilikuwa nampa heshima ya bi mdogo kama ulovyoomba tumuite (badala ya mchepuko). Ila baada ya kusoma hitimisho lako nimeona jina sahihi la kumpa huyo mwanamke ni Mchepuko. Toka nimeanza kukusoma sijaona mahali kuwa ulifunga naye ndoa huyo mchepuko. Cha kufanya hiyo nyumba mshirikishe mke wako halali (bi mkubwa). Hiyo kesi muuzie bi mkubwa ataimaliza fresh kabisa. Huyo mchepuko hastahili tena upendo wako. Hata mwenyezi Mungu hutoa adhabu kwa wanaokosea wewe ni nani usimpe adhabu huyo mwanamke? Najua kisheria kuna kauponyo kidogo anaweza kukupelekesha kwa kuwa umeishi naye kwa muda mrefu lakini nina uhakika ukikomaa anaweza asipate hata cent tano. Hiyo nyumba itakuwa yenu (wewe na mke mkubwa). Watoto wa mchepuko unaweza kuwapa kama urithi kwa baadae. Mwisho kabisa, najua unampenda sana huyo mchepuko ila kaka mkubwa umeshamla vya kutosha sana. 20 years unamkamua hana jipya tena na huna ulichobakiza kwake. Mfutilie mbali kabisa.
Ahsante sana, Mwenyezi Mungu akubariki sana, ni ushauri mzuri, kwanza niliogopa sana, kumfukuza nikijua kuwa, atasema labda nimemtumia vya kutosha sasa nimemchoka narudi kwa mke,
Lakini baada ya kugundua anaendelea na mwanaume ambaye, nilishamtuhumu miaka 10 iliyopita pamoja na visa vyote hivi na kiburi, kumbe naye ana bwana yake pembeni, hapana uzalendo umenishinda, potelea mbali , kama ataniraumu basi ni mwendelezo wa akili zake ndogo kutokujua makosa, kwa kipindi chote hicho,

Lingine nililogundua kumbe hata hizo biashara ya mchele huko Morogoro walikuwa wapo pamoja,

Ila mbaya zaidi pamoja na malalamiko yangu kwa wazazi wake, lakini hawaonyeshi hata kushtuka,

Mfano halisi ni sasa hivi, mtoto wao yupo kwao lakini hata kunipigia simu, kuniulizia kulikoni hakuna! Mpaka bajiuliza hii ni familia ya aina gani,

Mpaka nawaeleza waziwazi kabisa mbona mtoto wenu anatembea na aliyewahi kuwa mkwenu ( huyo bwana alishawahi kuoa binamu ya mke mdogo) wakagombana baada ya kufumaniana,

Na jamaa akataka kumuua mgoni wake kisu,
Akatoroka kijiji kwa muda fulani.
Lakini mpaka nafikia hatua ya kuwaambia wazi wazi, kuwa mlikuwa mnanidanganya kumbe mnajua mtoto wenu ana wanaume wawili halafu mkiendelea kuniomba vimisaada, na kuwakatia simu ambapo leo ni wiki ya tatu hawanipigia tena!
 
Father achana na huyo mwanamke..achana na hiyo familia.
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
142,909
2,000
Samahani km ntakwaza watu lakini mi naupenda uislamu wangu uliohalalisha wake wanne. Kwa kweli toka dunia ianze wanaume hawajawahi kutosha huyo Dada Leo miaka 20 na zaidi anaishia kuitwa mchepuko wakati angekua muislam angemuoa.

Kingine mbona wakurya wana mitala nnao huku kanda maalum yaani mitala kama zote .

Huyo demu nae kimeo 20yrs unakubali kufichwa km Arv vile...!!! Au ndo tamaa ya pesa mweee!pole yake aseh

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu; hivi utaratibu wa kusilimu ukoje?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom