Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

kila kitu kipo tayari computer kama kumi tatizo sijajua gharama za bundle ntanunuaje wakuu msaada

Kaka mm ni mtaalamu wa mambo ya internet.
Nitafute. Nutakuwekea net ya bei nzuri zaidi, itakuwa hauna haja ya kuwabana wateja kuangalia video ila sharti langu uweke wikwazo kwa yyt atakae angalia vitu kinyume na maadili. C
 
unataka kufungua computer training, utaajiri walimu? Kama mwalimu ni mwenyewe inakuwaje hujui hata maana ya WIFI,

Acha ushamba, ualimu na umiliki ni vitu viwili tofauti. hana ulazima kufundisha yeye mmiliki.

pili, wifi haimzuii mtu, wifi ni wireless internet program haina uhusiano na kuijua ndo ufungue cafe. wifi isikuzingue ni kitu kidogo na program ya kawa. kama alivyo jieleza. c lazima kuwa na komputer nyingi. tano,sita zitatosha ukichanganya na mpesa,tigo, dstv,luku nk na mambo mengne. just do it men.
 
Kaka mm ni mtaalamu wa mambo ya internet....
Nitafute. Nutakuwekea net ya bei nzuri zaidi.... itakuwa hauna haja ya kuwabana wateja kuangalia video... ila sharti langu uweke wikwazo kwa yyt atakae angalia vitu kinyume na maadili.

Bei gani ntajie bei zako nicheki inbox
 
mapato yakoje kwa mwezi,

mimj yangu minimum maana ni internet cafe natoa huduma za photocopy na printing so daily minimum napata 30000 siku nyingine napata mpaka 90000, nimeweka wasimamizi wazuri maana mimi sikai
 
Nitaajili walimu mana nimepata Desktop kumi nimeona ni bora nisajili Training Centre ya Computer ambayo naamini itakuwa ni ya maana sana kwangu..Kwenye ishu za Internet siko vizuri kihivoo ila kupitia hawa walimu itanisaidia sana..
 
kila kitu kipo tayari computer kama kumi tatizo sijajua gharama za bundle ntanunuaje wakuu msaada

Umechezea mtaji wako sanaaa. Hebu kabla hujafanya biashara fanya research na muombe Mungu akupe busara za kufanya smart business decisions/moves. Mtu anaeijua pesa vizuri hawezi fanya biashara kama hyo...ni aheri ungenunua bajaj used/mpya ukaendesha mwenyewe. Hii biashara siku hzi haina dili tena kwa hapa mjini sababu ziko nyingi fanya research utajua. Kama utaifanya basi weka karibu na chuo au sehemu yenye wingi wa watu lakn still kwa maono yangu naona hailipi return ni ya kusua sua sanaa.
 
Hahahahaha utani mwingine kiboko, yaani wewe unatarajia kufungua shule ya kompyuta na hujui maana ya wifi?
Ebo! Hao utakaowafundisha wataishia kuangalia filamu na nyimbo za kina Diamond.

Sasa hiyo shule da.na unafungua internet cf hata msingi wa komputer tu huna.na hiyo shule? Mi nazani ni vizuri kuwa na hataka idea kakomputer ili ukiajiri mtu usije ibiwa.
 
Msibishane jamani kwani nani alizaliwa na computer zote zimetoka ulaya wewe usielewa tafuta mda ujifunze ni rahisi. kwenye maisha ili ufanikiwe lazima ujiamini kama unaweza.
 
Biashara ya internet cafe africa na Tanzania kwa ujumla bado ni big deal, cha muhimu ni location tu ambayo mtu anahitaji kusite. Mi nipo kwenye hii biashara tangu 2007 na nimesoma A'level na chuo kwa mgongo wa hii biashara ya internet cafe ambayo wengi wetu hapa wanaona kama imekufa kibudu.

Ni kweli ujio wa smartfones umepunguza biashara ya internet cafe , nacho amini kila siku katika hii biashara, Biashara ni wewe mwenyewe unavyo ihandle, speed nzuri ya mtandao, mazingira safi na machine zako zikoje hasa katika mantainance. internet cafe nyingi zimekufa hasa kutokana na wengi kufanya biashara hii bila kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu computer, matengenezo na n.k. hivyo kuwafanya kuwa watumwa kwa mafundi computer kitu ambacho kinapelekea kuua mitaji na machine kufa.

Tusidanganyane kwamba eti kwenye simu na tablet waweza surfing kama unavyofanya kwenye computer, na simu zenyewe zinavyokula chaji kama zina majini. Jipange na simamia biashara yako kwa uhakika bro, speed iwe ya uhakika na ufanye mantainance....utaenjoy hii biashara.
 
Binafsi sikushauri biashara hiyo. mimi nilifanya biashara hiyo mwaka 1999-2003, hapa Dar es salaam.. niliweka Internet cafe pale juu ya jengo la Vijana, nyingine kwenye kona ya Jamhuri na Moscow mitaa ya Kisutu, na nyingine mtaa wa Zanaki. karibu na keep left ya Channel Ten. zilikuwa zinaitwa PLANET INTERNET C@FE.... IC nilikuwa napiga mshiko. nusu saa tsh 1000.

Hadi wakati wa Y2K Mwaka 2000. nilikuwa nauza JACKPORT BINGO, VOCHA ZA TRITEL daaah umenikumbusha mbaaali sana. cafe moja nilifunga computer 17, nyingine 14 nyingine 9.

usiku wahindi kibao walikuwa wanakuja kuangalia picha za x.. wa Tz wengi walikuwa hawajui kutumia internet, so kumsajili mtu e-mail moja ilikuwa sh. 3000. wakati huo biashara ilikuwa nzuri sana.

ilipokuja Vodacom hapo nikwa nauza na line za voda. ilikuwa Tsh. 30'000 kwa line moja.
ilikuwa biashara safi sana.

sasa hivi. utapataje faida kwenye internet? face book ipo mikononi mwa watu.
Bank wenyewe sasa hivi wanapunguza Tellers, kwasababu ya Tigo pesa na M-pesa.

Bora ufungue stationary ya kawaida tu.
 
Habari za asubuhi wadau wa jukwaa hili,

Natumai miongoni mwetu kuna watu ambao wanafanya biashara tajwa hapo juu, waliowahi kuifanya na wenye idea na biashara hiyo.

Je ni vifaa gani vinavyohitajika na vya muhimu ili kuendesha biashara hiyo? Ni mahali gani ninaweza kupata vifaa hivyo kwa bei nzuri na genuine? Ni jinsi gani unaweza kumonitor biashara hiyo? Na kama kuna angalizo ama chochote ambacho unakifahamu kuhusu biashara tajwa tafadhali usisite kutoa mchango / mawazo yako.

Natangulisha shukrani.

Wasalaam
CL
 
Back
Top Bottom