Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

Shukrani kwa mtoa mada pamoja na wachangiaji wote. Binafsi pia niko kwene mchakato wa biashara ya namna hii, tatizo ni kwamba sijafanya utafiti wa kutosha juu ya soko, zaidi location, nimekuwa nikifikilia zaidi Dar au Mwanza ambako kote nina makazi, hata hivyo mpaka hivi sasa bado sijapata uamuzi wa wapi pa kwenda na lini kwani upatikanaji wa taarifa/market research umekuwa unasumbua na kunitatanisha kwa namna fulani.

Sehemu ya plan zangu ni kuwa na mass printing including posters, tayari nina baadhi ya commercial/heaavy duty equipments ie design jet printer, printer for tshirts, caps, pens tea cups and plates, stickers etc, pia nina printer ya kutengeneza plastic IDs zisizo na chip lakini pia kuna uwezekano wa kupata yenye chip iwapo nitakuwa na uhakika wa kupata wateja kwani hili kidogo linahitaji kuwa na kitu kama contaract hivi na office au shule ambapo pia itabidi niwe na either help desk au nawatembelea mara kwa mara as it need software to do it.

Kwa haya machache nitashukuru kama nitapata maelezo mawili matatu kutoka kwenu wana JF, Natanguliza shukrani.
 
zaidi location, nimekuwa nikifikilia zaidi Dar au Mwanza

Am sure Dar kuna more Competition kuliko Mwanza, lakini uzuri wa siku hizi Transport between regions ni rahisi unaweza ukaweka heavy machines dar, lakini ukawa na office mikoani mfano mwanza. Hii Issue its all about marketing kama utapata mteja lets wa poster Mwanza, unaweza ukafanya graphics design Mwanza ukatuma Dar wakafanya Kazi alafu ikarudishwa Mwanza kwa mteja, sababu hizi kazi normally mtu anakupa muda even two to three weeks.

Kuna watu wengi ni madalali wa printing hawana mashine, kazi zao ni kwenda wilayani kutafuta tenders na kupeleka kwa mwenye mashine kufanyiwa kazi na kupata cha juu (printing brokers) sasa maadam wewe una mashine na kazi yako ni nzuri, utapata wateja tena hata sehemu ambazo hauna office (uzuri wa technology you can have an office in your briefcase).., Mfano mzuri watu wengi wanaoprint rangi mikoani huwa hakuna colour separation inabidi wapeleke dar. My point is its not necessary to do everything, you can outsource.
 
Nimetaja competition sababu as you know wewe ndio unajua ubavu wako, je una nguvu kiasi gani ? na je unaouwezo wa kutoa good quality at a low price kulinganisha na wenzako ?, kwahiyo cha kufanya ni kwa haraka kuangalia bei za wenzako na kuona kama you can do better than them au kama wenyewe na bado ukatoa bei kama yao au chini ya kwao. Kuhusu Tshirts je itakuwa screen printing au Heat transfer, au vyote. Kuhusu ID hapa mara nyingi utategemea Tenders kwahiyo hata kama unayo ofisi lakini inabidi uingie mitaani au wilayani kutafuta tender, pens, teacups and plates hapa unaweza ukapata maharusi kuweka picha zao kwenye sahani etc au ukaongea na kampuni zikakupa matangazo yao ili uyaweke kwenye hizo pen

I hope kwa niliyosema hapo juu umegundua kwamba biashara yako haitegemei sana window shopping kwamba mtu hajui anachotaka katika pitapita zake alafu anaona kitu na kusema haa nakitaka hicho, which means utahitaji kufanya marketing and promotion na wateja wengine unaweza ukawa unawapata kwa kuwafuata maofisini kwao na kuwaonyesha sample (mfano printing kwenye pens) au ukipeleka sample ya printed sahani kwenye mikutano ya harusi, au tshirt printing ukiwatengenezea watu vizuri kwenye misiba au sherehe zao. IDs kazi ikiwa nzuri watu watakujua through word of mouth, na pia unaweza ukapeleka sample zako kwenye secretarial services ambapo utawapa comission kama wakikupatia mauzo.

Conclusively Choice between Dar and Mwanza depends na umahili wako and how big you want to be (can you fight with the big boys?, although you dont have to be big unaweza ukawa Dar lakini bado ukawa unatoa hizi huduma utapata tu, customer base) au Mwanza ambapo competition sio kali kama Dar kwahiyo ukiweza kuoffer better quality at a lower price then its fine, lakini the best scenario unaweza ukawa Dar alafu Mwanza ukawa una agents (watu wenye secretarial services) ukiongea nao ili wawe wanachukua orders na wewe unafanya kazi dar unawatumia alafu unawapa commission.

Kuhusu kupata mtu anayefanya hii biashara akuambia watu ni wachoyo kukwambia, the only way to find out ni wewe kujifanya mteja ili uende from different suppliers na uulizie bei zao na uangalie quality ya kazi zao alafu ufanye comparison na kazi yako, kumbuka kama nilivyosema usiogope kuanza.., start small utajifunza kwa makosa.., na hata kama hauna mashine zote still unaweza ukachukua kazi ukafanya kwa watu wenye mashine..., Nimeona umesema unazo heavy duty machines..., how heavy is heavy.., sababu kama una desktop printer ya kawaida inabidi ujue if it can handle mitikisiko ya kazi isije ikawa ni printer moja alafu katikati ya kazi inaalibika..., Kuhusu Glass and Plates hivi ni rahisi sana kuviuza sababu maharusi watapenda wawe na ukumbusho and its something unique.., kuhusu pens kama quality ni nzuri every company is potential customer unaweza ukaweka majina ya kampuni kwenye hizo pens..., kampuni nyingi zitakupa tender.[/quote]
 
Biashara ya stationery ni nzuri japo inategemea location (yaani mahali ilipo). Ukifanikiwa kuweka stationery karibu na taasisi ya elimu yaani shule/chuo uwezekano wa kulipa kwa haraka ni mzuri. Hata hivyo kama zilivyo biashara zingine itategemea unapata mzigo kwa bei gani na wewe utauza/kutoa huduma kwa bei gani kwani stioneries ni nyingi na bei za bidhaa zinatofautiana toka duka moja kwenda lingine.

Binafsi nina stationery Arusha lakini ilinichukua muda kuanza kupata faida. Mtaji wangu ilikuwa karibia mil 10 ila ni kwa sababu mimi niliweka internet cafe, photocopy machine, printing, lamination, scanning, na uuzaji wa stationeries zenyewe. vifaa na stationeries nilichukulia/nachukulia Arusha, japo naanza kuangalia uwezekano wa kuona kama naweza kuwa nachukulia Dar kutegemea gharama za usafiri.

Ukipata location nzuri na bei zako zikawa reasonable uwezekano wa kufanikiwa kwenye biashara hii ni mkubwa.
 
Nimewahi kufanya biashara ya stationery ni biashara nzuri but what real matters is the location of the busness.

kuuza kwa jumla na rejareja ni nzuri sana.

All the best!
 
Asante Mkuu,

This is valuable contribution.
Smarter biashara ya stationery ni nzuri japo inategemea location (yaani mahali ilipo). Ukifanikiwa kuweka stationery karibu na taasisi ya elimu yaani shule/chuo uwezekano wa kulipa kwa haraka ni mzuri. Hata hivyo kama zilivyo biashara zingine itategemea unapata mzigo kwa bei gani na wewe utauza/kutoa huduma kwa bei gani kwani stioneries ni nyingi na bei za bidhaa zinatofautiana toka duka moja kwenda lingine.

Binafsi nina stationery Arusha lakini ilinichukua muda kuanza kupata faida. Mtaji wangu ilikuwa karibia mil 10 ila ni kwa sababu mimi niliweka internet cafe, photocopy machine, printing, lamination, scanning, na uuzaji wa stationeries zenyewe. vifaa na stationeries nilichukulia/nachukulia Arusha, japo naanza kuangalia uwezekano wa kuona kama naweza kuwa nachukulia Dar kutegemea gharama za usafiri.

Ukipata location nzuri na bei zako zikawa reasonable uwezekano wa kufanikiwa kwenye biashara hii ni mkubwa.
 
Ni biashara nzuri ila kila biashara ina matatizo yake. Mimi binafsi narun biashara hyo hapa dar.ushauri wangu kwako ni huu

1. Ongeza mtaji kwani 3m ni ndogo sana itakusumbua kichwa
2.Baada ya kupata mtaji kama 15m na kuendela. Fanya yafuatayo:

- Tafuta frem ya biashara sehemu nzur mfano barabara yenye pilika nyingi,karibu na
chuo,mahakama,shule nk
- Tengeneza frem yako vizur ,milango ya alluminium na makabati yake,ac ndani,

Ukishafanya hayo 0713144200 kwa ushauri zaidi
 
Hii thread ni nzuri ikiwa utapata feedback kwa walionza biashara hiyo.

Mimi binafsi bado nina nia ya kuanzisha biashara hii na kilichonivutia zaidi ni kuwa nilikuwa nanunua vifaa vya ofisi pale Pran Pen Corner kwa kweli jamaa wanauza vitu in very reasonable price na kwa kuwa sasa nimehamia Tanga kimaisha ndio imenijia Idea hii ya kutaka kufungua biashara hii na kuwaweka wao kama main supplier wa vitu vingi vya stationery.

Mtaji bado unasumbua na kama nitapata feedback nzuri itanosaidia sana na nitapata mawazo mazuri zaidi jinsi ya ku approach biashara hii.

Tunasubiri michango yenu wana JF

Mkuu biashara kama hizi haziitaji mtaji mkubwa sana!
 
Naomba ushauri ndugu zangu ya kufungua biashara ya stationary mkoa wa songea je inalipa jaman tafadhali sana niambie kabla sijapoteza haka kapesa kangu kamkopo.
 
Biashara nyingi faida zake ni kati ya Tsh, 30/= na 300/=. Kama utapata sehemu (location) nzuri, bei zako zikawa si za KiTAMAA TAMAA, basi utatoka. Ukipata na Photo copy machine itakuwa nzuri sana. Ila zile card usizianike bila kuzifungia ndani ya nailoni kwani zitapauka. Ukipata na ka-kompyuta basi katakusaidia sana. Hongera
 
NAPENDA kutoa shukuran kwa wote ambao machango wao umenifanya nifanikiwe kufikia lengo langu la mwaka huu na sema ahsante sana na pia kwa wale ambao hawakusema kitu kwa sbb mbalimbali nami nawashukuru pia, nimefungua stationery songea karibu sana NA sokoni , stand pia karibu chuo cha sauti kinapo funguliwa.

Nazidi kuomba ushirikiano kwa kufanikisha biashara yangu, wan JF amani hakuna kinacho shindikana hapa dunia nawe unaweza weka nia utafanikiwa sana.

MUNGU AWABARIKI KWA KILA JAMBO UNALO FIKIRIA.

AHSANTEN SANA
 
Asante kushukuru. Jumamosi ntakuja hapo Makambi. Nikifika ntakuja kutoa photocopy.bei ni shilling ngapi?.mia
 
Kuna watu humu wanachukua points wanafanyia kazi wanatoka kimaisha, ila kuna wengine hawachangamki wanafanya masihara, kuna aidia niliichukua humu naifanyia kazia baada ya miezi miwili nitaleta report.

Mpendwa hongera sana
 
Mkuu hongera sana man. Just make sure your business inafika it's 1[SUP]st[/SUP] birthday and so on… A business, grows in cycles. It involves conceiving an idea, resource mobilization, start, growth and death. In short, a business is an invisible object, with the customer at its centre.

Poor or rich, an enterprise needs to attract customer's attention and, above all, their money. Just make sure you go with fast moving items (depending on demand) in order to keep your cash flow. Remember in business cash is power. Na mwisho watch your financial behavior.
 
wanan,

Hongera Sanaumedokeza karibu na Sauti wanafungua chuo songea.naomba kujua Wamejenga majengo mapya au wamekodisha? Naomba uniambie jina la mtaa, au street iliyokaribu na Sauti, nataka niangalie via Satalite map.Nimefika Songea 1996 mara ya mwisho.wanapokuja wanafunzi Chuo huwa kuna opportunities nyingine nyingi.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom