Naomba ushauri naumwa kuanzia shingoni hadi kifuani

Passed

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
561
156
Hii hali bado inaendelea kunisumbua kuanzia shingoni hadi kifuani panauma shingoni panakuwa kama pamejibana au kama mtu ameniviriga kamba kifua kuwaka moto na mgongo kuwaka moto pia na hii yote imesababishwa na msongo wa mawazo wa muda mrefu nina last chance ya kusoma maana nilishachezea nafasi nimepelekwa shule mara ya pili mawazo yananijia ya kukata tamaa ya kusoma hali ambayo napingana nayo kila siku niko vizuri tu kimasomo je nikijilazimisha lazimisha hii hali itapotea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana mkuu hali hii ilinikuta mwaka jana, nilikuwa na msongo sana wa mawazo hali iliyonipelekea kua na maumivu shingoni then yanakuja hadi kifuani...saivi kidogo afadhali japo kifua huwa kinauma nikiwa nimejikunja.

Bro. wangu ni Dr. alipatia dawa za antibiotic zilinisaidia japo niliacha kwa uvivu wa kutokuzimeza maumivu yalipungua kabsaaa.

lakin now yapo kidogo nampango wa kuendeleza dozi
 
Mawazo yanaleta stress na anxiety, mwaka 2013 niliumwa sana usiku nikiwa nimelala nilikuwa nasikia kizungu zungu na mwili kama unazima hivi nashindwa hata kunyanyua miguu au mikono ila najitaidi kuamka nashindwa najilazimisha mpaka hali inakata. Nilienda hospital moja inaitwa Family Care Dispensary iko upanga kwa professor Matuja, nikapima mpaka MRI. In short jitahidi sana usiwe mtu wa kuwa na mawazo

Mie naangalia movie na series za comedy na najitahidi kukaa na watu positiveili wasikupe stress. Huwezi kukwepa stress ndugu yangu ila unaweza kukaa mbali na vitu ambavyo vinakupa mawazo. Jitahidi mno kuepuka mambo ya kukutia mkazo kichwani na utapata amani na utakaa sawa pia. .
 
Kamuone daktari physician atakuhudumia!
Kuwahi ni vizuri kuliko kuchelewa!

Halafu soma Neno la Mungu hudhiria mafundisho itakusaidia sana.

Mfano hapo pamoja na mambo mengi ipo shida ya kujihesabia hatia!

Hapo adui anaweza kukukandamiza kupitia hiyo usitoboe kusonga mbele!

The past is like anchor that can stop you to sail to get what you expect!


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom