MJADALA: Je, Pikipiki gani ni bora kwa matumizi ya nyumbani au biashara kwa Tanzania?

mengi tumeshakutajia mkuu. humu unganisha fikra ufanye maamuzi yako. ukiendekeza kila kitu uambiwe mwishowe utakosa la kufanya.

mimi nimekupa yangu kama mzoefu kimatumizi toka 2003 hadi sasa natumia pikipiki, sina gari, mara chache naendesha ya wadau lkn naukubali utamu wa pikipiki kuliko gari tofauti na kero za mvua.

pia mafundi na wauzaji wameshabwaga yao.

ukichambua kwa umakini utagundua washauri wengi wanapendekeza umiliki aina walizo nazo bila kuzingatia vigezo vyako ulivyoainisha ktk main post. hivyo kazi ni kwako.

NYONGEZA:
service ya maana ni ku-fix lolote kabla hakijaleta madhara, ukisubiri sana ukaendeleza kutembelea tatizo huzaa mengine.
mf. upepo mdogo hichana tairi na kuvinba/kutunishwa nyaya au kupasuka au kukata nali.

oil rojorojo (zaidi ya km 1000) huchakaza/ziba filters na kuzalisha moshi au kuunguza piston rings, plugs kuungua na kukosa nguvu.

jenga mazoea ya kuhudumiwa na fundi mmoja kwa service ya uhakika labda ukiwa mbali naye kwa dharula.

jenga hulka ya kutomwamini fundi. asikununulie spea nunua mwenyewe yeye awe mfungaji. aghalabu wanakula na wenye maduka. unatozwa bei ya spea halisi anakufungia bomu ya bei chee anajilia chenji na huku unamlipa kabhour charges, ukitembea km chache unarudi kwake.

jenga tabia ya kujifunza kutambua hitilafu kabla ya kupeleka kwa fundi. wapo wanaobadili spea. mf unaenda kubadili rings za piston unamuachia chombo, anafungua plates au plugs zako org. anamufungia mteja mwingine. hii ni tabia ya mafundi wengi hasa watz ndio waizi waizi toka tumeacha kunyonya.

usimpe ovyo mtu baki usafiri wako. wewe ndiye unayejua thamani na umuhimu wa hicho chombo. wapiga norinda kwenye lami, wacheuaji na upanguaji wa fujo mara nyingi. vyombo si vyao-wamekodi. fikiria kwanini iwe ngumu kumkabidhi mtu hata memsahibhu pochi yenye 1,500,000 akushikie ukienda msalani lkn iwe nyepesi kumpa ignition key mtu. aburuze boxer yako uliyotolea 2.3m eti aisikilize!!

thamini vyako hata kama utasemwa au wakiona ni cha bei chini. wangapi hawana? A MAN BRAGS HIS PENIS HOWEVER TINY (usitafsiri kwa kiswahili hii sio mada ya Piston)
WEKK SAID BRO, na mimi humu kwa kweli nakusanya maoni ya watu wanaotoa ili nifanya maamuzi yangu..maana kila mtu anasema kwa experience yake but utaona tu zilizotajwa tu zote zinafaa.....
 
Umechoka na maisha? 😳

Habari za wakati huu wana JF, kama title inavyojieleza hapo juu;

A]
Nataka kununua pikipiki kwa ajili ya matumizi yangu binafsi na baadae kidogo kwa biashara. Hivyo naomba ushauri wa aina ya pikipiki itakayofaa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo;
1)mwonekano mzuri (mvuto)
2) injini kubwa (uwezo wa kuhimili milima -speed)
3)upatikanaji wa spear zake na bei nafuu
4)ubanifu wa mafuta (economical fuel consumption)
5)bei yake nafuu sana

KATI YA PIKIPIKI HIZI ( BOXER 150, TVS, HAOJUE /HONDA ACE, HERO, TANHERO)

NITOE USHAMBA TAFADHALI KTK HAYA
*Pia kati ya Boxer old model na New model ipo bora, na kwann?
*Boxer BM 150 na 125 ipi nzur/kubwa (injini)
*Je kuna boxer yenye gia 5 na ipi.?
* Hivi plate namba A inamaanisha chombo ni cha kitambo xana na uwezo/ubora wake ni mdogo ukilinganisha na namba B, C, na D,?
Mfano nikinunua chombo (gari au pikipiki kwa mtu Je ishu ya kubadilisha umiliki inakuaje?


#NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU KWAKO MWANA JF... %
 
Sasa hivi zipo za kutosha
Duuh kama ni hvyo kwel bas inaweza kuwa best kwenye mafuta...... Lakin napata wakati mgum napowaza Upatikanaji wa Spear parts zake mana inasemekana kutoka kwa watumiaji kuwa ni adim sana had Nairobi mana nipo Moshi... Wenye tvs kwa observation yang naona ni wachache kuliko wenye boxer na nyinginezo
 
hiyo block nini kitu gani mkuu
1129201


Hii ndio block. Na katikati hapo ndio kunakuwa na piston.
Watu wengi wanakosea sana kwenye suala la service ya hizi pikipiki, matokeo yake huwa zinawasumbua sana na kusingizia ubovu wa pkpk kumbe ni umakini tu
 
Hata ukitaka kwa matumizi binafsi hiyo ni wewe tu.
Hizi ni kati ya pkpk imara za mchina na bado hazijachakachuliwa sana na wajanja. Kama sanlg zilivyoingia zilikuwa imara sana lkn wajanja wakaanza kuchakachua sahv zinauzwa kwa sababu ya jina tu
sawa mdau
 
Back
Top Bottom