Naomba ushauri: Nijiajiri au niendelee kuajiriwa?

I AM NO ONE

JF-Expert Member
Aug 7, 2020
389
576
Habari.

Naomba ushauri aise katika hili. Nataka kuanzisha biashara yangu binafsi ya genge mix duka. Mpk dk hii tyr 90% nimeshafanya nimekod fremu meza shelf tyr nimetengeneza na rangi safi nyeupe nimepiga. Ila nakabiliwa na mgogoro wa baina ya mawazo yangu na mawazo ya wazazi wangu.

Wazazi wananiambia nisiache kazi. Me mawazo yangu nataka kuacha kazi. Maana kipato nachoingiza ni kidg mno ukilinganisha na mtaji ambao naotaka kuuweka kwenye duka langu.

Nataka kuacha kazi kwakuwa nataka nilinde mtaji wangu ninaotaka kuuweka dukani na kwenye gengelangu. Maana nimesota sana mpk kupata mtaji huo.

Wananishauri niweke kijana lakn akili yangu na fikra zangu zinaniambia nisimamie kazi yangu. Yan napata roho ya ujasiri inayoniambia simamia kazi yako. Rizk sio mpka ajira. Hta ukijiajiri mwenyewe pia utapata mafanikio makubwa kuliko kusubiri laki 3 ya muhindi
 
Kama unajiamini acha hiyo kazi ila baadae usije kusema unajuta kuacha kazi

Mazingira yenyewe ya biashara siku hizi kizungumkuti
 
Usiache kazi kabla biashara yako haijasimama kwa miguu miwili. PIA ukiendelea kubaki na kazi yako utakuwa una source mbili za mapato kwa muda flan mpka biashara yako itakapo simama. Tatu tafuta ndugu yako wa karibu ndio akae kwanza dukan sio mtu usiefahamiana vizur.

Na mwisho kabisa fanya recording nzuri ya miezi 6 ya mapato na matumizi na pia uweke servings, baada ya miez hiyo 6 ndio uamue either uache kaz au la, hapo utakuwa umeshajua mzunguko wa biashara kama inaweza kukulipia pango la miezi 6 ijayo na ukabakiwa na mtaji plus hela ya faida. ZA KUAMBIWA, CHAMBUA NDIO UZICHANGANYE NA ZA KWAKO
 
Kama unafanya kazi kwa Mhindi mkuu, na sasaivi umepata mtaji nakuambia kwa moyo mkunjufu kabisa nenda kajiajili kimbia kabisa uko mkuu nawajua hao watu
Hawa jamaa ni shida huu mwaka wa pili sasa kutoka laki 3 wameongeza 20000 inachekesha lkn inauma mno
 
Usiache kazi kabla biashara yako haijasimama kwa miguu miwili. PIA ukiendelea kubaki na kazi yako utakuwa una source mbili za mapato kwa muda flan mpka biashara yako itakapo simama...
Fresh imekaa poa hii mkuu
 
Wapo sahihi na wew upo sahihi,shida ni upi muda wa kufanya lipi. Fungua genge endelea na kazi mpka pale utakapoona linaweza kuendesha maisha yako kuliko kazi unayofanya.

Hayo ya motivational speakers kuwa ukiamini basi itakuwa achana nayo maana utajua hujui pale utakapoacha kazi na biashara haienda huku mtendaji anakuletea kadi ya mjasiriamali kwa 20,000.
 
Wapo sahihi na wew upo sahihi,shida ni upi muda wa kufanya lipi.
Fungua genge endelea na kazi mpka pale utakapoona linaweza kuendesha maisha yako kuliko kazi unayofanya.

Hayo ya motivational speakers kuwa ukiamini basi itakuwa achana nayo maana utajua hujui pale utakapoacha kazi na biashara haienda huku mtendaji anakuletea kadi ya mjasiriamali kwa 20,000.
Sawa mkuu shukran
 
Do this. Usiache Kazi, lkn husika na biashara Yako 100%.

Amka mapema zaidi nenda sokoni kanunie mzigo wako. Ufikishe gengeni na panga bei zako na take note kwenye daftari. Kisha wewe nenda job.

Jioni ukitoka nenda kwenye hiyo side hustle yako- genge kapige mahesabu na iweje Mambo sawa huku ukichukua kiasi Cha kesho Cha kuingia sokoni Alfajiri tena.

Nakurudia tena usiache Kazi huku unaingia kwenye side hustle mpya kwa miguu yote miwili. Ajira ni mbaya ukiwa nayo. Ukitoka kiboya utasaga na kung'ata meno na ukirudi hapa hatutasita kukunyoosha.
 
Sasa ushaingia gharama zote hizo ndio unaomba ushauri? Laki 3 ya muhindi ndogo sana huo mtaji umeupata wapi? Punguza kukurupuka fikiria kwa kina vinginevyo utafeli vibaya.
 
Sasa ushaingia gharama zote hizo ndio unaomba ushauri? Laki 3 ya muhindi ndogo sana huo mtaji umeupata wapi? Punguza kukurupuka fikiria kwa kina vinginevyo utafeli vibaya.
Mtaji wa million na nusu mzee ni mkubwa cjatomba hovyo mm cjahonga kiboya nimejikza balaa.
 
Weka kijana kwa sasa
Usiache kazi mkuu
Acha biashara ichangamke kwanza unaweza kuacha kazi baadaye ukipata mtaji mwingine tena Mkuu
Biashara ni ngumu sana sana mwanzoni naileta stress utakupa mawazo nakukubuka ajira yako mapema sana
 
Do this. Usiache Kazi, lkn husika na biashara Yako 100%.

Amka mapema zaidi nenda sokoni kanunie mzigo wako. Ufikishe gengeni na panga bei zako na take note kwenye daftari. Kisha wewe nenda job.

Jioni ukitoka nenda kwenye hiyo side hustle yako- genge kapige mahesabu na iweje Mambo sawa huku ukichukua kiasi Cha kesho Cha kuingia sokoni Alfajiri tena.

Nakurudia tena usiache Kazi huku unaingia kwenye side hustle mpya kwa miguu yote miwili. Ajira ni mbaya ukiwa nayo. Ukitoka kiboya utasaga na kung'ata meno na ukirudi hapa hatutasita kukunyoosha.
Ushauri wako ni mzuri lakini jamaa atasagika hasa.
Kama yupo dar hii narudia tena atasota sana kufanya vyote kwa wakati mmoja.
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom